Alhamisi, 12 Januari 2012

MESSI AIBUKA MCHEZAJI BORA WA DUNIA MWAKA 2011.


Lionel Messi ameshinda tuzo ya Fifa ya mwanasoka bora wa mwaka 2011 ya Ballon d'Or, na kuwa mchezaji wa nne katika historia duniani kushinda tuzo hiyo mara tatu. Mshambuliaji huyo kutoka Argentina mwenye umri wa miaka 24, aliwashinda Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na mchezaji mwenzake wa Barcelona, Xavi.  Kocha wa Manchester United Sir Alex Ferguson alishinda tuzo ya huduma kwa soka, huku meneja wa Messi, Pep Guardiola akipata tuzo ya kocha bora wa mwaka. Messi, ambaye aliwahi pia kushinda tuzo hiyo yenye hadhi mwaka 2009 na 2010, alikuwa mchezaji bora katika mechi ya fainali ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka 2011, dhidi ya Manchester United, na pia alishinda ligi ya Uhispania, kombe la Supercopa la Uhispania, Kombe la Uefa Super Cup na Kombe la Dunia la klabu mwaka jana

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni