Jumapili, 3 Juni 2012

MBUNGE WA BAHI CCM AKAMATWA KWA RUSHWA YA MILIONI MOJA.

Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel
Neville Meena na Fidelis Butahe

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi wa Serikali.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo zinaeleza kuwa Badwel alikamatwa na maofisa wa Takukuru jana saa 9:00 alasiri katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Badwel ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) anadaiwa kukamatwa wakati anapokea rushwa kutoka kwa maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani jana.

Mfungo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa wanaendelea kumshikilia huku wakati wanafanya uchunguzi hadi kesho ambapo watamfikisha mahakamani.

“Siwezi kumtaja aliyekuwa akitoa rushwa kwa sababu bado tunaendelea na upelelezi, ila mpaka sasa yuko mahabusu na tutamfikisha mahakamani Jumatatu(kesho),” alisema Mfungo.

Alisema kuwa mbali na kumfikisha mahakamani, pia watatoa taarifa zaidi za tukio hilo kesho.
SOURCE; Mwananchi via Kapinga's blog.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni