Jumanne, 27 Desemba 2011

MSONDO NA SIKINDE WAPAGAWISHA MASHABIKI MKESHA WA XMASS CHINI YA UDHAMINI WA KONYAGI

Mpambano huo ulivuta mashabiki wengi katika viwanja vya TCC Sigara ambapo bendi ya Sikinde, ilionekana kuwapiku wenzao wa Msondo kutokana na Shamrashamra zilizokuwa zikitawala wakati Msondo wakiimba jukwaani, Onyesho hilo limefanyika usiku wa kuamkia jana ikiwa ni pamoja na kusherehekea sikukuu ya Krismas.
Wanamuziki Shaban Dede na TX Moshi William Junior wa Msondo wakiimba jukwaani huku mashabiki wakiwashangilia kwelikweli wakati wa onyesho hilo lililofanyika TCC Chang'ombe usiku wa kuamkia jana.
TX Moshi William Junior akiimba katikati ya mashabiki , huku mashabiiki hao wakimshangilia.
Kutoka kulia ni mwimbaji wa Bendi ya Sikinde Hassan Kunyata, Yusuph Bernald na Shaban Lendi wapiga Saxaphone wakifanya vitu vyao jukwaani.
Mwimbaji wa bendi ya Sikinde Abdallah Hemba akicheza sambamba na wanenguaji wa bendi hiyo wakati bendi hiyo ilipotupa karata yake ya mwisho usiku wa kuamkia leo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni