Jumanne, 15 Mei 2012

KIM POULSEN ATAJA TIMU YA TAIFA, YANGA YATOA MMOJA SIMBA YATOA 11

 
Kim Poulsen
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Mei 14 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika dhidi ya Ivory Coast.

Akitangaza kikosi hicho ambacho kitaingia kambini kesho kutwa (Mei 16 mwaka huu, Kim amesema uteuzi wake umezingatia uwezo wa mchezaji uwanjani, nafasi anayocheza na ubora wake.

Wachezaji walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba), Mwadini Ally (Azam) na Deogratius Munishi (Mtibwa Sugar). Mabeki ni Nassor Masoud Cholo (Simba), Aggrey Morris (Azam), Amir Maftah (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Simba), Waziri Salum (Azam), Shomari Kapombe (Simba) na Juma Nyoso (Simba).

Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Salum Abubakar (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Jonas Mkude (Simba), Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Edward Christopher (Simba- U20), Mrisho Ngasa (Azam) na Frank Domayo (JKT Ruvu- U20).

Washambuliaji ni Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Ramadhan Singano (Simba-U20), Simon Msuva (Moro United- U20), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo), Haruna Moshi (Simba) na John Bocco (Azam).

Stars inayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya Kilimanjaro itacheza mechi ya kirafiki nyumbani Mei 26 mwaka huu dhidi ya Malawi kabla kuivaa Ivory Coast ugenini Juni 2 mwaka huu jijini Abidjan

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni