Jumanne, 17 Mei 2011

ZOMBE AIDAI FIDIA SERIKALI

Monday, 16 May 2011 20:57

Nora Damian
MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, ameiomba Mahakama Kuu ya Tanzania, itupilie mbali kesi ya madai ya fidia ya Sh5 bilioni, iliyofunguliwa na aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abdallah Zombe (57).

Mwanasheria huyo kupitia kwa wasaidizi wake pia umeiomba mahakamani imwamuru Zombe kulipa gharama zote za kesi hiyo.Zombe amefungua kesi ya madai ya fidia ya Sh5 bilioni dhidi ya serikali kwa madai ya kunyanyaswa, kudhalilishwa, kumbakiwa kesi na kukiuka kwa haki zake za sheria na kikatiba.
Ndg. Abdallah Zombe

Mpelelezi huyo ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wanne wa madini kutoka Ulanga, mkoani Morogoro, alifungua kesi hiyo hivi karibuni kupitia kwa wakili wake Richard Rweyongeza. Katika majibu ya upande wa Jamhuri yaliyowalishwa mbele ya Jaji Upendo Msuya, umeiomba mahakama itupile mbali madai hayo kwa kuwa si ya msingi.

Upande huo umedai kuwa Zombe alishtakiwa kihalali na kwamba hata sasa bado kuna kesi katika Mahakama ya Rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu.Jaji Msuya amepanga Mei 23 mwaka huu kuwa siku ya mdai kuwasilisha majibu yake dhidi ya serikali na kesi hiyo itatajwa tena Juni 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya madai, Zombe ametoa sababu 21 za kufungua kesi hiyo akidai fidia ya Sh5 bilioni na riba ya Sh200 bilioni. Anadai kuwa polisi ilikiuka sheria ya makosa ya jinai ya mwaka 2002, inayotaka mtu kabla ya kukamatwa, aelezwe za sababu kukamatwa na kufikishwa katika kituo cha polisi ambako anapaswa kuhojiwa.

Zombe alitaja sababu zingine za kufungua kesi hiyo kuwa ni pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Said Mwema, kushindwa kulijibu kusudio lake la kuishtaki serikali hata baada ya kutoa notisi ya siku 90.Anadai kuwa Septemba 27 mwaka jana, alikabidhi barua ya kusudio la kufungua kesi kwa IGP-Mwema na ilionyesha kupokelewa na kiongozi huyo, lakini hakujibu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni