Jumanne, 28 Februari 2012

PADRI WA KANISA AWASIMANGA WAKWERE WA LUGOBA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Naye ni Mkwele wa Lugoba Bagamoyo.
Padri Mkude alizuiwa kuongoza misa jana asubuhi parokiani hapo, baada ya waumini zaidi ya 200 kuandamana wakiwa na mabango zaidi ya 20 wakidai ahamishwe kwa kuwa amewatukana katika mahubiri yake, kwamba watoto wao ni wachafu na wao wamebaki kucheza ngoma badala ya kufanya maendeleo.

“Tumechoka na mahubiri ya huyu Padri, kila akihubiri kanisani lazima atuseme Wakwere,
tumemkosea nini? Mara atuseme tu masikini, mara watoto wetu wachafu na hatuwapeleki shule tunashindia ngoma, tumechoka, hatumtaki,” alisema muumini ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.

“Leo tumemzuia asisome misa kabisa, hakuna haja maana hakuna amani kanisani, hatujui ana kitu gani na sisi, sijui kwa sababu parokia hii ipo kwa Wakwere? “Hata Jumatano ya Majivu wiki iliyopita katusema tena, eti watoto wetu ni wachafu sana ukilinganisha na makabila mengine, hii ni kashfa.”

Wakwere ni moja ya makabila katika Mkoa wa Pwani linalopatikana wilayani Bagamoyo, Pia Rais wa Tanzania ni Mkwere. Muumini mmoja alidai mahubiri ya Padri huyo ya kuwasema Wakwere hayakuanza siku za karibuni, bali ni ya muda mrefu na yamekuwa kama ya kusutwa badala ya kulishwa Neno la Mungu.

“Hali hiyo imesababisha watu kutokwenda kanisani wakijua leo Padri huyo anaongoza misa, lakini akiongoza Katekista, misa inajaa utadhani Askofu amekuja, tunachotaka hapa ni Padri mwingine, kama Askofu anatujali atuletee mwingine,” alisema muumini huyo

Jumamosi, 25 Februari 2012

ETI TV ZA VICHOGO MWISHO KUTUMIKA 2013!!!?




NewsImages/6277570.jpg
Luninga lenye tumbo au wengine wanaita chogo
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa ametangaza kuwa Luninga - televisheni za teknolojia ya analojia zenye `michogo au matumbo’ hazitafanya kazi kuanzia Januari Mosi, 2013 au ziunganishwe na ving’amuzi vitakavyonunuliw
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa kutangaza kusitishwa kwa matangazo ya Televisheni kwa kutumia analojia kwenda digitali kuanzia Januari Mosi 2013. Bei ya ving’amuzi katika kampuni mbalimbali zinaanzia Sh70,000.


Wakati huo huo, kuna baadhi ya luninga za digitali ambazo ving’amuzi vimejengewa ndani hizo zitatumika kama kawaida. Wananchi wanapaswa kujiandaa mapema hasa kununua ving’amuzi kwa luninga ambazo zinatumia teknolojia ya analojia.


Wataalam wanasema faida ya digitali ni kuongezeka kwa ubora wa picha, matangazo na ongezeko la vituo vya televisheni. Pia kuingia kwa teknolojia ya digitali katika matangazo ya televishenikunapelekea kupatikana kwa wingi zaidi katika vyombo vya mawasiliano kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa intaneti

ASKARI POLISI WANNE WASHIKILIWA KWA MAUAJI YA RAIA HUKO SONGEA.

 KAMANDA WA POLISI MKOA WA RUVUMA MICHAEL KAMUHANDA
 ASKARI WAKITULIZA GHASIA JUZI
Mmoja wa marehemu aliyeuawa kwa kupigwa risasi na Polisi

Na, Stephano Mango ,Songea

VURUGU zilizojitokeza wakati wa maandano ya amani ya wananchi wenye hasira kali katika Halmashauri ya Manispaa ya Songea Mkoani Ruvuma zimesababisha hasara kubwa ya mali zenye thamani ambayo haikufahamika mara moja na kwamba katika sakata hilo Askari  Polisi wanne wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kuwapiga risasi za moto watu wawili ambao wamefariki kwenye maandamano hayo

Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda alisema kuwa hali ya mji kwa sasa hivi ni tulivu na hatua mbalimbali za kiusalama zinaendelea kuimarishwa ili wananchi waendelee na shughuli zao za kila siku

Kamuhanda alisema kuwa kwenye vurugu hizo watu 54 walikamatwa na wamefikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za kufanya maandamano bila kibali na kusababisha uvunjifu wa amani katika maeneo mbalimbali ya mji wa Songea na vitongoji vyake

Alisema kuwa Askari Polisi waliohusika na kupiga risasi raia kwa sasa wanahojiwa na Jeshi hilo ili kupata uhalali wa kutumia risasi za moto katika tukio la maandamano yaliyofanyika jana na kwamba ikidhibitika kuwa walifanya uzembe watachukuliwa hatua za kisheria

Alieleza zaidi kuwa wananchi wakiwa kwenye maandamano hayo walivamia Ofisi za Chama cha Mapinduzi Manispaa ya Songea  na Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Songea Vijijini walipiga mawe milango na kisha kuchoma bendera na kuleta hasara za mali nyingine za chama hicho, walivamia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Songea na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma,walivamia  Ikulu ndogo walipiga mawe, walivamia Kituo cha Polisi na kupiga mawe na kuharibu baadhi ya magari ya wananchi

Alieleza kuwa waandamanaji walirusha mawe hovyo na kuwajeruhi wananchi wenzao, kufunga barabara kwa kutumia mawe makubwa, magogo na kuchoma mataili moto ili gari zinazoingia na kutoka nje ya mji zisiweze kuendelea na safari zake pia waandamanaji walivamia gari la Polisi na kuanza kurusha mawe na kusababisha Askari waanze kujihami kwa kurusha mabomu ya machozi

Alifafanua kuwa fujo hizo zinadaiwa kuwa zimetokana kwa sababu wananchi wamekuwa wakilalamikia matukio mfululizo wa mauaji mbalimbali likiwemo la mwendesha Pikipiki aliyeuawa februari 22 mwaka huu majira ya 2 asubuhi huko katika eneo la mto Matarawe, kuwa Jeshi la Polisi halichukui hatua ya kuwadhibiti wauaji hao

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Thomas Oley Sabaya alisema kuwa baada ya kutokea matukio hayo ameitisha viongozi wa Serikali za mitaa ya yote na kuwapa maagizo kuwa kuanzia sasa ulinzi shirikishi unatakiwa kuanza kwa kasi zaidi na kwamba kama kunawatu wanajihusisha na mambo ya uhalifu wajisalimishe haraka kwenye vyombo vya dola badala kusubiri wakamatwe

Naye Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu amelaani kitendo kilichotokea juzi ambacho amesema sio cha kawaida hivyo kufuatia tukio hilo ameunda tume huru ya watu nane ambayo itafanya kazi ya siku saba ya kuchunguza kwa kina juu ya hali iliyojitokeza juzi mjini Songea na ripoti inapaswa kuwasilishwa arahamisi ijayo asubuhi ofisini kwake na kwamba hiyo tume inahusisha vyombo vyote vya dola

Baadhi ya wananchi wameiomba Serikali ichukue hatua za haraka kudhitibi hali iliyojitokeza juzi ambapo watu wawili waliuawa kwa kupigwa risasi na Polisi wakati wa wenye hasira kali walipokuwa wakipita mitaani kufanya vurugu huku wakidai kuwa Jeshi la Polisi limeshindwa kufanya kazi na mwingine kufa baada ya kutumbukia kwenye shimo na Pikipiki wakati wa vurugu hizo

 Wananchi hao ambao ni wakazi wa maeneo ya Mfaranyaki, Majengo, Bombambili na Mjini ambao wameomba majina yao yahifadhiwe walisema kuwa hali iliyojitokeza juzi haikuwa ya kawaida hivyo ni vyema Serikali ikatafuta njia muafaka ya kudhibiti chanzo cha vurugu badala ya kujishughulisha na kuzuia maandamano ya amani ya wananchi na kwamba thamani yake haikuweza kufahamika mara moja.

Jumatano, 22 Februari 2012

TAKUKURU NACHINGWEA YAFANYA MKUTANO WA UELIMISHAJI UMMA JUU YA MADHARA YA RUSHWA NA WANACHAMA WA NAIPANGA AMCOS.

Hapa anaonekana Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Lindi  Bw. Stephen Chami (mwenye suti nyeupe) akiongea na viongozi wa Chama cha Msingi cha Mazao na Masoko cha Naipanga wilayani Nachingwea kabla ya kuanza kwa mkutano na wanachama wa chama hicho ambao walielimishwa namna ya mapambano dhidi ya rushwa yanavyoendeshwa na jitihada za serikali katika kupambana na adui rushwa, pamoja na hayo wanachama walielezwa maendeleo ya uchunguzi dhidi ya wajumbe wa bodi ya zamani walioachishwa uongozi na mkutano mkuu wa chama mwezi julai 2011 kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa mali za chama ikiwemo ununuzi wa gari ya chama aina ya Fusso ambalo lilikataliwa na wanachama kwa sababu lilinunuliwa kinyume na utaratibu. Mwenye shajara mkononi ni Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Nachingwea Bw. Moses Oguda.

Kamanda Chami akiongea na wanachama wa Naipanga AMCOS.

Katibu wa Naipanga AMCOS akisoma taarifa fupi ya Mwenyekiti wa Chama, wa kwanza kabisa ni Mwenyekiti wa sasa wa Chama hicho Bw. Misere.

Wanachama wa Chama cha Msingi  Naipanga wakimsikiliza Kamanda Stephen Chami (hayupo pichani)

Kamanda wa Polisi wa wilaya SSP Thabit Milanzi alikuwepo, hapa akibadilishana mawazo na viongozi wengine mara baada ya mkutano na wanachama kumalizika. Wanachama walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa dukuduku zao mbalimbali.

Hilli ni jengo la PADEP kijiji cha Naipanga ambapo mkutano ulifanyikia.

TEVEZ AWAOMBA RADHI MANCHESTER CITY

Carlos Tevez, mshambulizi wa Manchester City, ameomba radhi kwa tabia yake isiyofaa hivi majuzi, na iliyoanza tangu alipogombana na meneja Roberto Mancini mwezi Septemba.
Carlos Tevez
Awaomba radhi Manchester City kwa makosa yake

Mchezaji huyo, mwenye umri wa miaka 28, alirudi katika klabu ya Man City wiki iliyopita, baada ya kuchukua hatua mikononi mwake, alipoamua kurudi nchini Argentina kwa kipindi cha miezi mitatu.
“Ningelipenda kuomba msamaha kwa dhati na pasipo kikwazo chochote kwa kila mtu, na kwa yoyote yule niliyemkosea kwa vitendo vyangu ikiwa nimemuudhi”, alielezea Tevez kupitia taarifa.
Wakati huohuo Tevez amefutilia mbali malalamiko aliyokuwa amewasilisha rasmi dhidi ya klabu ya Man City.
“Nia yangu sasa ni kuhusika zaidi katika kuichezea soka klabu ya Manchester City”, alisisitiza.
Baada ya kushindwa kujiunga na AC Milan ya Italia kama ilivyotazamiwa wakati wa usajili wa mwezi Januari, Tevez bila shaka alikuwa na uamuzi mgumu wa kuamua iwapo aendelee kupumzika na akicheza golf huko Argentina, ama arudi tena mjini Manchester na kujaribu kupigania nafasi yake katika timu yake.
Kuna uwezekano bado wa Tevez kuhama wakati wa msimu wa joto, lakini angalau inaelekea kwa hivi sasa uwanja wa Etihad umetulia, baada ya sokomoko iliyozushwa na mchezaji huyo.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina hajawahi kuichezea City tangu mwezi Novemba, wakati meneja Roberto Mancini anadai alikataa kuingia uwanjani kama mchezaji wa zamu, na hatimaye timu kushindwa na Bayern Munich ugenini magoli 2-0 katika mechi ya klabu bingwa mwezi Septemba.
Tevez anadai kulikuwa na hali ya sintofahamu na mkorogano wa lugha, na akaeleweka vibaya.
Moja kwa moja baada ya ugomvi huo, Mancini alisema Tevez “amekwisha” kama mchezaji wa City, lakini baadaye alielezea kuna uwezekano wa mchezaji huyo kukaribishwa tena katika timu, ikiwa ataomba msamaha.

Jumatatu, 20 Februari 2012

MAJAMBAZI WAIPEKUA MAITI.

MAJAMBAZI wamevamia na kuteka gari lililokuwa likimsafirisha maiti kutoka Mpanda mkoani Rukwa kwenda mkoani Mara na kumpekua maiti wakitafuta fedha na vitu vya thamani.

Utekaji huo ulifanyika Ijumaa iliyopita saa saba usiku katika eneo la Mtakuja Manispaa ya Tabora wakati wafiwa wakisafirisha mwili wa mtumishi wa Halmashauri ya Mpanda kwenda Musoma kwa maziko

 
Mkuu wa wilaya ya Tabora Mussa Chang'a(mwenye suti)


Akisimulia mkasa huo jana, Mkuu wa Wilaya ya Tabora, Moshi Musa Chang'a alisema baada ya gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser mali ya halmashauri hiyo kufika Mtakuja, walikuta mawe yamepangwa barabarani na liliposimama, ghafla kundi la majambazi lilitokea porini likiwa na mapanga na marungu na kuteka gari hilo.

Alisema baada ya kuteka gari hilo, waliwapekua waombolezaji waliokuwa wakisindikiza msiba na kuwapora zaidi ya Sh milioni mbili na simu za mkononi.

Chang'a alisema majambazi hao kabla ya kupora fedha hizo, waliwashambulia waombolezaji hao kwa marungu na ubapa wa mapanga na kuwasababishia majeraha madogo.

“Baada ya kumaliza kuwapora waombolezaji hao, ndipo wakaanza kuipekuwa maiti kwa lengo la kupata fedha zaidi au kitu chochote kilichokuwa kimefichwa kwenye jeneza hilo ili wakichukuwe,” alisema Chang’a.

Kwa mujibu wa Chang'a, muombolezaji mmoja alikuwa ameficha simu yake akatoa taarifa kwake na kwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda ambao walifikisha taarifa hizo Polisi Tabora waliofika eneo la tukio usiku huo.

Alisema polisi walipofika eneo la Mtakuja, hawakuwakuta majambazi hao na tayari wameanzisha msako wa kuwabaini majambazi hao.

Mkuu huyo wa Wilaya ya Tabora alisema majambazi hao hawako mbali na eneo la Mtakuja na kuwataka wananchi watoe taarifa Polisi ili wawakamate na kuwafikishwa katika vyombo vya sheria.

Alisema kila mwananchi wa Kata ya Mtakuja ana wajibu wa kushirikiana na Jeshi hilo ili kutokomeza kikundi hicho kinachosumbua watu mara kwa mara hasa nyakati za usiku.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Antony Rutta amekiri kutokea kwa uporaji huo na kuwataka wananchi kuwafichua watu wanaofanya uhalifu huo.

Aliwataka wananchi watoe taarifa hizo kwa siri ili Serikali ichukue hatua madhubuti kupambana na wahalifu hao ikiwemo kuwafikisha mahakamani watuhumiwa

Jumapili, 19 Februari 2012

JAJI MKUU AASA MAHAKIMU WAACHE TABIA YA KUHAIRISHA KESI

MAHAKIMU nchini wametakiwa kuacha utamaduni wa kuahirisha kesi bila sababu za msingi hali inayoleta manung'uniko kati ya mshitakiwa na mdai haki.

Aidha mawakili na wanasheria nao wameaswa kuacha tabia ya kujali maslahi kwa wateja wao
bali waangalie jinsi ya kuwasaidia kupata haki badala ya kuwatetea huku wakijua
wateja wao hawatafanikiwa.

Hayo yalisemwa jana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande wakati alipokuwa
akifungua mkutano wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unaofanyika mkoani
Arusha kwa siku mbili.

Alisema kwenye Mahakama kuna utamaduni kwa baadhi ya Mahakimu kuahirisha kesi bila
sababu za msingi na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo kunaleta malalamiko kati ya
mtuhumiwa na aliyefungua kesi hali inayopelekea wananchi kukosa imani na Mahakama.

Pia alisema si busara kwa mawakili ambao ni maofisa wa Mahakama kujali fedha kwa
wateja wao huku wakijua haki itatendeka na kuwaasa kuacha tamaa za fedha badala
yake watoe huduma kwa wananchi ambao wanahitaji msaada wa kisheria pasipo kuwa na
fedha.

"Acheni tabia ya kutaka fedha huku mkijua wateja wenu hawatafanikiwa katika kesi
inayowakabili pia na Mahakimu acheni tabia ya kuahirisha kesi bila ya kuwa na sababu
za msingi."

Aliongeza kuwa baadhi ya wananchi hawana uwezo wa kawaida kupata mawakili wa
kuwatetea kutokana na fedha lakini kisheria inatakiwa mawakili kujitolea kuwasaidia
washitakiwa kwenye kesi zao, hivyo wawe na moyo wa huruma na si kuangalia maslahi
yao binafsi.

Naye Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Francis Stola aliiomba Serikali
kutenga fedha kwa wakati za mashauri ya kesi za uchaguzi na yale ya dharura ili kesi
hizo ziweze kuamuliwa kwa wakati badala ya kupoteza muda.

Pia alisema wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maktaba, vitabu vya sheria
pamoja na tatizo la rushwa kwa baadhi ya wanasheria ambao wanatia doa taaluma hiyo
na kusisitiza kuwa taaluma hiyo ni muhimu katika kusaidia jamii mbalimbali

TAARIFA YA DK. HARRISON MWAKYEMBE KUIJIBU KAULI YA DCI MANUMBA(POLISI)

Dk. Harrison G. Mwakyembe (Mb), NW-UJ
 Dar es Salaam
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI  

Nimelazimika leo Jumamosi, tarehe 18 Februari, 2012 kutoa taarifa hii kwa vyombo vya habari kufuatia mkutano wa DCI Robert Manumba na waandishi wa habari jana (17/02/12) kuongelea, pamoja na mambo mengine, hali yangu ya afya na kuhitimisha, kienyejienyeji tu kuwa “sikunyweshwa sumu” ila naumwa tu ugonjwa wa ngozi bila kufafanua ugonjwa huo wa ngozi umesababishwa na nini!

Napenda nisisitize mapema kabisa kuwa msimamo huo wa Jeshi la Polisi umenikera sana katika hali niliyonayo ya ugonjwa, kwanza kwa kuingilia mchakato wa matibabu yangu na uchunguzi wa kina kuhusu kiini chake unaoendelea hospitali ya Apollo nchini India ambako bado sijahitimisha matibabu yangu; pili kwa ufinyu wa uelewa unaojitokeza bayana kwenye tamko la Jeshi la Polisi unaosisitiza kuwa “sikunyweshwa sumu” wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru, inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa tu; na tatu kwa Jeshi la Polisi kujiingiza kwenye suala ambalo kwa takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati ya kulielewa au kulichunguza mbali na kulifanyia mzaha kupitia magazetini.

Itakumbukwa kuwa tarehe 9 Februari, 2011 nilimwandikia barua IGP Said Mwema kumtaarifu kuhusu njama za kuondoa maisha yangu na ya viongozi wengine. Kwa kutambua kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania daima husisitiza kuletewa ushahidi kwanza ndipo lifanyekazi, nilihakikisha nimeainisha katika barua  hiyo kila ushahidi nilioupata au kupewa. (Utaratibu huu wa Jeshi la Polisi kusubiri kuletewa ushahidi mezani, kama ambavyo mahakimu wanavyosubiri ushahidi mahakamani, haupo popote pale duniani (ila Tanzania tu) kwani kazi ya msingi ya Polisi si kuletewa, ni kutafuta ushahidi. Polisi wanachohitaji duniani kote ni kupata clue au tetesi tu. Hiyo inatosha kufukua ushahidi wote unaohitajika). Pamoja na kujitahidi kuanika kila aina ya ushahidi niliokuwa nao, mambo manne yalijitokeza ambayo yalionyesha wazi kuwa Polisi hawakuwa na dhamira ya dhati ya kupeleleza suala hilo:

(i)                Siku chache baada ya kumkabidhi IGP barua hiyo, nilitumiwa timu ya “wapelelezi” ofisini kwangu kuja kuchukua maelezo yangu ya ziada. Timu hiyo ilikuwa inaongozwa na ACP Mkumbo, afisa wa polisi ambaye wiki chache zilizokuwa zimepita alikuwa miongoni mwa askari waliotuhumiwa kupokea rushwa kwa lengo la kumbambikizia madawa ya kulevya mtoto wa Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi, suala ambalo mpaka leo hii uongozi wa Polisi umeshindwa kulitolea maelezo ya kuridhisha. Kwa msingi huo, nilikuwa nimeletewa mtuhumiwa wa rushwa/ ujambazi kuendesha uchunguzi wa watuhumiwa wengine wa ujambazi! Nikatambua mara moja kuwa zoezi zima lilikuwa la mzaha, tena mzaha mkubwa!

(ii)              Wiki chache baada ya barua yangu kuwasilishwa kwa IGP na timu ya ACP Mkumbo “kuanza kazi”, Jeshi la Polisi likachukua hatua ya kuwapongeza na kuwazawadia askari niliowatuhumu kushirikiana na majambazi! Huhitaji kuwa profesa wa falsafa kuelewa kuwa huo ulikuwa ujumbe tosha wa kunipuuza.

(iii)            Hivi karibuni tuhuma za askari polisi kujihusisha na vitendo vya ujambazi mkoani Morogoro zilipopamba moto na kuwagusa askari “wale wale” niliowatuhumu kwenye barua yangu, IGP alichukua hatua ya kuwahamishia mikoa mingine!

(iv)           ili kunikatisha tamaa kabisa, barua yangu ya “siri” kwa IGP ikavujishwa kwa makusudi kwenye vyombo vya habari na kuchapishwa kama habari ambayo ilikebehi na kukanusha taarifa nzima niliyotoa, sijui kwa faida ya nani! Lakini huu ni mchezo wa kawaida kwa polisi kwani hivi karibuni Mhe. Waziri Samuel Sitta alipohojiwa na ofisa mwandamizi wa Jeshi la Polisi ofisini kwake, wakiwa wawili tu, taarifa ya kikao hicho ikawa kwenye moja ya magazeti ya mafisadi ikikebehi ushahidi aliotoa Sitta! The integrity of the police force leadership is on the line.

Nimeelezea vizuri katika barua yangu kwa IGP kuwa kundi hilo la mauaji lilikuwa limeelekezwa kuniua kwa kutumia sumu, taarifa ambayo kwa karibu mwaka mzima Polisi hawakutaka kuifuatilia kwa sababu wanazozijua wenyewe.  Sasa huu msukumo mpya wa Jeshi la Polisi kutaka kujua kama nilipewa sumu au la na kukurupuka kutoa tamko hata kabla ya kunichunguza nilivyo, kunihoji mimi na wasaidizi wangu ofisini na hata kuongea na mabingwa wa Kihindi wanaonifanyia uchunguzi, umetokea wapi?  Si ni polisi hawahawa ambao, badala ya kushukuru,  wamekuwa wakikerwa na tahadhari ambazo Waziri Sitta amekuwa akitoa ili suala hili lichunguzwe kwa kina?

Aidha napata taabu kuamini kama DCI Manumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matatibabu yangu au walisoma taarifa “nyingine”, na kama waliisoma taarifa hiyo wenyewe au “walisomewa”! Nasema hivyo kwa kuwa alichokisema DCI Manumba kwa wandishi wa habari hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya Apollo ambayo inatamka wazi kuwa kuna kitu kwenye bone marrow kinachochochea hali niliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaikia kukijua, kukidhibiti /kukiondoa huku vyombo vyetu vya dola vikipelekeshwa na mafisadi kusema bila msingi wa kisayansi wala aibu: “hakulishwa sumu”, “hakulishwa sumu”!

Nimesoma darasa moja Kitivo cha Sheria Mlimani na DCI Manumba. Baadaye IGP Mwema alikuwa mwanafunzi wangu wa sheria Mlimani. Vigogo hawa wawili wa usalama wa raia nchini hawajanitendea haki, nao wanajua. Wanajua vilevile kuwa sitakaa kimya au kumung’unya maneno come what may pale ambapo haki inakanyagwa.

Tuendelee kuombeana afya na uhai ili tutendeane haki na vilevile tuitendee nchi yetu haki kwa kuvimalizia viporo vinavyokera vya Dowans, EPA, Kagoda n.k. kwa maslahi mapana ya Taifa letu.

Mungu Ibariki Tanzania
.

NIMEIPENDA HII, SABABU KUU YA KUKOSEKANA MADAWA HOSPITALI ZA SERIKALI, MSD MPO!!!?

 

Alhamisi, 16 Februari 2012

LIBYA IMESHINDWA KUDHIBITI WAPIGANAJI


misrata
Watu weusi ndio wanateswa zaidi

Shirika la kutetea haki za binadamu, Amnesty International linasema visa vya mateso, mauaji na watu kuzuiliwa bila kufunguliwa mashataka vimekithiri nchini Libya.
Shirika hilo linasema ukiukaji huo unatekelezwa na makundi ya wapiganji waliojihami ambao walimng'oa Muammar Gaddafi madarakan
Walioathirika zaidi ni watu wanaohofiwa kuwa wafuasi wa Gaddafi, waafrika weusi na wahamiaji walioko Libya.
Kufuatia visa hivyo makundi ya watu waliolengwa sana na visa hivyo wamehama makaazi yao.
Shirika la Amnesty international linasema serikali mpya ya Libya imeshindwa kuwachukulia hatua watu wanaotekeleza vitendo hivyo.
Kuanzia mwezi uliopita BBC imekuwa ikikusanya ushaidi wa mateso yanaoendelea miji ya Misrata, Gharyan na kusini mwa mji mkuu Tripoli.
Ijumaa hii, sherehe zitafanyika kote nchini Libya kuadhimisha mwaka mmoja tangu mapinduzi yaanze ambayo yalitarajiwa kuleta mabadiliko.
Kuna wasiwasi mkubwa sasa kuwa watu waliosaidiwa na NATO kuupindua utawala wa zamani, sasa wanahatarisha siku za baadaye za nchi hii

Jumatano, 15 Februari 2012

CHANDRA BAHADUR DANGI ANAWEZA KUWA MTU MFUPI ZAIDI DUNIANI, ANA SENTIMETA 56 TU.

World's shortest man? Pensioner from Nepal hoping to become a record breaker measuring just 22 inches tall

Chandra Bahadur Dangi, a 72-year-old Nepali who claims to be the world's shortest man at 56 centimetres (22 inches) in height
Chandra Bahadur Dangi, pictured, a 72-year-old Nepali is just 56 centimetres or 22 inches tall. Mr Dangi says he has always been ashamed of his height but his life could be on the verge of changing if he gets official recognition in the Guinness Book of Records. The current record is held by Filipino Junrey Balawing, who measures 59.93 centimetres.

DK. MWAKYEMBE ARUDI TENA INDIA

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe anatarajia kuondoka nchini wakati wowote kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu.

Dk. Mwakyembe kabla hajapata maradhi ya ngozi.
Dk Mwakyembe amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya ngozi ambayo Oktoba 9 mwaka jana, alilazimika kupelekwa katika Hospitali ya Appolo nchini India kwa matibabu zaidi.

Jana, vyanzo vya karibu na Dk Mwakyembe vilidokeza gazeti hili kwamba naibu Waziri huyo na Mbunge wa Kyela anatarajiwa kurudi Appolo, kwa ajili ya kuangalia kama matibabu aliyopata yameweza kumsaidia kwa kiwango gani.

Vyanzo hivyo vilivyo karibu na Dk Mwakyembe, vilifafanua kwamba anachokwenda kufanya India ni "Uchunguzi tu wa kawaida kuona maendeleo ya matibabu." 

Dk. Mwakyembe alipougua na kutibiwa India.
"Atarudi katika uangalizi wa kawaida, kwasababu amekuwa akipata matibabu hivyo lazima achunguzwe kuona dawa alizokuwa akitumia zimemsaidia kwa kiwango gani," alisema.

Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela, hivi karibuni alijitokeza na kutoa kauli nzito kuhusu chanzo cha maradhi yanayomsibu, huku Serikali ikiendelea kukaa kimya hata baada ya washirika wake wa karibu kusisitiza kwamba alipewa sumu.

MALI ZA VIGOGO 60 KUHAKIKIWA NA TUME YA MAADILI YA VIONGOZI.

WAZIRI wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, ni miongoni mwa viongozi 60 watakaohakikiwa mali zao kuanzia Jumatatu.

Kwa mujibu wa Sekretarieti ya maaduili ya Viongozi wa Umma, wengine watakaohakiiwa ni pamopja na wakurugenzi, wabunge, madiwani na makanda wa Polisi wa mikoa.

Mbunge wa Ubungo, Mh. John Mnyika.

Kamishna wa Sekretarieti hiyo, Jaji Salome Kaganda, al;isem,a jana Dar es Salaam kwamba kazi hiyo itakamilika Machi mosi katika kanda sita na makao makuu, Dar es Salaam.

Wengine watakaohakikiwa katika awamu ya kwanza pamoja na Sitta na Mnyika ni, Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Injinia Stella Manyanya na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu.

Pia Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, Mbunge wa Lulindi, Jerome Bwanausi, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Liberatus Sabas na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Dk. Didas Massaburi.

Kadhalika yumo Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Charles Nyamrunda, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ludovic Mwananzila na Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Samia Suluhu.

Kanda zitakazohusika na uhakiki huo ni Nyanda za Juu Kusini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kati, Kanda ya Kaskazini, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kusini.

Jaji Kaganda alisema, kutokana na idadi ya viongozi kuwa kubwa, sekretarieti itaanza na uhakiki wa viongozi 60 wenye nyadhifa tofauti na kazi hiyo itafanywa kwa mujibu wa sheria na wanasheria waliobobea wa sekretarieti hiyo na wachunguzi.

“Sheria ya Maadili inamtaka kila kiongozi wa umma anayehusika na sheria hii, kutoa taarifa za mali na madeni katika kipindi cha siku 30 baada ya kupewa wadhifa na kila mwisho wa mwaka yaani ifikapo Desemba 31,” alisema Jaji Kaganda.

Alisema, mwitikio wa urejeshaji wa matamko ya kukiri mali na madeni ya viongozi umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 22.5 kutoka wastani wa asilimia 60 kwa mwaka 2010.

Jaji Salome aliwataka viongozi wote waliopangiwa kufanyiwa uhakiki kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maofisa wa Sekretarieti ili wafanikishe kazi hiyo.

Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi kushirikiana na Sekretarieti kutoa taarifa zitakazosaidia kugundua mali zilizofichika ambazo zinasadikika kuwa za viongozi wa umma wanaoguswa na Sheria ya Maadili.

Alisisitiza kuwa, viongozi waliotajwa kuhakikiwa wasifikiri kuwa wametajwa na wengine na waepuke matapeli ambao wanaweza kuwafikia wakiwataka kutoa rushwa ili wasihakikiwe wakijidai kuwa wao ni maofisa wa Sekretarieti.

Kuhusu vigezo vilivyotumika kuanza na viongozi hao, Jaji Kaganda alisema Sekretarieti iliteua sampuli bila kuzingatia vigezo, katika kila kanda na kupata viongozi hao na kuzingatia kanuni za uwazi ili kila mwananchi ajue kinachofanyika.

Katibu Msaidizi, Idara ya Viongozi wa Siasa, Coletha Kiwale alisema kazi ya uhakiki ni ya kawaida na viongozi waliotajwa hawana tuhuma yoyote bali ni moja ya utekelezaji wa majukumu ya Sekretarieti.

Alisema viongozi wanaohusika wamepelekewa barua na maelekezo yanayostahili na kutakiwa kuandaa nyaraka mbalimbali zitakazosaidia uhakiki huo.
Mali ni kosa?

Katika hatua nyingine, Jaji Kaganda alisema katika kikao cha Baraza la Maadili kilichokutana mwaka jana kuhoji baadhi ya viongozi ambao hawakujaza fomu ya kutambulisha mali zao, hawakufikia kutoa adhabu ya kufukuzishwa kazi kwa kiongozi yeyote badala yake wapo waliopewa onyo kali.

Jumatatu, 13 Februari 2012

KOCHA WA ZAMBIA ASEMA KOMBE LA AFRIKA NI KUMBUKUMBU KWA WACHEZAJI WA KK ELEVEN WALOKUFA KATIKA AJALI YA NDEGE PWANI YA GABON 1993.

Destiny! Renard dedicates Zambia glory to 1993 squad who perished in plane crash

By Sportsmail Reporter
Last updated at 12:33 PM on 13th February 2012

Zambia coach Herve Renard dedicated his side's African Nations Cup victory to Kalusha Bwalya and the fallen squad of 1993, claiming it was 'written in the sky'.
The Copper Bullets beat the Ivory Coast 8-7 on penalties after a goalless final on Sunday night in Libreville - the scene of a plane crash 19 years ago, en route to a World Cup qualifier against Senegal, which defines the country's modern footballing history.
The Zambia national team's plane crashed into the sea shortly after a refuelling stop, killing 18 players, but star player Kalusha only survived as he had travelled separately from Holland, where he was playing for PSV Eindhoven.
That's for you: Zambia coach Herve Renard is held aloft by his players as they celebrate winning the Africa Cup of Nations
That's for you: Zambia coach Herve Renard is held aloft by his players as they celebrate winning the Africa Cup of Nations
That's for you: Zambia coach Herve Renard is held aloft by his players as they celebrate winning the Africa Cup of Nations
Now the Zambian FA president, Kalusha joined the current squad as they paid tribute in a ceremony on the Beach Sabliere ahead of the final.
Renard said after Sunday's poignant triumph: 'Kalusha was one of the best Zambian players of the last century. Then he was coach of the national team, now our president.
'He survived the crash - he was supposed to have been on that plane which was going to play a World Cup qualifier against Senegal. He knows how terrible this crash was for the nation. I want to dedicate this title to him.'
Glory: Zambia beat Ivory Coast on penalties to win the tournament for the first time
Glory: Zambia beat Ivory Coast on penalties to win the tournament for the first time
He added: 'We wanted to honour the dead players and that strengthened us. Our first game (in this year's tournament) was against Senegal and the team was on its way to Senegal for a match when the plane crashed. The plane crashed in Gabon and we won the final in Gabon.
'It was a sign of destiny, written in the sky. There was a force with us. I think God has helped us and given us strength.'
It was Zambia's first Nations Cup title and their third final, including in 1994 when Kalusha led a makeshift squad to within one hurdle of glory.
'I said to the players that a team of 'replacements' took Zambia to the final in 1994, so why not us?' said Renard. 'We always believed and said this was our time.
'Winning on penalties is perhaps not the best way, but we cannot complain. It is cruel for the Ivory Coast, but we deserved it. We will savour this moment, we have made a permanent mark on Zambian football history.'
Zambia needed two opportunities to seal victory in the shoot-out, with Rainford Kalaba failing to capitalise on Kolo Toure's miss before Stophira Sunzu punished Gervinho's wayward spot-kick.
'(My penalty) was supposed to be the winning goal,' Kalaba said on the Zambian FA's website. 'These things happen in football, but then you have to move on. You just have to forget about the past and concentrate on the future.'
Tragic: Almost 19 years ago, 18 Zambian footballers died when their plane crashed off the coast of Libreville
Tragic: Almost 19 years ago, 18 Zambian footballers died when their plane crashed off the coast of Libreville
That he did, as he enjoyed his team's emotional celebrations.
'We wanted to honour the players that died here, so that the families of the deceased players can feel much better and I am pleased we achieved that,' he said. 'I have been dreaming about this wonderful moment.'
The Elephants had the better of the chances in normal time, with Didier Drogba missing from the spot and Yaya Toure and Max Gradel going close.
Remembering: Prior to the final, former African footballer of the year Kalusha Bwalya of Zambia (right) paid tribute to the victims of the 1993 air crash
Remembering: Prior to the final, former African footballer of the year Kalusha Bwalya of Zambia (right) paid tribute to the victims of the 1993 air crash
And coach Francois Zahoui said: 'We had chances to score and we didn't take them. We did not know how to kill off the match and Zambia took confidence from that.
'We knew it would be a difficult final, Zambia wanted the trophy like us and they were not there by chance.'
Goalkeeper Boubacar Barry added: 'It's disappointing but it's not the end of the world. We finished as the best defence and the best attack, so it's frustrating, but we must learn the lessons of this tournament

Jumamosi, 11 Februari 2012

JAMANI TUNAKOKWENDA NI HUKU AU TUMEKOSEA, MAUAJI YA KUTISHA HUKO SONGEA.

Majambazi wawili wachomwa moto wakiwa hai

Pichani ni miili ya watu wawili wanaodaiwa kuwa majambazi  ambao walipigwa na  kuchomwa moto hadi kifo katika eneo la Ruhuwiko manispaa ya Songea mkoani Ruvuma.

Baadhi ya wakazi wa eneo la Ruhuwiko ambao hawakutaka kutaja majina yao walidai kuwa kabla ya tukio hilo watu hao hawakuweza kufahamika majina yao waliwasili eneo hilo majira ya saa tatu asubuhi wakiwa na lengo la kuuwa na kuondoa viungo vya uzazi vya binadamu ambavyo inadaiwa vinauzwa kwa fedha nyingi.


Wananchi hao walidai kuwa watu hao walifika kwa mama mmoja ambao walidai wanamtafuta hatimaye wakiwa wanakunywa katika klabu moja ya pombe za kienyeji inadaiwa wakazi wa eneo hilo waliwatilia mashaka watu hao na kuaanza kuwahoji ambapo inadaiwa baada ya kupata kipigo na kuanza kuchomwa walieleza kwamba wao ni wauaji na walipewa fedha kwa ajili ya kuuwa na kwamba tayari wamekuwa wamefanya matukio kadhaa ya mauaji .

Chanzo cha habari kimebainisha kuwa wauaji hao walidai kuwa wapo 50 na wanatakiwa kuuwa watu zaidi ya 100 wakiwemo wanaume 60 na wanawake 40 kwa kuwaondoa sehemu zao za siri ambazo inadaiwa ni biashara ambayo inawapatia fedha nyingi .

Baada ya wauaji hao ambao walikutwa na shilingi 500,000 kukiri kuwa kazi yao ni kuuwa ndipo wananchi wengi wenye hasira waliamua kuanza kuwapa kipigo kizito kisha kununua petroli na kuanza kuwachoma wakiwa hai .Hadi polisi wanafika katika eneo hilo miili ya watu hao ilikuwa inaendelea kuungua kwa moto.

Uchunguzi umebaini kuwa wakazi wa Ruhuwiko waliamua kuchukua sheria mkononi baada ya matukio ya uharifu na  mauaji kujitokeza katika eneo hilo  na kwamba hii ni mara ya pili kwa wakazi wa Ruhuwiko kufanya mauaji ya kutisha ambapo miaka 25 iliyopita watu wengine wawili waliodaiwa kuwa ni majambazi sugu waliuwa na kisha miili yao kuchomwa moto.
"Mimi binfasi nimefurahia sana kitendo hiki labda sasa majambazi yataogopa kuendelea kufanya uharifu katika eneo hili,hivi sasa hatuna amani kabisa wizi imekuwa ni jambo la karibu kila siku ,mauaji nayo yanazidi kuendelea ,waharifu wengine wanakamatwa na kuachiwa  acha wananchi wajichukulie sheria mkononi'',alisema mama mmoja ambaye hakutaka jina lake kuandikwa.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Ruvuma Michael Kamuhanda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na polisi bado wanaendelea na uchunguzi.
albano.midelo@gmail.com

JIHADHARI NA WIZI WA MTANDAONI-CYBERCRIME HASA KWENYE MOBILE SIM BANKING.

Ujumbe ufuatao nimeupokea kwenye e-mail kutoka kwa mtu ninayefahamiana naye.
Mfano wa simu inayowezesha huduma za za kibenki(simbanking)
Leo yamenifika, na ninapenda kutoa tahadhari hii kama hili halijawahi kukumba. Leo asubuhi kuna jamaa alinipigia simu akidai kuwa anatoka kitengo cha NMB mobile banking akaniambia kuwa airtel wanatoa bonus kwa wateja wazuri wanaotumia service hiyo. Sasa bila kujua hili wala lile nikatoa taarifa za simu yangu na hata za account yangu.

Guess what?

Baada ya muda nikarealise kuwa line yangu imekuwa blocked na ndipo niliposhtuka na kujua kuwa nimeliwa!

Nilipiga simu kwa Bank Manager na kumweleza suala hilo na baadaye alinidhhirishia kuwa account yangu imekombwa yote. Hivyo nikamwambia wai-block, kitu ambacho pia kilikuwa kinawapa shida kwa sababu line ilikuwa imeshachakachuliwa. Kama isitoshe, wakaanza kupiga simu kwa watu ambao awali walitaka niwape namba tano za watu ninaowapigia simu mara kwa mara, wakiwataka hao watu wanitumie pesa na kwa sababu simu ilionyesha kuwa inatoka kwangu wengine walikuwa karibu waanze ku-act.

Kwa hiyo ni kuwa zile information za simu yangu ziliwasaidia ku-disable line yangu toka kwenye simu card yangu na na kuziweka kwenye simu card yao maana pia walihitaji ICC number ya sim card yangu, hivyo kuweza kuwasiliana na watu waki-impose kuwa ni mimi. Pili details za benki ziliwapa access kwenye account yangu na kuikwangua yote.

Kwa hiyo ndugu, kama hujawahi tokewa na hili au ulikuwa unalisikia tu kwa mbali leo hii mimi ninakuwa shahidi kwako na tafadhali usotoe taarifa zako zozote kupitia simu kama nilivyofanya mimi. Teknologia ina faida na hasara zake kwa hiyo siyo mbaya kushiriki vyote ila pale iwezekanapo jaribu kuepuka hasara. Kama utataka kujua mbinu waliyotumia unaweza kuuliza nikujuze ili uwe makini kitokea mtu akakupigia simu kama hiyo.

Mungu awabariki sana!

Wenu Mhanga wa Teknolojia


Source: http://www.wavuti.com/

MADAKTARI WAMALIZA MGOMO JANA HUKU WAKIFURAHI MADAI YAO KUKUBALIWA.

Mh. Mizengo Pinda, Waziri Mkuu JMT.
SIKU moja baada ya kumalizika kwa mgomo, madaktari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
na zingine za umma nchini, wamerejea kazini.

Akizungumza na 'HabariLeo' jana, mmoja wa viongozi wa Kamati ya Kufuatilia Madai ya Madaktari, Dk. Frank Kagoro, alisema wamerejea kazini bila kinyongo. Alisema ingawa mazungumzo yao na Waziri Mkuu hayakutoa majibu ya matatizo yao yote, lakini wameamua kurejea kazini ili kuridhia makubaliano hayo.

“Ingawa hatukuridhika na baadhi ya maelezo ya Waziri Mkuu, tumekubali kurudi kazini na kuchapa kazi kwa bidii, kwa sababu Serikali imeonesha nia ya kukaa meza ya mazungumzo, kutusikiliza na kutafutia ufumbuzi wa matatizo yanayotukabili,” alisema Dk. Kagoro.

Alisema madaktari hao watatumia nafasi waliyopewa ya kutoa mapendekezo mapya kwa kugusia pia mambo ambayo hayajawaridhisha na kisha kuyawasilisha kwenye Tume iliyoundwa kwa lengo la kuchunguza na kutoa mapendekezo kuhusu kero zao. Alisema kwa kuwa madaktari walipewa fursa ya kuendelea kukutana na viongozi wa Serikali kwa ajili ya kushughulikia matatizo yao, wamepanga kufanya mkutano huo Machi 3.

“Mkutano huo ndio utakaokuwa na majibu sahihi kama madaktari wameridhika au la, lakini la muhimu zaidi tunaiomba Serikali itimize tuliyokubaliana,” alisema Dk. Kagoro. Madaktari walirudi kazini jana baada ya kufanya mgomo uliodumu takribani mwezi mmoja kwa lengo la kuishinikiza Serikali kutekeleza madai yao.

Mgomo huo ulimalizika juzi baada ya Waziri Mkuu Pinda kukutana nao Muhimbili ambapo pamoja na mambo mengine, alitangaza kuwasimamisha kazi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk. Deo Mtasiwa.

Alisema Blandina na Mtasiwa wamesimamishwa kazi kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili na madai kwamba wamekuwa kiini cha matatizo kilichosababisha madaktari
hao kugoma. Pia Waziri Mkuu alikubali kushughulikia mapendekezo manane yaliyotolewa na madaktari hao.

KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA LINDI ATEMBELEA SEKONDARI KUHAMASISHA VILABU VYA WAPINGA RUSHWA.

Kamanda Steven Chami akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Naipanga Nachingwea juzi.
Wanafunzi wakisikiliza mawaidha ya kamanda
Viongozi wa wanafunzi wakitoa neno la shukurani.

Alhamisi, 9 Februari 2012

ZAMBIA KUKUTANA NA IVORY COAST KWENYE FAINALI YA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA.


Ivory Coast watakutana na Zambia kwenye fainali
Ivory Coast wameifunga Mali 1-0 na kufuzu fainali
Ivory Coast itakutana na Zambia kwenye fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika baada ya timu hizo mbili kushinda mechi zao za nusu fainali.
Ivory Coast imefuzu baada ya kuishinda Mali 1-0 katika nusu fainali yao mjini Libreville, nchini Gabon.
Bao la ushindi la Ivory Coast lilifungwa na mchezaji wa Arsenal Gervinho katika kipindi cha pili.
Awali katika mji wa Bata nchini Gabon Zambia iliibandua Ghana kutoka mashindano hayo kwa kuifunga 1-0.
Bao la Zambia lilifungwa katika dakika ya 78 na mshambuliaji Emmanuel Mayuka.
Katika kipindi cha kwanza mshambuliaji wa Ghana Asamoah Gyan alikosa kufunga penalti, mlinda mlango wa Zambia akautema nje mpira.
Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika itachezwa siku ya Jumapili mjini Libreville, nchini Gabon, mechi ambayo itatangazwa moja kwa moja kupitia Idhaa ya Kiswahili ya BBC

Jumanne, 7 Februari 2012

JIJI LA NAIROBI LAFIKIRIA KUTENGA ENEO KWA AJILI YA MACHANGUDOA.

The Nairobi City Council is now planning to give commercial workers a license to operate freely in the Central Business District. The Mayor George Aladwa says he has received petitions from hundreds of twilight girls who claim they are harassed by city askaris while on duty. As James Smart of  NTV reports, City Hall has chosen a rather significant day to make the big announcement

WAZIRI ATIMULIWA NA NYOKA KANISANI.

Mh. Aggrey Mwanri kushoto akiwa na Askofu Thomas Laizer(Picha na Maktaba)
NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Aggrey Mwanri, juzi
alitimua mbio kunusuru maisha yake na waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini, Usharika wa Sanya Juu, mtaa wa Kilingi.

Hali hiyo ilitokea baada ya tukio la nyoka kutoka kusikojulikana kuingia kanisani humo huku Naibu Waziri akijiandaa kuendesha harambee ya ujenzi wa Kanisa hilo. Tukio hilo lilitokea katika ibada ya saa nne iliyokuwa ikiongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini, Dk. Martin Shao, ambayo pia ilikuwa ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi huo.

Mwanri aliyekuwa mgeni rasmi kwa ajili ya kuendesha harambee hiyo ya Kanisa la Kilingi, akiwa na mkewe meza kuu, aliwashangaza waumini alipokimbia akiwa amenyanyua mikono juu. Kutokana na kuibuka kwa nyoka huyo, waumini walikimbizana na kiumbe huyo kwa mawe na viti bila kujali kama walikuwa ibadani, huku Askofu na wachungaji wengine wakiendelea kusali na waumini kutakiwa kurejesha utulivu katika ibada.

Hata hivyo, jitihada za waumini za kumkimbiza nyoka huyo kutaka kumwua hazikufanikiwa, baada ya kutoweka asionekane tena, jambo lililoacha simulizi la ni kwa jinsi gani alifika mahali hapo. Awali mgeni rasmi wa harambee hiyo, alikuwa awe Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, lakini kutokana na kubanwa na shughuli za sherehe za maadhimisho ya miaka 35 ya kuzaliwa CCM, alishindwa kufika.

'Habarileo' lilishuhudia Mwanri ambaye pia ni Mbunge wa Siha akikimbia huku akitamka maneno ya “shindwa kwa Jina la Yesu wewe shetani, shetani shindwa kwa Jina la Yesu,” huku wageni wengine waalikwa wakianguka chini wakijiokoa.

Jumatatu, 6 Februari 2012

GHANA NA MALI ZAINGIA NUSU FAINALI KOMBE LA MATAIFA HURU YA AFRIKA.

Ghana siku ya Jumapili ilifuzu kuingia nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kuishinda Tunisia magoli 2-1, katika muda wa ziada.

Kipindi cha kawaida cha dakika 90 kilipokwisha, timu hizo zilikuwa sare ya 1-1.
Wachezaji wa Ghana
Black Stars ya Ghana sasa kupambana na Zambia katika nusu fainali
Nahodha wa Black Stars ya Ghana, John Mensah, alifunga bao la kwanza katika mechi hiyo, katika dakika ya tisa, kabla Sabeur Khalifa kuisawazishia Tunisia kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika.
Bao la ushindi la Ghana lilifungwa na Andre 'Dede' Ayew.
Katika historia ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika, Tunisia haijawahi kuishinda Ghana.
Black Stars sasa wana matumaini ya kuendelea katika mashindano hayo na kupata ubingwa baada ya subira ya miaka 30, na watakutana na Zambia katika nusu fainali itakayochezwa uwanja wa Bata, siku ya Jumatano, tarehe 8 Februari, na ikiwa ni nusu fainali ya kwanza.
Mali na Ivory Coast nao watapambana katika nusu fainali ya pili siku ya Jumatano, katika uwanja wa Libreville.
Mali ilifuzu kuingia nusu fainali baada ya kuwashinda wenyeji Gabon 5-4 katika kupiga mikwaju ya penalti, baada ya mechi kumalizika kwa sare ya 1-1, na mabao kukosekana hata katika muda wa ziada.
Bao la Eric Mouloungui lilikuwa limewatia matumaini wenyeji Gabon, ambao mwaka huu wamekuwa wakishirikiana na Equatorial Guinea kuandaa mashindano ya mwaka huu.
Lakini kutangulia sio kufika, na Tidiane Diabate aliweza kuisawazishia Mali, zikiwa zimesalia dakika tano tu kabla ya mechi kumalizika.
Kwa kushindwa kufungana katika muda wa ziada, ilikuwa ni pigo kubwa wakati wa mikwaju ya penalti, Pierre-Emerick Aubameyang aliposhindwa kuifungia Gabon bao.
Gabon hawajawahi kufuzu kufika nusu fainali za mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika.
Idhaa ya Kiswahili ya BBC, ikishirikiana na redio washirika, itakutangazia nusu fainali kati ya Mali na Ivory Coast kutoka mjini Libreville, Gabon, katika matangazo maalum ya Ulimwengu wa Soka.
Charles Hilary vile vile atakutangazia mechi ya fainali ya mashindano hayo

MADAKTARI VS SERIKALI, BADO!!?

Jumapili, 5 Februari 2012

NDOA ILIYODUMU KWA MIAKA 82, BADO WANAPENDANA NA KUHESHIMIANA.

'True love never fades': Husband, 100, and wife, 99, who have been together 82 years

anniversary
The loved-up pair from Dover are one of the country's oldest married couples having tied the knot in 1936, and 75 years later are still going strong. They have clocked up almost 200 years between them, 162 of which have been spent in marital bliss

MGAO WA MECHI YA SOKA, BMT YAPATA SHLINGI 51/- TU.


Boniface Wambura.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema jana kuwa kiasi
cha Sh 45,000 kilipatikana kutokana na watazamaji 15 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo, ambalo Lyon ilishinda mabao 2-0.
“Baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni Sh 6,864.41 kila timu ilipata Sh 2,591, Uwanja Sh 514, TFF Sh 514, DRFA Sh 205, FDF Sh 257 na BMT Sh 51, “ alisema Wambura.
Pia Wambura alisema mechi ya Simba na JKT Oljoro iliyofanyika Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza Sh 40,191,000.


“Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT), kila timu ilipata Sh 7,023,171, uwanja Sh 2,341,057, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Sh 936,423, TFF Sh 2,341,057, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh 1,170,528 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Sh 234,106,” alisema Wambura.

Jumamosi, 4 Februari 2012

BUNGE LAJADILI MGOMO WA MADAKTARI.

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, imepewa jukumu la kuangalia mgogoro
uliopo kati ya madaktari na Serikali kwa lengo la kulishauri Bunge namna ya kumaliza
mgogoro huo na kuhakikisha hali hiyo hairudii.

Pamoja na uamuzi huo, Bunge pia jana kupitia Naibu Spika, Job Ndugai, limetaka madaktari warejee kazini mara moja na kuacha mgomo. Agizo la mgogoro huo kupelekwa katika Kamati hiyo, lilitolewa na Ndugai, wakati akijibu Mwongozo wa Spika ulioombwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika (Chadema), kabla ya Serikali kuwasilisha kauli yake juu ya mgomo huo.

Mnyika aliomba Mwongozo kwa kuzingatia Kanuni ya 5 ili kauli ya Waziri ijadiliwe na wahusika wawajibishwe. Hoja ya kujadiliwa kwa kauli ya Serikali ilihitaji kwanza kutenguliwa kifungu cha 49 cha Kanuni za Bunge lakini haikuweza baada ya wabunge kutounga mkono hoja ya Mbunge wa Kasulu Mjini, Moses Machali (NCCR-Mageuzi), ambaye alizungumzia haja ya kutumia Kanuni ya 55 (3) na Kabwe Zitto aliyetaka hoja ijadiliwe.

Hata hivyo, kwa kutumia busara zake, Ndugai, aliagiza Kamati ikae na kujadili suala hilo kwa kukutanisha pande zote - madaktari na Serikali, kabla ya kulifikisha katika Bunge kwa ushauri ambao si lazima uwe agizo. Alisema kurejesha suala hilo kwa Kamati ambayo Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Viti Maalumu, Magreth Sitta (CCM) na Makamu wake ni mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile (CCM), kulitokana na haja ya kusikiliza pande hizo zenye mgogoro na kufuatilia shauri lingine ambalo halikuwekwa wazi bungeni la wizara kuwa na baadhi ya viongozi wasiowajibika na wenye lugha za kashfa.

Alisema wamesikia upande mmoja na kwa kuwa upande wa pili (madaktari) haukuwapo, ni
vema ukawepo utaratibu wa kuusikiliza pia. Pamoja na kuwa hakuna muda uliopangwa, uamuzi wa Naibu Spika uliungwa mkono na Bunge, kwa kushangiliwa na pande zote. Spika aliitaka Kamati hiyo ifanye kazi haraka na itoe taarifa kuhusu yaliyojiri kwenye mazungumzo
hayo na ushauri wa Bunge kwa pande husika.

Ndugai aliomba pande zinazosigana kutoa ushirikiano kwa Kamati hiyo, ambayo vikao vyake, wabunge wengine wenye nia wanaruhusiwa kuhudhuria. Kamati hiyo inatarajiwa kukutana na Serikali, Chama cha Madaktari, Jumuiya ya Madaktari na madaktari bingwa. Pamoja na kurejesha tamko hilo kwa Kamati hiyo, jana kabla ya kuahirisha kikao cha asubuhi, Ndugai aliwataka madaktari kwa niaba ya wabunge kurejea kazini kusaidia Watanzania wenzao.

“Tunawapenda madaktari, warudi kazini waheshimu viapo vyao,” alisema Ndugai. Awali Bunge lilielezwa hatua zilizofanywa na Serikali katika kutafuta suluhu ya mgomo wa madaktari na kusema kwamba kila masharti mapya yalipojitokeza yalionesha, kwamba madaktari hawataki suluhu. Kauli ya Serikali Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, akiwasilisha bungeni kauli ya Serikali, alisema pamoja na hayo yote, imeundwa Kamati ya kushughulikia tatizo hilo na kutaka wadau wote kuipa maoni.

“Serikali imedhamiria kwa dhati kulitatua tatizo lililopo mbele yetu. Kwa mantiki hiyo, tunawasihi madaktari, wataalamu wengine wa sekta ya afya na wadau wote wa sekta hiyo, kutumia fursa iliyo mbele yetu, kutoa maoni yao kwenye kamati iliyoundwa na Serikali ili kupata namna bora ya kutatua mgogoro uliojitokeza,” alisema Dk Mponda.

Januari 30, Serikali iliunda kamati ya kushughulikia maazimio yaliyowasilishwa kwa Waziri Mkuu, ili kuyachambua na kutoa maoni na mapendekezo yatakayoisaidia Serikali kumaliza mgogoro wa watumishi wa sekta ya afya. Aidha, Dk. Mponda aliwaeleza wabunge, kwamba Serikali inasikitika kwa athari zilizotokea kwa wananchi kutokana na mgogoro huo.

Hata hivyo, aliliambia Bunge, kwamba huduma zimeanza kutengamaa katika hospitali ya
Taifa Muhimbili (MNH) lakini huduma za dharura na wodini katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili
(MOI) zimedorora kwa kuwa madaktari 21 hawajarudi kazini. “Mipango ya kupeleka madaktari
kutoka jeshini inakamilishwa, ili huduma za wagonjwa wa nje (OPD) zirejeshwe,” alisema
Mponda. Aliongeza kwamba madaktari walio kwenye mafunzo kwa vitendo kwenye maeneo mengi, wengi bado hawajarudi kazini Muhimbili.

Alilieleza Bunge kuwa, huduma zinatolewa kama kawaida katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, na pia hali ni kama hiyo katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando, Mwanza. Alisema, madaktari 81 walio kwenye mafunzo kwa vitendo kwenye Hospitali ya Rufaa ya KCMC Moshi wamerudi kazini, hivyo huduma zinaendelea kama kawaida.

Hali Bugando

Naye Clara Matimo, anaripoti kutoka Mwanza, kwamba uongozi wa Bugando umesema matibabu kwa wagonjwa yanakwenda kama kawaida licha ya baadhi ya vitisho kutoka kwa wafanyakazi wachache wanaoeneza uvumi wa kuwapo mgomo wa madaktari.

Mkurugenzi wa Bugando, Dk Charles Majinge, alisema jana kwamba tangu mgomo wa madaktari uanze katika baadhi ya hospitali za serikali nchini, Bugando bado inaendelea na matibabu na wagonjwa wanapata huduma kama kawaida. "Sisi katika hospitali yetu ya rufaa Bugando, tunafanya kazi kwa maadili zaidi ambayo yanaendana na yale ya kiroho, ukizingatia kuwa hospitali hii inaendeshwa kwa misingi ya dini ya Kanisa Katoliki… tunajali afya zaidi za jamii kuliko kuweka maslahi mbele," alisema Dk. Majinge.

Alitoa ushauri kwa madaktari wengine nchini wanaoendelea na mgomo, kufanya subira wakati Serikali inatafakari namna ya kuboresha maslahi yao, kuliko kuacha wagonjwa wanateseka na baadhi yao kufariki dunia kutokana na mgomo huo wa madaktari. Wanaogoma Aidha, alisema wanaoendelea kugoma katika hospitali hiyo ni wanafunzi ambao wanachukua mafunzo ya udaktari bingwa ambao mara kwa mara wamekuwa wakipiga simu kwa baadhi ya wagonjwa
wanaotaka kutibiwa katika hospitali hiyo, kuwa wasifike kutokana na hospitali kuendelea na
mgomo.

Hata hivyo, uchunguzi wa 'Habarileo' katika baadhi ya wodi pamoja na kufanya mahojiano na baadhi ya madaktari katika hospitali hiyo, ambao walisema wako kwenye mgomo baridi na kwamba wanaofanya kazi katika hospitali hiyo ni wakuu wa vitengo pekee na si madaktari. Baadhi ya wodi wagonjwa waliokuwa wamelazwa, waliondolewa na ndugu zao kwenda kutibiwa katika hospitali zingine za binafsi

Ijumaa, 3 Februari 2012

SIKU YA SHERIA TANZANIA YAADHIMISHWA MAHAKAMA YA WILAYA NACHINGWEA LEO KWA MAHAKAMA YA WAZI.

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nachingwea akimsomea mashtaka mtuhumiwa ajulikanae ka ma Tuju wa Matangini Nachingwea ya kosa la kupatikana napombe haramu ya Gongo nusu lita leo asubuhi katika siku ya kuadhimisha mwanzo wa kalenda ya Mahakama Tanzania.




Tuju akiwa kizimbani. Ujunbe a siku ya sheria leo ni 'adhabu mbadala'

Alhamisi, 2 Februari 2012

KOMBE LA MATAIFA HURU YA AFRIKA, MATOKEO NA RATIBA.


GROUP A
Equatorial Guinea 1 Libya 0
Click here to read the match report
Senegal 1 Zambia 2
Click here to read the match report
Libya 2 Zambia 2
Click here to read the match report
Equatorial Guinea 2 Senegal 1
Click here to read the match report
Equatorial Guinea 0 Zambia 1
Click here to read the match report
Libya 2 Senegal 1
Click here to read the match report
Click HERE for the Group A table
GROUP B
Ivory Coast 1 Sudan 0
Click here to read the match report
Burkina Faso 1 Angola 2
Click here to read the match report
Sudan 2 Angola 2
Click here to read the match report
Ivory Coast 2 Burkina Faso 0
Click here to read the match report
Sudan 2 Burkina Faso 1
Ivory Coast 2 Angola 0
Click here to read the match report
Click HERE for the Group B table
GROUP C
Gabon 2 Niger 0
Click here to read the match report
Morocco 1 Tunisia 2
Click here to read the match report
Niger 1 Tunisia 2
Click here to read the match report
Gabon 3 Morocco 2
Click here to read the match report
Gabon 1 Tunisia 0
Click here to read the match report
Niger 0 Morocco 1
Click here to read the match report
Click HERE for the Group C table
GROUP D
Ghana 1 Botswana 0
Click here to read the match report
Mali 1 Guinea 0
Click here to read the match report
Botswana 1 Guinea 6
Click here to read the match report
Ghana 2 Mali 0
Click here to read the match report
Mali 2 Botswana 1
Click here to read the match report
Ghana 1 Guinea  1
Click here to read the match report
Click HERE for the Group D table
 
QUARTER-FINALS
Feb 4, Match 25, Bata, Equatorial Guinea
Group A winner vs. Group B runner-up, 1600 GMT
Match 26, Malabo, Equatorial Guinea
Group B winner vs. Group A runner-up, 1900 GMT
Feb 5, Match 27, Libreville, Gabon
Group C winner vs. Group D runner-up, 1600 GMT
Match 28, Franceville, Gabon
Group D winner vs. Group C runner-up, 1900 GMT
SEMI-FINALS
Feb 8, Bata, Equatorial Guinea
Match 25 winner vs. Match 28 winner, 1600 GMT
Libreville, Gabon
Match 27 winner vs. Match 26 winner, 1900 GMT
THIRD PLACE
Feb 11, Malabo, Equatorial Guinea, 1900 GMT
FINAL
Feb 12, Libreville, Gabon, 1900 GMT