Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HAPPY BIRTHDAY. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo HAPPY BIRTHDAY. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 22 Desemba 2011

HAPPY BIRTHDAY MAMBOBADO!!!!!! BLOG YATIMIZA MWAKA MMOJA TANGU IANZISHWE, HONGERA KWA WADAU WOTE WANAOTEMBELEA HAPA KWA KUTENGENEZA JAMII YETU ILIYOSIMAMA IMARA.

Kama mtoto huzaliwa na kisha baadae kukua na kupitia hatua kadhaa za mabadiliko, basi kijiwe chetu kilianza hivyo mwaka mmoja uliopita kama sehemu binafsi ya kujifurahisha kwa mitundiko ya nyumbani na marafiki zetu, lakini baadae kikakua na kujumuisha mambo mengi ya kijamii.
Shukurani kwenu wote mliobahatika kuona kijiwe hiki kwa njia yoyote ile na kufanya wengi zaidi Duniani kote wakifahamu na kuongeza idadi ya kurasa zinazofunguliwa na kufanya jamii yetu ikue kwa kasi, wachache kati yao si vibaya nikiwataja Kamanda Phili wa Manyanya wa kule bondeni kwa Madiba, Pastor Kalu toka Mbeya, Dada Yasinta(Kapulya Mdadisi) akiwa na shemeji yetu huko Ughaibuni, Simon Kitururu Mzee wa Falsafa ndani ya Neno, Israel Saria wa BBC, Emu Three, Rehema Fussi wa Dar, Flora Talent, Michuzi mkubwa.
Huyu dogo anaitwa Omari, naye ni mdau maana huwa anapenda kushika vifaa vyangu vya kazi na kunifanya nimbembeleze aache ili niendelee na kazi, Maoni yenu ni muhimu ili kuboresha Kijiwe chetu, mwisho tumshukuru Mungu kwa kutupa uwezo wa kuendeleza mambo yetu tunayoyapenda mpaka tukafanikiwa hivi. 
Kamanda Hansom Omari akiwa katika pozi anatafakari, nimechelewa kuweka maelezo haya sababu ya shida ya umeme huku kwetu mikoa ya Lindi na Mtwara, tusameheane,tupo pamoja msijali,Tchao.

Jumanne, 19 Julai 2011

PAMOJA NA KUANDALIWA KABURI LAKE ZURI HUKO KIJIJINI KWAKE,MZEE MANDELA AFIKISHA MAKA 93.

Happy birhday Mandela. 


Nelson Rolihlahla Mandela, Rais wa zamani wa Afrika Kusini jana aliadhimisha mwaka wa 93 wa kuzaliwa kwake akiwa pamoja na jamaa na marafiki huko kijijini kwao Zunu huku wananchi wa Afrika Kusini wakiungana kwa nyimbo na huduma za kijamii na shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi.
Mamilioni ya wanafunzi wa shule waliimba nyimbo ya kumpongeza Mandela kwa kutimiza miaka 93 huku salamu za pongezi zikimiminika kutoka kila kona ya dunia.
Mwaka 2009 Umoja wa Mataifa ulizindua rasmi Siku ya Kimataifa ya Nelson Mandela kwa heshima ya shujaa huyo wa Afrika wakati alipoadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kutoa huduma za kijamii.
Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitumia fursa hiyo ya maadhimisho ya siku ya kuzaliwa Nelson Mandela kwa kutoa mwito kwa walimwengu wabadilike na wajibidiishe kusomesha watoto, kuwalisha wenye njaa na kujitolea katika huduma za hospitali na jumuia za kijamii

HAPPY BIRTHDAY SOPHIA

Sofia akicheza kiduku mbele ya babake katika kusheherekea siku ya kuzaliwa kwake nyumbani kwao Mabibo Luhanga jumapili iliyopita,urithi wa mtoto ni elimu baba, mpe haki yake.

Jumatatu, 10 Januari 2011

HAPPY BIRTHDAY TO YOU

Happy birthday mkubwa
09/01 

 Maisha ni malengo na juhudi zinahitajika,usikate tamaa




 Mtu na dadaye
Mdau ameshaanza kuzeeka
Baba na mwana