Alhamisi, 12 Mei 2011

ULIPUAJI MABOMU GONGOLAMBOTO WACHELEWESHWA TENA.

Wananchi wakiangalia mabaki ya mabomu.


JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa mara nyingine limeahirisha ulipuaji wa masalia ya mabomu hadi hapo itakapotangazwa tena.Taarifa ya JWTZ kwa vyombo vya habari ilisema jana kuwa ulipuaji huo uliokuwa ufanyike leo hautafanyika, lakini haikueleza sababu za shughuli hiyo kusogezwa tena mbele.

"Ulipuaji huo wa masalia ya mabomu hautafanyika tena leo ... Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania linapenda kuwasihi wananachi wote kuendelea kusikiliza vyombo vya habari hadi hapo taarifa za ulipuaji wa masalia zitakapotolewa tena," iliseme sehemu ya taarifa hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa JWTZ kuahirisha ulipuaji wa mabomu hayo

Hivi karibuni JWTZ ilitangaza kulipua mabomu hayo kila siku kuanzia saa moja asubuhi hadi saa sita mchana kwa wiki nzima, lakini shughuli hiyo ikaahirishwa bila kutolewa sababu zozote.

Februari 16, mwaka huu mabomu yalilipka katika maghala 23 kwenye kambi ya Gongolamboto na kusababisha vifo vya watu 27 na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa, huku wengine wakikosa makazi.MAJIRA.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni