Jumapili, 20 Mei 2012

SERENGETI KUDHAMINI TUZO ZA MWANAMICHEZO BORA WA TANZANIA MWAKA 2011

 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda.
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti imetangaza kudhamini tuzo za Mwanamichezo Bora wa Tanzania Mwaka 2011 kwa sh. Milioni 150, tuzo ambazo zinaandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Udhamini huo ulitangazwa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda, alipokuwa akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye klabu ya City Sports Lounge, Dar es Salaam, ambapo aliambatana na viongozi wa TASWA.

Alisema kampuni yake inaona fahari kuendelea kudhamini tuzo za TASWA ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo, hivyo mwaka huu wameongeza udhamini zaidi ili…

 Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya Bia ya Serengeti Teddy Mapunda.
....... kuziboresha.
Alisema tuzo hizo zitafanyika Juni 14 mwaka huu ukumbi wa Diamond Jubilee (VIP) Dar es Salaam na kwamba wana matumaini makubwa zitakuwa bora kuliko zilizopita.
Naye Mwenyekiti wa TASWA, Juma Pinto aliwashukuru Serengeti na kusema udhamini huo ni ishara ya namna kampuni hiyo inavyothamini wanamichezo hapa nchini na kwamba umeongezeka kwa kiasi kikubwa kutoka sh. Milioni 80 za mwaka jana.
Hata hivyo Pinto alisema milango ipo wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza kama wadhamini washiriki kwa
vile bajeti ya tuzo hizo ambayo awali chama chake kimepanga ni sh. milioni 370, lakini hata udhamini huo unatosha kufanya kitu kizuri zaidi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando alisema Kamati Maalum ya Tuzo hizo inaendelea na mchakato wake wa kupata wanamichezo hao na kwamba kadri watakavyokuwa wanapiga hatua watatoa taarifa kwa wanahabari.
Kwa miaka mitano iliyopita walioshinda Tuzo ya Mwanamichezo Bora wa TASWA walikuwa ni Samson Ramadhani (2006), Martin Sulle (2007), Mary Naali (2008), ambao wote ni wanariadha, wakati 2009 na 2010 alikuwa mcheza netiboli Mwanaidi Hassan.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni