Jumatano, 27 Aprili 2011

UBABE WA MADEREVA WA MAGARI YA SERIKALI USIKU.

Gari hili aina ya Land Cruiser(Mkonga) namba SM 3992 likiwa barabarani maeneo ya Sinza Kamanyola usiku wa tarehe 19-04-2011 lilisababisha ajali kwa makusudi pale dereva wake alipolikwaruza kwa makusudi Daladala(Hiace) namba zimehifadhiwa, hali iliyosababisha vioo vya pembeni kuvunjika na kujeruhi baadhi ya abiria. Alipoulizwa dereva huyo wa Cruiser kulikoni avunje vioo vya daladala lenye abiria ndani, alijibu yeye hana kosa hivyo hakuwa na namna nyingine ya kutovunja vioo, tumlaumu dereva wetu wa daladala. Hata hivyo ukweli ni kuwa dereva wa daladala aliomba apewe nafasi aingize gari lake lakini dereva wa cuiser alibana kwa makusudi.

 HUU NI UBABE USIO NA TIJA  HASA UKIZINGATIA GARI ILIYOHUSIKA NI YA UMMA NA SIJUI KAMA WANA KIBALI CHA KUTUMIA GARI USIKU, PIA WALIONEKANA WAMELEWA DEREVA NA ABIRIA WAKE. WANANCHI WALIOKUWEPO WALIKASIRISHWA SANA NA KITENDO HICHO, ACHENI UBABE NA MPATE VIBALI VYA KUTUMIA MAGARI HAYO KWA MAMBO YENU BINAFSI.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni