Jumapili, 27 Mei 2012

ZANZIBAR HALI SI SHWARI TENA, KANISA LA ASSEMBLIES OF GOD LACHOMWA MOTO, SERIKALI YAZUIA MIKUSANYIKO YOYOTE.

Kumbe Zanzibar tatizo si muungano bali udini?Baada ya polisi wa kupambana na ghasia kutunishiana mikono na kundi la JUMIKI au Jumuia ya Uamsho na  Mihadhara ya Kiislamu kanisa la Tanzania Assembly of God (TAG) la mtaa wa Kariakoo Zanzibar limechomwa usiku wa kuamkia leo. Je hii ni bahati mbaya au kuna ushirika wa kundi hili linaloanza kutishia amani ya nchi? Tunaambiwa watu wasiojulikana wamechoma kanisa hili. Je kweli waliochoma hawajulikani wakati dalili zote zinaelekea kwa JUMIKI? Kuna haja ya serikali kuwa serious na kundi hili ambalo lina kila alama za kigaidi. Hata Al Shabaab ilianza hivi. Maana bado kuna wendawazimu wanaodhani nchi inaweza kutawaliwa kidini. Hii si karne ya saba na kumi na nne.Je tatizo la Zanzibar ni muungano au udini

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni