Alhamisi, 26 Januari 2012

WIZARA YA ARDHI YAMSHUSHUA JUSSA





NewsImages/6214910.jpg
Tibaijuka akifafanua jambo
Mtandao wa ippmedia unaripoti kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka, amemshushua kwa kuweka wazi kuwa mpango wa Tanzania kuuomba Umoja wa Mataifa (UN).
Kuiongezea maili 150 sawa na kilometa 241.5, kutoka usawa wa mwambao wa Tanzania, haukufanywa na wizara yake peke yake bali una baraka zote za Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar.

Profesa Tibaijuka alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa ameshangazwa na taarifa zilizotolewa katika vyombo mbalimbali vya habari vilivyoripoti kwamba Serikali ya Tanzania imefanya makosa kuandaa, kupeleka maombi ya kutaka kuongezewa mipaka ya eneo tengefu la bahari kuu (EEZ) bila kuishirikisha Zanzibar.

“Hili suala sijaliamua mimi wala wizara yangu peke yake, lakini nashangaa taarifa zilizotolewa kwenye vyombo vya habari kwamba nimefanya makosa, nisingeweza kwenda mimi bila Mkuu wa nchi kujua na kukubali. Pia tulikuwa na ujumbe kutoka Zanzibar tuliokwenda nao kwa hiyo nashangaa wanaosema hatujashirikisha Zanzibar,” alisema.

Profesa Tibaijuka alisema Tanzania iliingia mkataba na Serikali ya Norway katika kufadhili mradi huo ambapo kulikuwa na wawakilishi kutoka Zanzibar. Aliwataja wawakilishi hao kuwa ni Ayoub Mohamed Mahmoud, ambaye alisema alishiriki kikamilifu katika ziara ya Norway na alipewa nafasi ya kuongea kwa niaba ya SMZ na Zakia Meghji.

“Kwa hiyo madai ya Chama cha Wananchi (CUF) kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar haikushiriki au kushirikishwa hayaendani na yaliyojiri na hayana ukweli wowote,” alisema Profesa Tibaijuka

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni