Jumanne, 19 Julai 2011

PAMOJA NA KUANDALIWA KABURI LAKE ZURI HUKO KIJIJINI KWAKE,MZEE MANDELA AFIKISHA MAKA 93.

Happy birhday Mandela. 


Nelson Rolihlahla Mandela, Rais wa zamani wa Afrika Kusini jana aliadhimisha mwaka wa 93 wa kuzaliwa kwake akiwa pamoja na jamaa na marafiki huko kijijini kwao Zunu huku wananchi wa Afrika Kusini wakiungana kwa nyimbo na huduma za kijamii na shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Mamilioni ya wanafunzi wa shule waliimba nyimbo ya kumpongeza Mandela kwa kutimiza miaka 93 huku salamu za pongezi zikimiminika kutoka kila kona ya dunia.
Mwaka 2009 Umoja wa Mataifa ulizindua rasmi Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela kwa heshima ya shujaa huyo wa Afrika wakati alipoadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa huduma za kijamii.
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitumia fursa hiyo ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Nelson Mandela kwa kutoa mwito kwa walimwengu wabadilike na wajibidiishe kusomesha watoto, kuwalisha wenye njaa na kujitolea katika huduma za hospitali na jumuia za kijamii

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni