Jumatano, 11 Mei 2011

JWTZ KULIPUA MASALIA YA MABAKI YA BARUTI LEO NA KESHO HUKO GONGOLAMBOTO.

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatarajia kufanya uteketezaji wa mabaki ya mabomu na baruti yaliyotokana na mlipuko katika kambi ya Jeshi ya Gongolamboto.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya JWTZ, ilisema kuwa uteketezaji wa mabomu hayo utafanyika Mei 11 na 12 majira ya saa 3 hadi mchana katika kambi hiyo.



Taarifa hiyo ilisema kuwa masalia hayo yatawaka moto mkali lakini kutakuwa na utaratibu maalumu kwa kupishana kwa saa kadhaa katika ili kuacha kuwashitua wananchi.

Ilisema kuwa uchomaji wa masalia hayo hayana madhara yoyote ya kuweza kuharibu mazingira ya watu katika maeneo yaliyo karibu na kambi hiyo.

Taarifa hiyo ilisema kuwa wananchi wanatakiwa kuacha wasiwasi juu moto ambao unatokana na uchomaji huo

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni