Jumamosi, 21 Mei 2011

KAHAWA YAPUNGUZA UWEZEKANO WA KANSA YA KIBOFU.

Utafiti unaonyesha wanaume wanaokunywa kahawa kwa wingi wana nafasi nzuri ya kuepuka kensa ya tezi la kibofu cha mkoj
Anyalem Barayes prepares to conduct a traditional Eritrean coffee service.
Picha; VOA. Kahawa ni kinywaji kikubwa katika nchi za Afrika Mashariki na Ethiopia.

"wanaume wanaokunywa vikombe sita au zaidi vya kahawa kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata kensa hiyo kwa asilimia 60 ukilinganisha na wanaume wasiokunywa kabisa kahawa."
Utafiti mpya uliofanywa kwa kushirikisha wanaume elfu 50 unasema kuwa watu wanaokunywa kahawa kwa wingi wana nafasi nzuri ya kuepukana na saratani au kensa ya tezi la kibofu cha mkojo.
Kwa muda wa zaidi ya miaka 20 kumekuwa na imani kuwa unywaji kahawa unasaidia katika kuepusha kensa hiyo, lakini katika tafiti huu mpya wanasayansi wanasema wamegundua tofauti kubwa katika kuepusha saratani kali.
Mwanasayansi Kathryn Wilson wa Idara ya afya ya umma ya chuo kikuu cha Havard nchini Marekani anasema "wanaume wanaokunywa vikombe sita au zaidi vya kahawa kwa siku wanapunguza uwezekano wa kupata kensa hiyo kwa asilimia 60 ukilinganisha na wanaume wasiokunywa kabisa kahawa."
Kahawa ina kemikali mbali mbali, ikiwa na viambatisho vinavyopambana na magonjwa na hiyo huenda ni pamoja na kemikali zinazozuia kensa ya tezi la kibofu cha mkojo.
Kensa hiyo ni ya pili kwa kuuwa wanaume duniani, ikiwa inasababisha vifo vya watu wapatao robo millioni kwa mwaka.
Dr. Wilson na wenzake walichapisha matokeo ya utafiti wao katika jarida la kisayansi la "Journal of the National Cancer Institute."

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni