Alhamisi, 17 Mei 2012

SIMBA SC YAFIWA NA MCHEZAJI WA KIMATAIFA PATRICK MAFISANGO USIKU WA KUAMKIA LEO.


Mchezaji Patrick Mafisango,amefariki dunia alfajiri baada ya gari alilokua anaendesha kupata ajali. Alikuwa akitoka Club Maisha yeye na rafiki zake ambao wamenusurika katika ajali hiyo.

Picha mbili za gari namba T387BMZ alilokuwa akiendesha Marehemu Mafisango baada ya kupata ajali leo alfajiri.(Picha kwa hisani ya GPL)

Kwa taarifa tulizozipokea, mchezaji huyo nguli ambaye ni raia wa Rwanda mwenye asili ya Congo, alikua anakwepa baiskeli mitaa ya Chang’ombe jijini Dar es salaam na ndipo akaingia kwenye Mtaro na gari na kufariki papo hapo.
Bongo5 inafanya jitihada za kupata taarifa za msiba kutoka kwa familia ya ndugu Mafisango ambapo tutazidi kuwahabarisha.
Taarifa hizi zimekuja kama pigo kubwa kwa wadau wapenzi n mashabiki wa mpira na wa mchezaji huyo, na mchezo huo umepoteza mchezaji mahiri.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni