Jumatano, 13 Julai 2011

WASANII WAOMBA MSAADA.



Baadhi ya wasanii wa kundi la Fish Group
Wednesday, July 13, 2011 5:01 AMKUNDI la sanaa za maigizo na filamu nchini la Fish Group linasaka wadhamini ili kuendelea kukuza vipaji vya wasanii wachanga na kuinua tasnia ya filamu nchini.
Wakiongea na Kalimanzila wa Nifahamishe.Com ofisini kwao Magomeni jijini Dar es Salaam, jana viongozi wa kundi hilo, Hamis Yusuph na Juma Mwamwindi ‘Stopa’ walisema kuwa wanasaka wadhamini hao kwa kuwa mpaka sasa tayari wameishawaandaa vijana kwa kiwango kikubwa kwenye sanaa.

Viongozi hao walisema kwamba kundi hilo limefanikiwa kuwaokoa baadhi ya vijana wa mtaani toka kwenye matendo mbalimbali ya uhalifu.

“Lengo letu ni kukuza vipaji na kuendeleza sanaa hivyo tunaomba wadau kujitokeza na kutupa tafu ya kuendeleza gurudumu hili mpaka sasa tunajiendesha wenyewe bila wadhamini” alisema Mwamwindi ‘Stopa’.

Mpaka sasa kundi hilo linawasanii 64 na linanolewa na walimu wazoefu wakiwemo Hamad Abdala ‘Mr.Eddo na Mode ambao ni wasanii wazoefu kwenye tasnia hiyo.

Aidha waliongeza kuwa, malengo yao zaidi ni kuhakikisha mbali na sanaa ya maigizo na filamu pia wanataka kuwa na kundi la ngoma na sarakasi.

Kwa upande wake mkuu wa nidhamu wa kundi hilo, Ramadhan Shaban ‘Max well’ alisema kuwa wamepata faraja kwa wazazi wa wasanii waliojiunga na kundi hilo kuwaunga mkono kwa kuwaruhusu watoto wao kufanya sanaa tofauti na zamani ambapo sanaa ilionekana kama uhuni.

“Tunajisikia faraja wazazi kuikubali sanaa hivyo Tanzania tunakoelekea soko litakuwa zaidi ni kushirikiana kwa pamoja” alisema Max.

Max aliongeza kuwa kama mtu atakuwa tayari kulidhamini kundi hilo basi anaweza kuwasiliana nao kwa simu hizi 0652513951 au 0719302000 ama anaweza kufika ofisini kwao Magomeni Mapipa, kituo cha mabasi cha Mapipa mkabala na Shibam Restaurant

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni