Jumamosi, 30 Julai 2011

WANAWAKE WAJIHADHARI NA MUUAJI WA WANAWAKE GESTI.



Wanawake jihadharini na mwanaume huyu


Friday, July 29, 2011 2:19 AM
WANAWAKE wa jiji la Dar es salaam mnatakiwa kuwa makini na macho na hasa kupunguza tamaa za kimwili na mali kwa kuwa amejitokeza mwanaume mmoja anayenyonga wanawake mara amalizapo kufanya nae mapenzi imedaiwa.
Mwanaume huyo inasemekana ni mmoja ambaye hadi sasa ameshanyonga wanawake wapatao saba na wa saba ni mwanamke aliyekuwa mke wa mwanamziki wa kundi la Taarabu la Five Star aitwae Issa Kamongo(pichani-Farida) mazishi yake yaliyofanyika juzi Bunju

Kutokana na kukua kwa idadi ya wanawake wanaonyongwa kuongezeka siku hadi siku wanawake wanatakiwa kuwa makini na mwanaume huyu anayenyonga wanawake kwa sababu ambayo haijafahamika hadi sasa

Mwanaume huyu inasemekana anapendelea sana wake za watu, wanawake weupe na wenye mvuto na kisha kumrubuni kuingia nae nyumba ya wageni’gest’ na kisha kumnyonga mwanamke huyo na kumlaza kifudifudi na yeye kutimka

Mwanaume huyo anahisiwa kuwa ni mmoja kwa mujibu wa mashuhuda wanaomuona aingiapo na wanawake ambapo maelezo ya wahudumu wa gesti wanapokufa wanawake huwa yanafanana

Wasifu wa mwanaume huyo anadaiwa kuwa ni Mweupe, mzuri wa maumbile na sura yaani Handsome’ na anapendelea kuvaa kofia aina ya kep

Jana mwanamke mmoja aliweza kuongea ndani ya Redio na kukiri ni kweli mwanaume huyo yupo, na ameshawahi kukatana nae maeneo ya ubungo na mwanaume huyo alimwita kwa lengo la kumuuliza amsaidie kwa kuwa eneo hilo yeye ni mgeni na mwisho akaanza kumrubuni na kumtaka aende nae kwenye msitu wa Chuo Kikuu

Amesema walishaanza safari na mwanamke huyo wakati akiongea nae machale yakamcheza na alijisikia kama haongei na mwanadamu wa kawaida na mwili kuwa kama umekufa ganzi na ghafla mwanamke huyo alimwambia amuache kwanza kuna kitu amesahau pale alipotoka na kumuahidi angerudi na ndipo alipoponea kwenye tundu la sindano

Hata hivyo inahisiwa kuwa huenda mwanaume huyo hutumia pia nguvu za giza kuwapata wanawake hao kwa kutojielewa.

Awali mwanzoni mwa mwezi Juni, jeshi la polisi lilishatoa tahadhari kwa wanawake na kuahidi kumsaka mwanaume huyo lakini bado hajakamatwa na kutangazwa

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni