Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MABOMU. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo MABOMU. Onyesha machapisho yote

Alhamisi, 12 Mei 2011

ULIPUAJI MABOMU GONGOLAMBOTO WACHELEWESHWA TENA.

Wananchi wakiangalia mabaki ya mabomu.


JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa mara nyingine limeahirisha ulipuaji wa masalia ya mabomu hadi hapo itakapotangazwa tena.Taarifa ya JWTZ kwa vyombo vya habari ilisema jana kuwa ulipuaji huo uliokuwa ufanyike leo hautafanyika, lakini haikueleza sababu za shughuli hiyo kusogezwa tena mbele.

"Ulipuaji huo wa masalia ya mabomu hautafanyika tena leo ... Jeshi la Ulinzi la wananchi wa Tanzania linapenda kuwasihi wananachi wote kuendelea kusikiliza vyombo vya habari hadi hapo taarifa za ulipuaji wa masalia zitakapotolewa tena," iliseme sehemu ya taarifa hiyo.

Hii ni mara ya pili kwa JWTZ kuahirisha ulipuaji wa mabomu hayo

Hivi karibuni JWTZ ilitangaza kulipua mabomu hayo kila siku kuanzia saa moja asubuhi hadi saa sita mchana kwa wiki nzima, lakini shughuli hiyo ikaahirishwa bila kutolewa sababu zozote.

Februari 16, mwaka huu mabomu yalilipka katika maghala 23 kwenye kambi ya Gongolamboto na kusababisha vifo vya watu 27 na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa, huku wengine wakikosa makazi.MAJIRA.

Jumatano, 11 Mei 2011

JWTZ KULIPUA MASALIA YA MABAKI YA BARUTI LEO NA KESHO HUKO GONGOLAMBOTO.

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatarajia kufanya uteketezaji wa mabaki ya mabomu na baruti yaliyotokana na mlipuko katika kambi ya Jeshi ya Gongolamboto.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya JWTZ, ilisema kuwa uteketezaji wa mabomu hayo utafanyika Mei 11 na 12 majira ya saa 3 hadi mchana katika kambi hiyo.



Taarifa hiyo ilisema kuwa masalia hayo yatawaka moto mkali lakini kutakuwa na utaratibu maalumu kwa kupishana kwa saa kadhaa katika ili kuacha kuwashitua wananchi.

Ilisema kuwa uchomaji wa masalia hayo hayana madhara yoyote ya kuweza kuharibu mazingira ya watu katika maeneo yaliyo karibu na kambi hiyo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa wananchi wanatakiwa kuacha wasiwasi juu moto ambao unatokana na uchomaji huo

Ijumaa, 6 Mei 2011

WAHAMA WAKIHOFIA ULIPUAJI WA MABOMU KAMBI YA JESHI GONGOLAMBOTO.

Thursday, May 05, 2011 12:29 PM
BAADHI ya wakazi wa Gongo la Mboto walilazimika kuhama kwa kuogopa zoezi la ulipuaji wa mabaki ya mabomu katika kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Gongolamboto na kurejea makazi yao jeshi hilo lilipotangaza kusitisha zoezi hilo.



Nyumba iliyoharibiwa na mabomu
Moto unaishia

Makamanda wakiangalia mabaki ya mabomu.
Wakazi hao waliondoka kwenye makazi hayo kwa hofu ya kulipukiwa na mabomu hayo kama awali japo jeshi hilo limetangaza kuwa hakutakuwa na athari yoyote kwa wakazi hao.

Jumatatu ya wiki hii jeshi hilo lilitangaza kumalizia kulipua masalia ya mabomu katika kambi hiyo na zoezi hilo kuahirishwa jana na kutangazwa.

Taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari wa JWTZ zilidai kuwa walipanga kulipua mabomu hayo ndani ya kambi hiyo kwa kuhofia kuyalipua kwa kuyabeba kuyahamishia mahali pengine kwani kwa  kufanya hivyo kungeweza kuleta madhara makubwa.

Februari 16, mwaka huu, katika ghala la kambi ya Gongolamboto mabomu yalilipuka na kusababisha vifo vya watu 30 na wengine zaidi ya 300 kujeruhiwa huku wakazi wengine kukosa makazi na wengine kuharibiwa mali zao na mifugo.

Jumanne, 8 Machi 2011

GONGOLAMBOTO

WALIOKUFA GONGOLAMBOTO KULIPWA TSH. 8.5 KILA MMOJA.

Serikali imesema ipo tayari kulipa kifuta machozi cha shilingi milioni 8.5 kwa kila aliyekufa kwa milipuko ya mabomu katika kambi ya JWTZ Gongolamboto, Dar es salaam. Idadi kamili wa waliokufa kwa sasa ni 29 baada ya watu wengine wawili kuongezeka hiyo juzi.
Kadhalika shule 10 na zahanati zilizoharibika kwa milipuko hiyo, zitaanza kujengwa na Jeshi la Kujenga Taifa ili ziendelee kutoa huduma. Kaimu Mkuu wa Mkoa amewaomba wafiwa waharakishe utaratibu wa kupata wasimamizi wa mirathi mahakamani na hatimaye walipwe kifuta machozi chao.
Shule tatu kati ya kumi zilizoharibiwa zimepata wahisani wa kuzijenga upya ambazo ni sekondari ya Pugu itakayojengwa na Taasisi ya Shree Hindu Mandal, Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) shule moja na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) litajenga moja na saba zilizobaki zitajengwa na SUMA JKT.