Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo IKULU. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo IKULU. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 4 Juni 2012

KIKWETE ATEMBEA MITAA YA ARUSHA HUKU AKIFANYA MAZOEZI, WANANCHI WAFURAHISHWA.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliye katika mapumziko mafupi jijini Arusha, akiwa katika mazoezi yake ya kutembea kilomita tatu kila asubuhi na jioni kabla ya kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. Wakaazi wengi wa Arusha ambao wamemuona akitembea wamesisimkwa na kufurahishwa sana na hatua hiyo ya kiongozi mkuu wa nchi kuwa mstari wa mbele katika kujenga afya kwa mazoezi ya kila siku, na kutaka kila mtu, si viongozi tu, kuiga mfano wake.PICHA NA IKULU.
 
Mkuu wa Nchi akiwapeleka puta wasaidizi wake wakati wa mazoezi ya jioni akiw amapumzikoni huko Arusha hivi karibuni, safi sana Mkubwa nasi pia tunaanza leo.

Jumamosi, 31 Desemba 2011

BALOZI SEFUE AMEAPISHWA LEO IKULU KUSHIKA WADHIFA MPYA WA UKATIBU MKUU.

Hapa Balozi akisubiri shughuli za kuapishwa zianze rasmi.

Rais Jakaya M. Kikwete akimwapisha Balozi Ombeni Sefue kuwa Katibu Mkuu leo asubuhi Ikulu Dar es Salaam.

BALOZI OMBENI SEFUE ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU KIONGOZI, KUMRITHI LUHANJO.

Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi mpya, kabla ya kuteuliwa alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Jumamosi, 17 Septemba 2011

RAIS KIKWETE AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA MIKOA IKULU LEO ASUBUHI


 Rais Dkt. Jakaya Kikwete , akimwapisha Mwantum Bakari Mahiza, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo asubuhi katika Viwanja vya Ikulu Dar. Katikati ni Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo.



Rais Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wake, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiteta jambo baada ya kuwaapisha wakuu wa mikoa Ikulu,jijini Dar es Salaam leo.



Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete amewaapisha wakuu wa mikoa aliowateua hivi karibuni.Sherehe za kuwaapisha wakuu hao wapya wa mikoa imefanyika leo asubuhi katika viwanja vya ikulu jijini Dar es Salaam.Pichani ni Mkuu mpya wa Mkoa wa Tabora. Bi.Fatuma Mwassa akila kiapo mbele ya Rais Dkt. Jakaya Kikwete na kukabidhiwa miongozo ya kazi. 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Leonidas Tutubert Gama, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro
 
Rais Dkt. Jakaya Kikwete, akimwapisha Fabian Inyasi Massawe, kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Kikwete, Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, wakiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Mikoa walioteuliwa kushika nyadhfa hizo baada ya kuwaapisha katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Viwanja vya Ikulu Dar es Salaam leo, asubuhi.