Jumamosi, 16 Aprili 2011

HAKI ZA BINADAMU ZIPO WAPI?



J
 Huyu jamaa ambaye kwa sasa ni marehemu alikamatwa kaiba viti vya plastiki kanisani huko Mbeya, hakufikishwa katika vyombo vya sheria, badala yake aliteswa na kuuawa na kama vile haitoshi alichomwa moto bila kujali kuwa ni binadamu kama sisi. Jamani jambo hili linafaa kweli japo mwizi,tutafika kweli iwapo mtu akituhumiwa tu kwa jambo basi auawe? Nawaasa binaadamu wenzangu tuwe na subira kwenye mambo kama haya japo najua kuwa kuibiwa kunaumiza na kurudisha maendeleo ya mtu nyuma. Je hawa mafisadi wangeletwa mbele yetu japo kwa dakika tano itakuwaje,maana wao ni wezi wakubwa.


 

Moto unaanza kukolea
Jamaa anateswa (picha kwa hisani ya kalulunga.blogspot.com)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni