Jumapili, 17 Aprili 2011

HAKI ZA BINADAMU ZIPO KWELI JAMANI?

Yule kijana wa Kigamboni aitwae Lillah ambaye juma lilopita alilipotiwa kuchomwa moto huko south beach kigamboni amefariki dunia jana na anatarajiwa kuzikwa leo huko mjimwema kigamboni. Matukio haya ya watu kujichukulia sheria mkononi nimeyazungumzia sana na tunaona madhara yake yanavyojionesha. Lillah yeye alikamatwa na walinzi wa south beach kwa tuhuma za kuzamia disco bila kuwa na tiketi, akapelekwa kwa meneja wa hoteli ambaye aliamuru achomwe moto na amri ikatekelezwa kwa kumwagiwa petroli na kupigwa kiberiti, alikimbilia baharini na baadae wasamalia walimpeleka hospitali kigamboni akaamishiwa muhimbili, amefariki jana,ameacha mke na watoto. Meneja na walinzi wawili  walikamatwa, sijui kama waliachiwa, TUNAOMBA SHERIA ICHUKUE MKONDO WAKE NA HAKI IONEKANE KUWA IMETENDEKA. Buriani Lillah. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni