KARIBU KATIKA BLOGU HII YA KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUONYA KUPITIA MADA MBALIMBALI NA HATA PICHA. ONGEZA MAHUSIANO KWA KUJUMUIKA NA WENZIO HAPA.UNAWEZA TUMA PICHA NA MAELEZO KWA ANUANI HII;mkuu74@gmail.com
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo PICHA YA LEO. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo PICHA YA LEO. Onyesha machapisho yote
Jumapili, 22 Julai 2012
Jumapili, 15 Julai 2012
Jumatatu, 2 Julai 2012
PICHA YA LEO; KABLA HUJAFA HUJAUMBIKA, DK. ULIMBOKA APELEKWA AFRIKA KUSINI KWA MATIBABU.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini Dk Stephen Ulimboka wakati Waziri Mkuu alipokutana na Madaktari Jijini Dar es Salaam hivi karibuni, kweli kabla hujafa hujaumbika, Daktari huyu hivi sasa yupo nchini Afrika ya Kusini alikoenda kutibiwa baada ya kushambuliwa na kuumizwa vibaya na watu wasiojulikana majuzi.
Jumamosi, 2 Juni 2012
Ijumaa, 25 Mei 2012
PICHA YA LEO; MSAFIRI KAFIRI.
Punda afe mzigo ufike, unaikumbuka methali hii? Bahati yao ni kwamba gari ni zuri tu na barabara pia ni nzuri, sasa tatizo sijui ni nini? Anataka kuharibu gari lake maana kalichoka ili anunue jingine!!! sijui, au anabana mafuta kwa kuogopa kurudiarudia safari, mzigo ukifika faida njenje kwa mwenye mzigo ila ni hasara ya service ya gari kwa mwenye chombo. Tutafakari kwa pamoja je haya ni matumizi sahihi ya nyenzo zetu tulizonazo zinazotusaidia kazi mbalimbali!!?
Jumatano, 25 Aprili 2012
Jumatano, 18 Aprili 2012
Jumanne, 20 Machi 2012
PICHA YA LEO; MAJ. JENERALI SAMWEL NDOMBA NI MKUU MPYA WA JKT.
Mh. Rais Kikwete akiwa pamoja na Mkuu mpya wa JKT kulia Maj. Gen. Samwel Ndomba mara baada ya kumwapisha hivi karibuni, kushoto ni Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Generali Mwamunyange.
Jumatano, 29 Februari 2012
Alhamisi, 2 Februari 2012
PICHA YA LEO; SHIDA HULETA MAARIFA,MBINU SALAMA YA KUVUKA BARABARA KWA WANAFUNZI
Waliyosema wahenga kuwa "shida huleta maarifa" "shida huleta akili" hawakukosea kwani, kwani mfano huu wa picha inayoonekana hapa ambapo watoto wanavuka barabara kwa kushikana mikono na na kuvuka kwa pamoja, ni njia nzuri ya kuepukana na shida za waendesha vyombo vya usafiri barabarani ambao baadhi yao si makini katika kuwaruhusu waenda kwa mguu kuvuka barabara. Wengine hawajali kabisa watoto wadogo ambao ndiyo wanajifunza matumizi ya barabara.
Kila leo wanafunzi wanagogwa na kuachwa na vilema huku wengine wakipoteza uhai wao.
Mbinu hii ya kuvuka barabara nadhani ni sahihi zaidi hasa maeneo yasiyo na alama za pundamilia za kuvukia barabara.
Kila leo wanafunzi wanagogwa na kuachwa na vilema huku wengine wakipoteza uhai wao.
Mbinu hii ya kuvuka barabara nadhani ni sahihi zaidi hasa maeneo yasiyo na alama za pundamilia za kuvukia barabara.
Jumamosi, 21 Januari 2012
Ijumaa, 9 Desemba 2011
PICHA YA LEO;MKESHA WA MIAKA HAMSINI YA UHURU, SANAMU YA BISMIN(ASKARI) YANG'AA PALE MITAA YA SAMORA NA AZIKIWE KUAMKIA LEO.
Leo ni miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Hata hivyo, shamra shamra za kufikia kilele zilianza muda na jana kulikuwa na mkesha nchi nzima ulioandamana na mapambo ya kila namna. Hapa ni eneo maarufu la Mnara wa Askari jijini Dar es Salaam likimeremeta jana usiku na kubadilisha mandhari yake yaliyozoeleka ikiwa ni sehemu ya kukaribisha siku hii muhimu ya leo. (Picha na Robert Okanda).
Jumamosi, 3 Desemba 2011
PICHA YA LEO; SIFA ZA KIJINGA, SASA HAPO ANASAIDIA NINI ILI KULINASUA GARI ZAIDI YA KUHATARISHA MAISHA YAKE!!?
Mkazi wa Iramba akihatarisha usalama wake kwa kuingia chini ya gari la Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, Mwigullu Lameck Nchemba kulinasua gari hilo lililokuwa limekwama kwenye mto Ndurumo Kata ya Kidaru Mkoani Singida juzi. (Picha na Abby Nkungu) |
Ijumaa, 4 Novemba 2011
PICHA YA UHURU; MIAKA 50 YA UHURU.
Miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika, harakati za kupigania Uhuru zilianza kabla, 1954 TANU ilianzishwa, pichani Mwl. Julius Nyerere na wanaharakati wenzie wakielekea kwenye Mkutano wa Chama cha TANU.
Jumanne, 1 Novemba 2011
PICHA YA LEO; SHOKA LANASA KICHWANI BAADA YA KUPIGWA NA MAJAMBAZI
Juzi saa 12 asubuhi hospitali ya taifa Muhimbili imempokea mgonjwa anayeitwa Mussa Shabani(42) akiwa na shoka iliyonasa kichwani kwake kama picha inavyooneka.
Imeelezwa kuwa Mussa ni mlinzi katika nyumba ya Joseph Mwakyusa huko Tabata, Majambazi yalipofika nyumbani kwa
Mwakyusa yalimjeruhi kwa shoka mlinzi huyo yalifungua spea za gari aina ya Toyota verosa.
Mwakyusa yalimjeruhi kwa shoka mlinzi huyo yalifungua spea za gari aina ya Toyota verosa.
Kwa bahati nzuri Mwakyusa alishtuka na ndipo majambazi hayo yalipokimbia na kutoweka yakimuacha mussa katika hali mbaya na shoka ikiwa imenasa kichwani.
Madaktari wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI walifanya kazi ya ziada kuitoa shoka hiyo na sasa Mussa yupo chumba cha wagonjwa mahututi.
Madaktari wa taasisi ya tiba ya mifupa MOI walifanya kazi ya ziada kuitoa shoka hiyo na sasa Mussa yupo chumba cha wagonjwa mahututi.
Jumaa Almasi ambaye ni afisa uhusiano mkuu wa MOI amethibitisha tukio hilo na kusema ''Ni kweli Mussa amepokelewa hapa MOI akiwa na shoka iliyonasia kichwani mwake lakini madaktari wamemfanyia upasuaji na kuitoa na sasa hivi yupo chumba cha wagonjwa mahututi''
Alhamisi, 27 Oktoba 2011
ZITTO KABWE KALAZWA HOSPITALI MUHIMBILI.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akiwa amelazwa katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili. Kushoto ni rafiki wa yanke , Alex Kitumo. Picha na Venance Nestory
Jumanne, 25 Oktoba 2011
PICHA YA LEO;HAKI YA KIKATIBA, RAIS WA ZANZIBAR AAPISHWA ILI AINGIE KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI JMT.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Othuman Chandeiakimwapisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohammed Shein kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ikulu Dar es Salaam huku Rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo (katikati) wakishuhudia. (Picha na Yusuf Badi).
Jumamosi, 15 Oktoba 2011
Jumamosi, 8 Oktoba 2011
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)