Jumatano, 16 Mei 2012

ASP ALPHONSE MAGABE, ASKARI POLISI WANNE NA RAIA WAWILI WALIFIKISHWA MAHAKAMANI JANA KWA MARA YA PILI.

ASKARI WATANO NA RAIA WAWILI WAFIKISHWA KORTINI WILAYANI LINDI NA KUPATA DHAMANA 

polisi
WATU saba wakiwemo askari Polisi watano na raia wawili wamefikishwa katika mahakama ya mkoa wa Lindi, wakikabiliwa na mashitaka mawili,likiwemo dai la kusaidia usafirishaji wa watu 13 wenye asili ya Pakstani mwishoni wiki iliyopita.
Watuhumiwa hao wamefikishwa Leo, mbele ya Hakimu wa mahakama hiyo, Aluu Nzowa na kusomewa kosa lao na wakili wa Serikali, Mwahija Hamadi.
Waliofikishwa mahakamani hapo ni,ASP Alphonce Magabe, E 5754 Coplo Hilari,F 6069 D/c Francis, G2334 Pc James,PC Joseph, wote ni askari wa kituo cha Lindi mjini,Kasimu Mussa na Emmanuel Joseph,madereva na na wakazi wa Jiji la Dar es salaam.
Akiwasomea makosa yao katika kesi hiyo namba 44/2012,mwanasheria wa Serikali, Mwahija Hamadi,amedai mahakamani hapo kuwa mei 03 mwaka huu,usiku washitakiwa wote kwa pamoja walisaidia kusafirisha raia hao wenye asili ya Pakistani.
Katika Shitaka la pili,linalowakabiri washitakiwa wa kwanza hadi wa watano,mwanasheria huyo wa Serikali alidai mahakamani hapo kuwa ni uzembe wa kushindwa kutekeleza majukumu yao, huku wakijua fika ni waajiriwa wa Jeshi la Polisi.

Raia hao wa kipakistani walikuwa wakisafiri kutoka jijini Dar es salaam, kuelekea nchi jirani za Msumbiji na Afrika ya kusini, wakitumia usafiri wa basi ndogo Toyota Coaster yenye namba za usajili T 368 BPW iliyokuwa ikiendeshwa na mshitakiwa Kassimu Musa.
Mwanasheria huyo wa Serikali aliiambia mahakama hiyo kwamba washitakiwa wote kwa pamoja wamefanya makosa chini ya vifungu vya Sheria namba 5/2008 kifungu kidogo cha 1 na 2 na Sheria namba 148 chini ya Sheria ya uzuiaji usafirishaji binaadamu.
Washitakiwa wote kwa pamoja wamekana makosa yote waliyokuwa wamesomewa na kupelekwa rumande, kesi yao itatajwa tena mei 15 mwaka huu.Aidha, mwanasheria huyo aliiambia mahakama hiyo kwamba chini ya Sheria kifungu namba 6/2008 Shitaka la aina hii mara nyingi halina dhamana.
Kauli hiyo ya mwanasheria ilipingwa vikali na washitakiwa hao,huku wakiiomba mahakama iwape Stahiki kwani Shauri lao,halihusu mauaji wala ujambazi hivyo kuwanyima dhamana ni kuwanyima Haki zao za msingi.
“Mh, Hakimu tunaomba mahakama itupe Stahiki kwani sisi sio majambazi,kwani kuna watu wameshawahi kushitakiwa kwa mauwaji,lakini wanapewa dhamana inakuwaje sisi tusipewe dhamana kwa hili”Alidai mshitakiwa wa kwanza ASP Alphonce Magabe.
Aidha,baada ya Hakimu Nzowa kusikiliza kwa pande zote mbili,ameamua kutoa uwmuzi huo wa kuwapa dhamana au la mei 15 mwaka huu, hali iliyowafanya washitakiwa wote kupelekwa rumande.
Baada ya matamshi hayo na Hakimu Nzowa kutelemka kutoka kwenye kiti chake,mke wa mshitakiwa wa kwanza ASP Magabe, aliongoza msafara wa vilio,uliochangia kundi la maaskari waliofurika mahakamani wakiwemo polisi na washitakiwa wenyewe kushindwa kujizuia na kuangusha vilio, huku mke wa askari huyo akipewa msaada wa kutoka nje na watumishi wa kike wa mahakamani hapo.
wife
Katika kile kinachoonekana wasipigwe picha na waandishi wa Habari waliokuwepo mahakamani hapo,washitakiwa wote saba walipitishwa mlango mwingine badala ya ule wa kawaida na kusafirishwa kupelekwa rumande na gari aina ya Land Cruser yenye namba za usajili STK 3941 inayotumiwa na mwanasheria wa serikali. alieongoza kesi hiyo
DHAMANA YA WATUHUMIWA HAWA IMETOLEWA JANA TAR. 15/05/2012

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni