Jumanne, 19 Julai 2011

MREMBO AHAIDI KUVUA NGUO KUSHANGILIA USHINDI WA PARAGUAY

Mrembo Kusaula Nguo Kushangilia Ushindi wa Timu ya Taifa


Larissa Riquelme
Tuesday, July 19, 2011 1:10 AMMacho ya washabiki wa soka wa nchini Paraguay yameelekezwa kwa mrembo maarufu nchini humo ambaye aliahidi kusaula nguo zake zote iwapo timu yake ya taifa ingevuka hatua ya robo fainali ya kombe la Copa America.
Mrembo wa nchini Paraguay, Larissa Riquelme aliahidi kumwaga radhi hadharani katika kushangilia timu yake ya taifa iwapo timu hiyo itavuka hatua ya robo fainali ya kombe la Copa America.

Hivi sasa macho ya washabiki wa soka wa nchini Paraguay yameelekezwa kwa Larissa kwani timu ya taifa ya Paraguay imeweza kuvuka hatua ya robo fainali baada ya kuibugiza Brazil mabao 2-0 kwa penalti na kuitupa nje ya mashindano ya Copa America.

Katika mechi hiyo iliyoamuliwa kwa penalti baada ya mechi kuisha sare ya 0-0, Brazil ilikosa penalti zote nne ilizopiga wakati Paraguay iliweza kuzamisha kimiani penalti mbili kati ya tatu ilizopiga.

Wakati Paraguay ikijiandaa kupambana na Venezuela siku ya jumatano kwenye mechi ya nusu fainali, washabiki wa soka wanasubiri kuona kama Larissa atatimiza ahadi yake.

Larissa aliwahi kutoa ahadi kama hiyo wakati wa kombe la dunia nchini Afrika Kusini mwaka jana, lakini kwakuwa Paraguay haikufika mbali hakulazimika kuitimiza ahadi yake.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni