Boniface Wambura.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema jana kuwa kiasi cha Sh 45,000 kilipatikana kutokana na watazamaji 15 waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo, ambalo Lyon ilishinda mabao 2-0.
“Baada ya kuondoa asilimia 18 ya VAT ambayo ni Sh 6,864.41 kila timu ilipata Sh 2,591, Uwanja Sh 514, TFF Sh 514, DRFA Sh 205, FDF Sh 257 na BMT Sh 51, “ alisema Wambura.
Pia Wambura alisema mechi ya Simba na JKT Oljoro iliyofanyika Jumatano Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam iliingiza Sh 40,191,000.
“Baada ya kuondoa gharama za awali za mchezo na asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT), kila timu ilipata Sh 7,023,171, uwanja Sh 2,341,057, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) Sh 936,423, TFF Sh 2,341,057, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) Sh 1,170,528 na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Sh 234,106,” alisema Wambura.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni