Jumatatu, 4 Juni 2012

KIKWETE ATEMBEA MITAA YA ARUSHA HUKU AKIFANYA MAZOEZI, WANANCHI WAFURAHISHWA.


Rais Jakaya Mrisho Kikwete, aliye katika mapumziko mafupi jijini Arusha, akiwa katika mazoezi yake ya kutembea kilomita tatu kila asubuhi na jioni kabla ya kufanya mazoezi ya viungo na kuingia gym, katika kuuweka mwili wake katika hali ya ukakamavu na afya. Wakaazi wengi wa Arusha ambao wamemuona akitembea wamesisimkwa na kufurahishwa sana na hatua hiyo ya kiongozi mkuu wa nchi kuwa mstari wa mbele katika kujenga afya kwa mazoezi ya kila siku, na kutaka kila mtu, si viongozi tu, kuiga mfano wake.PICHA NA IKULU.
 
Mkuu wa Nchi akiwapeleka puta wasaidizi wake wakati wa mazoezi ya jioni akiw amapumzikoni huko Arusha hivi karibuni, safi sana Mkubwa nasi pia tunaanza leo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni