Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, Naye ni Mkwele wa Lugoba Bagamoyo. |
“Tumechoka na mahubiri ya huyu Padri, kila akihubiri kanisani lazima atuseme Wakwere,
tumemkosea nini? Mara atuseme tu masikini, mara watoto wetu wachafu na hatuwapeleki shule tunashindia ngoma, tumechoka, hatumtaki,” alisema muumini ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
“Leo tumemzuia asisome misa kabisa, hakuna haja maana hakuna amani kanisani, hatujui ana kitu gani na sisi, sijui kwa sababu parokia hii ipo kwa Wakwere? “Hata Jumatano ya Majivu wiki iliyopita katusema tena, eti watoto wetu ni wachafu sana ukilinganisha na makabila mengine, hii ni kashfa.”
Wakwere ni moja ya makabila katika Mkoa wa Pwani linalopatikana wilayani Bagamoyo, Pia Rais wa Tanzania ni Mkwere. Muumini mmoja alidai mahubiri ya Padri huyo ya kuwasema Wakwere hayakuanza siku za karibuni, bali ni ya muda mrefu na yamekuwa kama ya kusutwa badala ya kulishwa Neno la Mungu.
“Hali hiyo imesababisha watu kutokwenda kanisani wakijua leo Padri huyo anaongoza misa, lakini akiongoza Katekista, misa inajaa utadhani Askofu amekuja, tunachotaka hapa ni Padri mwingine, kama Askofu anatujali atuletee mwingine,” alisema muumini huyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni