Jumatano, 21 Desemba 2011

NEWS ALERT!!!!!! JIJI LA DAR LAKUMBWA NA MAFURIKO MABAYA ASUBUHI HII, MAGARI YA SAFARI ZA MIKOANI YAKWAMA HUKO MBEZI BAADA YA DARAJA MOJA KUFURIKA MAJI HADI JUU YA NJIA, MABIBO RELINI HAKUPITIKI, MAGARI YASOMBWA,WANANCHI WACHUKUE TAHADHARI.

Wananchi wa eneo la Jangwani Dar es salaam wakiwa barabarani wakikimbia nyumba zao ambazo ziliingiliwa na mafuriko ya maji jana kutokana na mvua zinazonyesha kuanzia jana hadi leo, maafa ni makubwa

Wananchi wa Jangwani Magomeni wakijaribu kuokoa baadhi ya vifaa baada ya mafuriko kuzidi, pembeni kuna mkokoteni uliosheheni taka na kutelekezwa hapo, Idara ya Afya ijidhatiti kwa lolote maana magonjwa ya mlipuka yanaweza kutokea, poleni sana.
(Picha kwa hisani ya issamichuzi blog)

PICHA ZAIDI
Eneo la Jangwani
Gari ya Zimamoto bila kujua ilipita kwenye barabara iliyojaa maji kumbe daraja limekatika.
Harakati za uokoaji.
Jangwani haifai tena na si eneo salama la kuishi, poleni waathirika wote.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni