Hapa anaonekana Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Lindi Bw. Stephen Chami (mwenye suti nyeupe) akiongea na viongozi wa Chama cha Msingi cha Mazao na Masoko cha Naipanga wilayani Nachingwea kabla ya kuanza kwa mkutano na wanachama wa chama hicho ambao walielimishwa namna ya mapambano dhidi ya rushwa yanavyoendeshwa na jitihada za serikali katika kupambana na adui rushwa, pamoja na hayo wanachama walielezwa maendeleo ya uchunguzi dhidi ya wajumbe wa bodi ya zamani walioachishwa uongozi na mkutano mkuu wa chama mwezi julai 2011 kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa mali za chama ikiwemo ununuzi wa gari ya chama aina ya Fusso ambalo lilikataliwa na wanachama kwa sababu lilinunuliwa kinyume na utaratibu. Mwenye shajara mkononi ni Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Nachingwea Bw. Moses Oguda.
Kamanda Chami akiongea na wanachama wa Naipanga AMCOS.
Katibu wa Naipanga AMCOS akisoma taarifa fupi ya Mwenyekiti wa Chama, wa kwanza kabisa ni Mwenyekiti wa sasa wa Chama hicho Bw. Misere.
Wanachama wa Chama cha Msingi Naipanga wakimsikiliza Kamanda Stephen Chami (hayupo pichani)
Kamanda wa Polisi wa wilaya SSP Thabit Milanzi alikuwepo, hapa akibadilishana mawazo na viongozi wengine mara baada ya mkutano na wanachama kumalizika. Wanachama walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa dukuduku zao mbalimbali.
Hilli ni jengo la PADEP kijiji cha Naipanga ambapo mkutano ulifanyikia.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni