Jumapili, 22 Mei 2011

MAUAJI NCHINI SOMALIA

Mogadishu:
Makruti wa Jeshi la Somalia wakiwa mafunzoni nchini Uganda
Askari Wanafunzi
Bildunterschrift: Makruti wa Jeshi la Somalia wakiwa mafunzoni nchini UgandaWatuwasiopungua 14 wameuwawa kufuatia mapambano makali kati ya wapiganaji wa Kiislamu na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika (AMISOM) katika soko la Bakara mjini Mogadishu, Somalia.
Mkuu wa huduma za dharura mjini humo, Ali Muse, amesema makombora yaliyovurumishwa kwenye soko hilo, yaliwajeruhi pia raia wengine zaidi ya 60.
Naye msemaji wa AMISOM, Paddy Ankunda, alisema Jumatatu wiki hii kwamba wanajeshi wa Uganda na Burundi walioko Mogadishu, waliazisha kampeni mpya mapema mwezi huu kuyalenga maeneo yanayodhibitiwa na kundi la Al-Shabbab. Ankunda alisema kwa sasa AMISOM inadhibiti asilimia 60 ya mji mkuu wa Mogadishu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni