Jumapili, 25 Desemba 2011

MSONDO NA SIKINDE WAKO KWENYE MPAMBANO MKALI USIKU HUU, NANI ATAIBUKA MKALI!!!?

Nani zaidi kati ya Msondo na Sikinde leo?

Na Mwandishi Wetu
Bendi kongwe nchini Msondo Ngoma Music na Mlimani Park Orchestra “Sikinde Ngoma ya Ukae”
zinatapambana leo (Krismasi) mchana hadi usiku wa manane kwenye viwanja vya TCC Club Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Pambano hilo ambalo tayari limevuta hisia za mashabiki wa muziki wa dansi imeandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment chini ya udhamini wa Konyagi.
Onyesho hilo pia ni maalum kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Krisimasi ambapo wapenzi wa muziki watajumuika kwa pamoja kwenye viwanja hivyo kufurahia kumalizika kwa mwaka.
Bendi hizo ambazo zina mashabiki wengi nchini kuliko bendi nyingine zozote, zimeahidi kutowaangusha mashabiki wao kwa kila moja ikijinasimu kuwa itaibuka na ushindi.
Mara nyingi bendi hizo zikipambana huwa ni patashika nguo kuchanika, kwani mbali na mashabiki kushangilia bendi wanazozipenda vibweka na vituko kemkem vimekuwa vikitawala.
Sikinde ambayo iliweka kambi jijini Dar es Salaam imejinasibu kuibwaga Msondo na kudai kuwa hivi sasa haitishi kama ile ya miaka kadhaa iliyopita.
Itakuwa ni mara ya kwanza bendi hizo kupambana Wilayani Temeke na pia sikukuu ya Krisimasi tangu zianzishwe

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni