Ijumaa, 9 Desemba 2011

JE UNAMJUA VIZURI MNYAMA PORI AITWAE KIBOKO!? SOMA TABIA ZAKE HAPA UELIMIKE.


Viboko hutumia muda mwingi wa siku kwa kukaa ndani ya maji. Hii inatokana na ukweli kwamba ngozi yake haina uwezo wa kupambana na mikimiki ya jua. Huwa wanatoka nje kwa ajili ya kutafuta chochote baada ya jua kuzama. Picha juu ni moja ya mapito ya viboko ambayo tulikutana nayo wakati wa game walk ndani ya pori la akiba la Selous. Inakoelekea njia hiyo ndipo ulipo mto Rufiji.
Kutokana na hali ya kuwa na himaya, ni jambo la msingi sana kwa kiboko kujua ilipo himaya yake ili asijikute kaingia kwenye himaya ya mwingine na kuzua mgogoro wa himaya. Ndio maana viboko wanakuwa na tabia ya kuweka alama kwenye mapito yao kwa kutumia haja kubwa ili kuweza kujua njia ya kuweza kumfikisha kwenye eneo lake mtoni au bwawani. Picha juu ni kinyesi cha kiboko ambacho amekitapanya kwenye mti ikiwa ni kama alama yake ya barabarani kumuonyesha njia ya kufuata kwenda malishoni na kurudi mtoni.
"Kamwe usiombe kukutana nae akiwa njiani kurudi mtoni halafu na wewe ukawa umesimama kwenye njia yake bila kujua" Hayo yalikuwa ni maneno ya guide wetu siku hii akitutahadharisha hatari za kukutana na kiboko uso kwa uso. Viboko huwa anakosa imani anapokuwa nje ya maji kwana hujiona yeye ndio mvamizi. mara nyingi anapohisi tishio lolote yeye huanza kutafuta njia ya kurudi mtoni kwenye himaya yake. Kwa mantiki hiyo hataweza kuruhusu jambo lolote limzuie ktk barabara yake kwa namna yoyote ile. Ikitokea wewe ndio umesimama kwenye njia yake basi utapewa kikumbo ambacho kinaweza kukupa majeraha ya kudumu kama sio kuondoa uhai wako.

Hii ni sehemu nyingine kwenye njia yao ambayo nayo walikuwa wameweka alama zao



Wote huweka alama, lakini zinakuwa ni tofauti kidogo

Viboko Dume hutawanya kinyesi chao kwa mkia ktk eneo ambalo anaweka alama yake ya kufuata anaporudi bwawani.

Kiboko jike huweka alama, lakini kwakuwa yeye sio mmiliki wa eneo alama zake huwa anazishora chini. Huwa hatapanyi kwa mkia kama vile ambavyo dume anafanya. ktk picha mbili hizi utaona kuna aina moja ya 'mzigo' umetupwa chini wakati mwingine umerushwa mpaka kwenye matawi ya mti ulio pembeni. Ni baadhi ya mambo unayoweza kujionea kwa ukaribu na kujifunza unapoamua kufanya game walk safari.
Chanzo cha habari na picha;tembeatz.blogspot.com

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni