Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ADUI WA HAKI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo ADUI WA HAKI. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 16 Juni 2013

DK. HOSSEAH WA TAKUKURU AFUNGUKA, ASEMA TAKUKURU INATENGWA NA SERIKALI.


Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah 

Dodoma. Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah, amefunguka na kueleza sababu za taasisi yake kushindwa kuwakamata walarushwa wakubwa kwa kuwa Serikali imemfunga mikono.
Akitoa majumuisho katika Mkutano Mkuu wa Chama cha Wabunge Wanaopambana na Rushwa nchini (APNAC) jana, Dk Hoseah alisema kuwa Serikali imeitenga Takukuru na kuwafanya waishi kama yatima.
Huku akishangiliwa na idadi kubwa ya wabunge, mkurugenzi huyo alisema kuwa amekuwa akishangazwa na lawama ambazo amekuwa akibebeshwa kila wakati kuwa ameshindwa kumaliza rushwa wakati bila kuziangalia sheria.
“Mnanipa lawama kila wakati, lakini huwezi kuanzisha chombo kama Takukuru halafu ukamfunga mikono mhusika, na mimi mmenifunga mikono nifanyeje jamani? Alihoji na kuongeza:
“Hata katika rasimu ya Katiba bado mmetutenga kama watoto yatima, wenzetu wote mmewaweka tena hata CAG mmesema kuwa mamlaka yake akiteuliwa basi asiingiliwe wala kuhojiwa…mamlaka gani mtu asihojiwe jamani, mimi nikiuliza Takukuru mnasema subirini Serikali ya Tanganyika.”
Gazeti la Guardian la Uingereza la Jumapili ya Desemba 19, 2010, lilitoa taarifa ya siri kuhusu wala rushwa wakubwa kulindwa Tanzania. Gazeti hilo lilichapisha taarifa za mtandao wa WikiLeaks uliokuwa ukimilikiwa na mwandishi wa habari wa Australia, Julian Paul Assange, ukimnukuu Dk Hoseah.
Dk Hoseah alinukuliwa na WikiLeaks akimueleza mwanadiplomasia wa Marekani aitwaye Purnell Delly, Julai 14 jijini Dar es Salaam mwaka 2007 kuhusu uwezo na nia ya Rais Kikwete katika kushughulikia ufisadi.
Alidai Rais Jakaya Kikwete alikuwa anakwamisha kuchunguzwa kwa vigogo wa Serikali wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa, na pia anahofia maisha yake kama mkuu wa Takukuru. Hata hivyo, Dk Hoseah kwanza alikiri kukutana na ofisa huyo ofisini kwake Julai 2007, lakini alikanusha kuzungumza kuwa Rais Kikwete alikuwa hataki sheria ichukue mkondo wake katika kuwachunguza vigogo wanaotuhumiwa kwa rushwa.
Atoa ushauri kwa Serikali
Kwa mara ya kwanza jana kiongozi huyo aliitolea uvivu Serikali kuwa imekuwa ikichangia mambo mengi katika rushwa ikiwamo usiri mkubwa katika rasilimali za nchi.
“Lazima Serikali iwe wazi, huwezi kuwaficha wananchi rasilimali zao eti ni siri kwa sababu ya sera mbovu, tunawaambia wananchi watanufaika na mirabaha ya asilimia tatu hiyo siyo sahihi jamani ndiyo maana tunashindwa kutoa majibu kwa wananchi wetu hilo ni tatizo jingine linalosababisha mambo ya rushwa,”alisema na kuongeza: “Siyo kila jambo ambalo serikali inapewa ushauri ni baya.”
Alipinga kitendo cha viongozi kuwa na kigugumizi katika uwajibikaji na akataka itungwe sheria kali ya kutaka kiongozi awajibike mara anapokuwa ametuhumiwa kwa jambo lolote aachie ngazi na kupisha uchunguzi kama ilivyo kwa nchi zingine.
Credits; Gazeti la Mwananchi

ELIMU YA NAMNA YA KUEPUKA RUSHWA KWA SEKTA YA AFYA WILAYANI NACHINGWEA.

Wadau wa sekta ya Afya toka maeneo mbalimbali ya wilaya ya Nachingwea wakiwa katika majadiliano ya njia za kujiepusha na adui rushwa hivi karibuni, mafunzo haya yalitolewa katika ukumbi wa TRC mjini Nachingwea na maafisa wa TAKUKURU(hawapo pichani).

Wanafunzi wa mwaka wa kwanza katika Chuo cha Uuguzi Nachingwea wakisikiliza maelekezo ya Maafisa wa TAKUKURU  juu ya mapambano dhidi ya rushwa na uundaji wa Klabu za Wapinga Rushwa Vyuoni na mashuleni.

Jumamosi, 29 Septemba 2012

JALADA KESI YA VIGOGO JKT LIPO KWA DPP.

James Magai
JALADA la kesi ya maofisa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wanaokabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya ofisi za umma, limekwama kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.Kesi dhidi ya maofisa hao saba waandamizi wa JKT, iko katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa SUMA JKT ambaye ni mmoja wa washtakiwa Kanali Ayoub Mwakang'ata kulia mwenye suti nyeupe.

Maofisa hao ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Uzalishaji Mali la jeshi hilo (Suma JKT), Kanali  Ayoub Emu Mwakang’ata na Mkuu wa Miradi, Luten Kanali Felix Andrew Samillani.
Wengine ni  Luteni Kanali Mkochi Chacha Kichogo, Luteni Kanali Paul Andrew Mayavi , Meja Peter Mabulla Lushika, Sajenti John Andrew Laizer na Meja Yohana Leonard Nyuchi.
Kesi hiyo ilitarajiwa kuanza kusikilizwa jana, katika hatua za awali ambapo washtakiwa wangesomewa maelezo kuhusu mashtaka yanayowakabili.

Hata hivyo ilikwama kutokana na kutokuwapo kwa jalada lao mahakamani.
Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Tabu Mzee, alidai kuwa jala la kesi hiyo bado liko kwa DPP, na akaomba mahakama ipange tarehe nyingine ya kuwasomea washtakiwa maelezo ya awali.

Hakimu Aloyce Katemana alikubaliana na ombi hilo na kupanga maelezo hayo yasomwe  Oktoba 26 mwaka huu.
Hii ni mara ya pili kwa vigogo hao wa JKT kushindwa kusomewa mashtaka kutokana na jalada la kesi yao kuitwa na DPP.
Awali, mahakama ilipanga washtakiwa hao wasomewe maelezo hayo  Agosti 30 mwaka huu, lakini ilishindikana kutokana na jalada la kesi kuitishwa na DPP.

Hatua hiyo ilimlazimisha mwendesha mashtaka huyo wa Takukuru kuomba kesi ipangiwe nyingine na mahakama ikapanga jana.

Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani  Julai 2 mwaka huu na kusomewa mashtaka saba yakiwemo ya kula njama na kuhamisha zaidi ya Sh3 bilioni kinyume cha sheria.

Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Donasian Kessy akisaidiana na Ben Lincoln, alida kuwa washtakiwa walitenda makosa hayo kwa nyakati tofauti.
Kessy alidai kuwa walitenda makosa hayo wakati wakipitisha uamuzi wa ununuzi wa magari na vifaa vya ujenzi chakavu, kula njama na kuhamisha mabilioni ya fedha kinyume cha masharti ya kifungu cha 156 cha kanuni za Fedha za Umma za mwaka 2001.

Akifafanua mashtaka hayo, katika shtaka la kwanza, Kessy alidai kuwa Machi 5, 2009 washtakiwa wote wakiwa ni wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Suma JKT, kwa makusudi walitumia vibaya madaraka yao kwa kupitisha uamuzi wa kununua magari ya mtumba na vifaa vya ujenzi vilivyotumika.

Alidai kuwa walitenda hayo bila mamlaka ya Bodi ya Wakurugenzi wa Takopa. Takopa ni muungano wa kampuni mbili za ujenzi ya Korea  zilizoingia ubia na  Suma JKT

Jumanne, 25 Septemba 2012

MAPAMBANO DHIDI YA RUSHWA YAMNASA HAKIMU.

HAKIMU WA ILALA ASOMEWA MASHTAKA YA RUSHWA KISUTU.

Hakimu na Rushwa                                                                    

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala Pamela Kalala (kushoto),akitoka katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana,baada ya kusomewa shitaka la kuomba rushwa ya Shilingi milioni tatu.Picha na Michael Matemanga

Jumatano, 11 Julai 2012

HUKUMU KESI YA MAHALU KUTOLEWA LEO KISUTU.

Mkapa
Profesa Mahalu (kushoto) akiwa na Wakili wake  Bw. Marandu mapema mwezi Mei 2012 wakati Mh. Rais msataafu Benjamin William Mkapa alipotoa ushahidi mahakamani akimtetea Mtuhumiwa na mwenzake. Leo hii asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu itatolewa hukumu ya shauri hili lililochukua takribani miaka mitatu kukamilika.

Ijumaa, 15 Juni 2012

TAKUKURU LINDI YAFANYA MKUTANO NA MAHAKIMU WAKAZI WA WILAYA NA MKOANI LINDI.


Hakimu Mkuu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa Lindi Bw. Ndunguru(katikati) akiwa pamoja na Mratibu wa NACCSAP  wa Lindi Bw. Kuhanda (kushoto) na Bi. Lilian, Hakimu Mkazi Lindi wakisikiliza hoja mbalimbali za mkutano huo ulioitishwa na TAKUKURU Lindi ili kubadilishana uzoefu juu Uendeshaji kesi Mahakamani. Mkutano ulifanyika majuma mawili yaliyopita Ukumbi wa Takukuru Lindi


Wajumbe wa Mkutano huo wakimsikiliza Mh. Ndunguru akitoa mada yake juu ya Wajibu wa Mahakimu na Waendesha Mashtaka katika kutoa Haki.


Mafunzo yakiendelea.


Mahakimu Wakazi na Waendesha Mashtaka wakisikiliza

Jumapili, 3 Juni 2012

MBUNGE WA BAHI CCM AKAMATWA KWA RUSHWA YA MILIONI MOJA.

Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel
Neville Meena na Fidelis Butahe

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inamshikilia Mbunge wa Jimbo la Bahi (CCM), Omary Badwel kwa tuhuma za kupokea rushwa ya Sh1 milioni kutoka kwa kiongozi wa Serikali.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkurugenzi wa Upelelezi wa taasisi hiyo, Alex Mfungo zinaeleza kuwa Badwel alikamatwa na maofisa wa Takukuru jana saa 9:00 alasiri katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam.

Badwel ambaye ni mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) anadaiwa kukamatwa wakati anapokea rushwa kutoka kwa maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani jana.

Mfungo aliliambia Mwananchi Jumapili kuwa wanaendelea kumshikilia huku wakati wanafanya uchunguzi hadi kesho ambapo watamfikisha mahakamani.

“Siwezi kumtaja aliyekuwa akitoa rushwa kwa sababu bado tunaendelea na upelelezi, ila mpaka sasa yuko mahabusu na tutamfikisha mahakamani Jumatatu(kesho),” alisema Mfungo.

Alisema kuwa mbali na kumfikisha mahakamani, pia watatoa taarifa zaidi za tukio hilo kesho.
SOURCE; Mwananchi via Kapinga's blog.

Jumanne, 8 Mei 2012

WATUHUMIWA SABA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KESI YA RUSHWA HUKO SAME.

Bw. Edward Hosseah, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU.
Omary Magongo, Same
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) imewafikisha watu saba katika mahakama ya Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro kwa tuhuma za udanganyifu,  ubadhirifu na matumizi mabaya ya madaraka.


Washtakiwa waliofikishwa mahakamani mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Gabriel Kurwijira,  ni Diwani wa Kata ya Vumari, Joseph Kateri na aliyekuwa Ofisa mtendaji wa kata hiyo, Dawson Daniel.

Wengine ni aliyekuwa Mkuu wa Sekondari ya Vumari, Johnson Misheto, Mwenyekiti wa bodi ya sekondari hiyo, Mchungaji mstaafu, Moses Tezura, Mwalimu Agnes Makundi, Mjumbe wa bodi, Ernest Mbike na mfanyabiashara Upendo Abraham, anayemiliki duka la vifaa vya ujenzi la Nashy Hardware wilayani hapa.

 Akisoma hati ya mashtaka mahakamani hapo, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Susan Baltazar, alisema washtakiwa kwa pamoja kati ya Januari na Juni 2008 wilayani hapa, walikula njama na kutenda kosa kwa kutumia nyaraka zenye maelezo ya uongo kumdanganya mwajiri wao kuwa Nashy Hardware alikuwa ameuzia vifaa vya ujenzi sekondari, jambo ambalo halikuwa kweli.

Baltazar alidai kuwa katika kipindi hichohicho, Misheto, Tezura, Daniel, Kateri na Mbike katika Sekondari ya Vumari, kwa makusudi walitumia vibaya madaraka yao kwa kuruhusu mfanyabiashara Nashy Hardware kulipwa kwa madai kuwa ameuzia shule vifaa vya ujenzi wakati haikuwa kweli, hivyo kusababisha ubadhirifu wa mali ya umma.

Katika kosa la tatu, ambalo linawahusu Misheto, Makundi na Abrahamu, wanatuhumiwa kutumia nyaraka za uongo kuwa wamepokea vifaa zilizothibitisha kuwa Nashy Hardware alikuwa amevifikisha shuleni hapo.
Washtakiwa hao ambao walikwamisha mradi wa ujenzi wa nyumba ya mwalimu, wanadaiwa kutenda makosa hayo kinyume na vifungu namba 22,31 na 32 vya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Washtakiwa wote wanadaiwa kuingizia Serikali hasara ya zaidi ya Sh13.4 milioni, walikana mashtaka na wako nje baada ya kutimiza masharti  kwa kuwa na mtu mmoja wa kuaminika na kusaini hati ya thamani ya Sh5 milioni.

Hata hivyo, Mshtakiwa Mbike alishindwa kukidhi masharti ya dhamana na kupelekwa rumande. Kesi iliahirishwa hadi Mei 16, mwaka huu itakapotajwa tena

Jumatano, 28 Machi 2012

TAKUKURU NACHINGWEA YAHAMASISHA WANAMICHEZO KUPAMBANA NA RUSHWA MICHEZONI.

Kaimu Kamanda wa TAKUKURU wilayani Nachingwea Nd. Zablon Ernest Ombory akiongea na viongozi wa Chama cha Mpira wa miguu wilayani Nachingwea (NAFA), wachezaji wa timu ya African Boys ya Rwangwa naTimberland almaarufu Kipande cha Ulaya ya Nachingwea pia waamuzi wa mchezo huo juu ya umuhimu wa michezo na mapambano ya rushwa michezoni kabla ya mechi kuanza katikati  ya mwezi huu.
Mgeni Rasmi akikagua wachezaji na waamuzi kabla ya mechi kuanza.

Mwenyekiti wa NAFA akiwaongoza wageni kurudi jukwaa kuu ili kuangalia burudani ya mchezo ambao uliishia kwa timu ya Timberland ya Nachingwea kuifunga African Boys 3-2. Waamuzi walikuwa Ndg. Chacha( kushoto) mwamuzi wa kati, Ndg. Ashomile na Malebo wakishika vibendera na Kamisaa toka Lindi.
Wageni jukwaani toka kushoto ni Afisa utamaduni wilaya ya Nachingwea Ndg. Mkungwi, Mweka Hazina wa NAFA Ndg. Nyoni, Kaimu Kamanda TAKUKURU Ndg. Ombory, Afisa wa TAKUKURU Ndg. Hassan na Hakimu Mfawidhi Mh. Hemela.
Wachezaji wa Timberland wakiwa mapumzikoni.

Wachezaji wa African Boys ya Rwangwa wakiwa mapumzikoni.

Jumatano, 7 Machi 2012

ASKARI POLISI WAWILI WAFUKUZWA KAZI BAADA YA KUDAI RUSHWA.

Askari hao wamefukuzwa kazi kwa kubainika kutenda kosa ambalo ni kinyume na utendaji kazi wa jeshi hilo ambalo walidai fedha hizo kutoka kwa Jacqueline Komba ili waweze kumuonyehsa gari lake lililokuwa limeibiwa na majambazi

Askari waliofukuzwa kazi akiwemo Koplo David na Koplo Lufefe wote wa jeshi hilo na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela.

Januari 16 mwaka huu Jacqueline aliripoti katika kituo cha polisi cha Chuo Kikuuu kuibiwa gari lake aina ya Suzuki Swift lililokuwa na namba za usajili T311 BWU alikuwa ameliegesha karibu na eneo la Swimming Pool chuoni hapo.

Kamanda wa Kenyela alisema, baada ya siku moja Komba alipigiwa simu na askari mmoja kutoka kituoni hapo kumtaka atoe kiasi cha shilingi Milioni 3 ili wamuonyeshe gari lake lilipo na yeye akawaomba kuwa amepungukiwa na kuwaahidi kuwapa kiasi cha shilingi Milion 2.5 na askari hao wakakubali na kumuahidi aje siku iliyofuata yaani Januari 19 wakutane eneo la Mlimany City wakachukue fedha hizo

Jaqueline aliweza kuripoti kituo kingine cha UIrafiki na mtego uliwekwa na watuhumiwa hao waliweza kukamatwa Februari 7, mwaka huu


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela.