Jumapili, 18 Desemba 2011

AVUNJA REKODI YA MSICHANA MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI.

Msichana mfupi kuliko wote duniani


NewsImages/6129114.jpg
Bibie Jyoti Amge akichukuliwa vipimo vya urefu wake.
Mwanafunzi wa Kihindi, Jyoti Amge, ni msichana aliyevunja rekodi ya dunia ya msichana mfupi kuliko wote duniani, kwa mujibu wa rekodi inayosajiliwa na kitabu cha rekodi cha Guinness.
Runinga ya NBC ya Marekani, siku ya Ijumaa 17/12/2011, imeripoti kuwa Jyoti Amge mwenye umri wa miaka kumi na minane 18, ana urefu wa sentimeta 62.8. sawa na inchi 24.7. Kwa hiyo msichana huyo ndio msichana mfupi kuliko wote duniani akiwa amempita msichana wa Kimarekani Bridgette Jordan mwenye umri wa miaka ishirini na miwili 22, ambaye ana urefu unaovuka ule wa Jyoti Amge kwa sentimeta saba 7. Kwa mujibu wa habari hiyo, Bridgette Jordan, alikuwa anashikilia rekodi hiyo tangu Septemba 2011.

Siku ya Ijumaa, Bibi Jyoti Amge, alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa katika jiji la Nagpur. Wakati huo huo amenukuliwa akisema “Furaha ilioje kwa kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka kumi na minane 18 nikishika rekodi mpya. Kwa kweli tukio hili ni zawadi ya nyongeza kwa sherehe ya kuzaliwa kwangu.”

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni