Jumapili, 3 Julai 2011

WALIOGOMA UDOM KUCHUJWA, WASIO NA MAKOSA NDIO WATAKAORUDI.

WANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha D o d o m a (Udom) waliosimamishwa masomo, hawawezi kurudi wote, imeelezwa.

Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Phillipo Mulugo, amesema Serikali ya Awamu
ya Nne si ya kuchezewa na kwa kuanzia, wanafunzi waliosimamishwa watachujwa na
watakaorejea ni wale tu wasio na makosa.

Alisema hatua kali zitachukuliwa kwa watakaobainika kuwa viongozi wa migomo chuoni hapo ili liwe funzo na onyo kwa wanafunzi wengine.

“Wale waliogoma hatuwezi kuwarudisha wote, tunataka kuonesha kuwa Serikali ipo na si
ya kuchezewa,” alisema Mulugo katika hafla ya chakula cha usiku walichoandaliwa wanafunzi 20 waliofanya vizuri katika mtihani wa kidato cha sita juzi.

Naibu Waziri aliwataka wanafunzi hao kuhakikisha kuwa wanapokwenda vyuoni waepukane na migomo, kwani ina athari kubwa kwa masomo kama ilivyotokea kwa wanafunzi wa Udom.

“Migomo haina tija kwenu,” alisema Mulugo katika hotuba yake na kuongeza kuwa
sheria za chuo ziko wazi hivyo ni jukumu la kila mwanafunzi kuhakikisha anazifuata.

Alisema kitendo cha Serikali kuwaenzi wanafunzi hao ni lazima wakikumbuke katika maisha
yao, kuwa Serikali yao inawajali, hivyo hawapaswi kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu.

Naye Waziri wa Tamisemi ambaye Wizara yake iliandaa hafla hiyo, George Mkuchika, alisema
Serikali inaangalia uwezekano wa kuweka zawadi kubwa ya Waziri Mkuu ambayo itamwezesha mwanafunzi bora asomeshwe chuo kikuu bure

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni