Jumatano, 13 Julai 2011

MWANAUME AKATWA UUME HUKO MAREKANI.



Kieu Becker
Wednesday, July 13, 2011 10:52 PMStaili ya wanawake kuwaadhibu wapenzi wao kwa kuzikata sehemu zao za siri imeendelea nchini Marekani ambapo mwanamke mmoja nchini humo amejikuta akitupwa rumande kwa kuukata kwa kisu uume wa mume wake na kisha kuusagasaga kwa mashine.
Mwanamke mmoja wa California nchini Marekani amejikuta akitupwa rumande baada ya kumlisha madawa ya kulevya mumewe, kumfunga kwa kamba na kisha kuukata uume wake kwa kisu na ili kuhakikisha kipande hicho cha uume hakitaungwa tena na madaktari alikidumbukiza kipande hicho cha uume kwenye mashine ya kusaga uchafu.

Taarifa ya polisi ilisema kwamba siku ya jumatatu usiku, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Kieu Becker mwenye umri wa miaka 48, alimuandalia mumewe chakula ambacho alikiwekea madawa ya kulevya.

Mumewe mwenye umri wa miaka 51 ambaye jina lake halikutajwa, alijihisi vibaya baada ya kula chakula hicho na haukupita muda mrefu alipoteza fahamu.

Kieu alimburuza mumewe na kumlaza kitandani ambapo alimvua nguo zake zote na kisha kuifunga mikono na miguu yake kwenye kitanda.

Kieu alisubiri mumewe apate fahamu kabla ya kuanza kumshambulia kwa kisu chenye urefu wa sentimita 25.4.

"Alikuwa ameishazinduka wakati uume wake ulipokatwa", alisema msemaji wa polisi.

Taarifa ya polisi ilisema kwamba Kieu alikichukua kipande cha uume wa mumewe na kukiweka kwenye mashine ya umeme ya kusaga taka ambayo huwekwa chini ya sinki la maji kwenye majumba mengi ya Marekani.

Baada ya kuhakikisha kipande hicho cha uume kimesagwasagwa sana kiasi cha kuwa vipande vidogo vidogo, Kieu alipiga simu polisi na kuwajulisha kilichojiri. Polisi walipofika walimkuta mumewe akiwa bado kitandani mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwa kamba, alikuwa akivuja damu sana.

Kieu alitupwa rumande akifunguliwa mashtaka ya kufanya ukatili, kuteka mtu na kumlewesha mtu kwa madawa ya kulevya ili kufanya kosa la jinai. Ili aachiwe huru kwa dhamana, Kieu alitakiwa kutoa dola milioni moja.

Mume wa Kieu aliwahishwa hospitali ambapo alifanyiwa operesheni ili kuokoa maisha yake. Ingawa hali yake bado ni mbaya sana, madaktari wanaamini mwanaume huyo atapona.

Kieu hakuleta upinzani wowote wakati alipokuwa akitiwa mbaroni na atapandishwa kizimbani siku ya jumatano.

Taarifa zaidi zilisema kwamba Kieu na mumewe walifunga ndoa mwezi disemba mwaka jana na walikuwa kwenye harakati za kuivunja ndoa yao ingawa sababu ya mgogoro kwenye ndoa yao haikujulikana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni