Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NACHI. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NACHI. Onyesha machapisho yote

Jumapili, 17 Juni 2012

MWENGE WAKIMBIZWA HUKO NACHINGWEA MKOANI LINDI.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Bi. Mrindoko akisoma Risala ya Utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati Mwenge wa Uhuru ulipokimbizwa wilayani humu juma lililopita.


Mwenge ulishikwa na baadhi ya wafanyakazi na wananchi wengine wilayani Nachingwea.


Ujumbe wa Mwenge ni Hamasa juu ya zoezi la sensa mwaka 2012, pia vita dhidi ya ukimwi, madawa ya kulevya na rushwa.


Watoto wakiangalia machapisho mbalimbali katika Banda la TAKUKURU wilaya ya Nachingwea ambao nao walikuwepo kufikisha ujumbe juu ya mapambano dhidi ya Rushwa.

Jumapili, 8 Aprili 2012

MH. CHIKAWE(MB) ATEMBELEA HOSPITALI YA WILAYA NACHINGWEA KUKAGUA JENGO LA MAABARA, KUONA WAGONJWA NA KUTOA MSAADA WA VIFAA JUMAMOSI YA PASAKA.

Mh. Chikawe akiwasili eneo la hospitali na kusalimiana na wadau mbalimbali wa afya wilayani Nachingwea hapo jana asubuhi.
Mh. Chikawe akisalimiana na mgonjwa mmojawapo katika wadi ya wanaume ambaye amevunjika mguu na mkono baada ya kupigwa na majambazi hivi karibuni. Pia Mh. Chikawe aliahidi kumsaidia usafiri na masurufu mzazi wa mtoto Khatibu Hashim(4) anayesumbuliwa na uvimbe kichwani na kapata rufaa kwenda Muhimbili Hospitali ya Dar es Salaam.
Hapa ni ndani ya jengo jipya la maabara, limejengwa kwa msaada toka Clinton Foundation ya Marekani.
Hapa akikabidhi vifaa mbalimbali ikiwemo kitanda cha kuzalishia na baiskeli ya kukalia wagonjwa.
Hapa Daktari Mfawidhi wa Nachingwea akipeana mkono na Mh. Chikawe kama ishara ya kumshukuru kwa msaada wake huo.

Jumamosi, 31 Machi 2012

PICHA YA LEO; KABURI LA MBWA HUKO NACHINGWEA.

Hili linaloonekana hapa ni kaburi la Mbwa wa Mzungu mmoja aliyejulikana kwa jina la Phills aliyewahi kuishi hapa Tanzania wilayani Nachingwea akifanya shuguli zake za kilimo cha karanga miaka ya 1950. Kaburi hili lipo maeneo ya Boma  Airport Road hapa mjini Nachingwea na limejengewa vizuri kwa zege imara ingawa limeanza kuhujumiwa kwa kuondolea kibao cha shaba kilichokuwa kinaelezea jina la mbwa huyo na uzio mdogo kubomolewa. 
Kwa nini mbwa ajengewe kaburi zuri la kudumu kama binadamu!!?
Mbwa huyu alikuwa maarufu enzi hizo kwani alikuwa msaidizi mkubwa kwa kazi za nyumbani za Mzungu Phills ikiwemo ulinzi wa makazi pia kutumwa sehemu mbalimbali ikiwemo sokoni kununua bidhaa.
Mbwa huyo marehemu alikuwa na akili za kuweza kwenda sokoni akiwa na kikapu na pesa na maelekezo ya maandishi ya bidhaa za kununua na duka au kibanda husika cha sokoni, muuzaji husoma maelekezo na kumpatia mbwa bidhaa kwenye kikapu shingoni hata kama ni nyama na huzifikisha kwa mwenyewe aliyemtuma ambaye ni Mzungu Phills. Baada ya kifo chake mzungu alihudhunika sana na kuamua kujenga kaburi zuri la kumbukumbu ya Mbwa wake ambalo lipo hadi leo maeneo ya Kilimani Boma Nachingwea. 

Jumatano, 22 Februari 2012

TAKUKURU NACHINGWEA YAFANYA MKUTANO WA UELIMISHAJI UMMA JUU YA MADHARA YA RUSHWA NA WANACHAMA WA NAIPANGA AMCOS.

Hapa anaonekana Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa mkoa wa Lindi  Bw. Stephen Chami (mwenye suti nyeupe) akiongea na viongozi wa Chama cha Msingi cha Mazao na Masoko cha Naipanga wilayani Nachingwea kabla ya kuanza kwa mkutano na wanachama wa chama hicho ambao walielimishwa namna ya mapambano dhidi ya rushwa yanavyoendeshwa na jitihada za serikali katika kupambana na adui rushwa, pamoja na hayo wanachama walielezwa maendeleo ya uchunguzi dhidi ya wajumbe wa bodi ya zamani walioachishwa uongozi na mkutano mkuu wa chama mwezi julai 2011 kutokana na tuhuma za ubadhirifu wa mali za chama ikiwemo ununuzi wa gari ya chama aina ya Fusso ambalo lilikataliwa na wanachama kwa sababu lilinunuliwa kinyume na utaratibu. Mwenye shajara mkononi ni Kamanda wa TAKUKURU wilaya ya Nachingwea Bw. Moses Oguda.

Kamanda Chami akiongea na wanachama wa Naipanga AMCOS.

Katibu wa Naipanga AMCOS akisoma taarifa fupi ya Mwenyekiti wa Chama, wa kwanza kabisa ni Mwenyekiti wa sasa wa Chama hicho Bw. Misere.

Wanachama wa Chama cha Msingi  Naipanga wakimsikiliza Kamanda Stephen Chami (hayupo pichani)

Kamanda wa Polisi wa wilaya SSP Thabit Milanzi alikuwepo, hapa akibadilishana mawazo na viongozi wengine mara baada ya mkutano na wanachama kumalizika. Wanachama walipata fursa ya kuuliza maswali na kutoa dukuduku zao mbalimbali.

Hilli ni jengo la PADEP kijiji cha Naipanga ambapo mkutano ulifanyikia.

Jumamosi, 11 Februari 2012

KAMANDA WA TAKUKURU MKOA WA LINDI ATEMBELEA SEKONDARI KUHAMASISHA VILABU VYA WAPINGA RUSHWA.

Kamanda Steven Chami akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Naipanga Nachingwea juzi.
Wanafunzi wakisikiliza mawaidha ya kamanda
Viongozi wa wanafunzi wakitoa neno la shukurani.

Jumapili, 22 Januari 2012

DUKA LA VINYWAJI BARIDI LANUSURIKA KUUNGUA MOTO STENDI YA MABASI NACHINGWEA JANA USIKU.


Viti vya plastiki vilivyoungua ndio bidhaa pekee iliyoathirika na moto huo.

Kumekuwa na tabia au dhana ya kulitaja sana Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuwa linahusika sana na kusababisha moto sehemu mbalimbali, lakini jana Mambobado ilishuhudia moto katika moja ya vibanda vya biashara kuzunguka Stendi kuu ya mabasi Nachingwea mida ya saa tano usiku uliosababishwa na mkaa wa moto uliohifadhiwa ndani ya kibanda hicho kwa ajili ya matumizi ya siku inayofuata.

Wasamaria wema wakishuhudia tukio hilo mara baada ya kuzimwa kwa moto huo ambao ulisababisha hasara kidogo maana ulizimwa kabla haujakolea na pengine kuhamia vibanda vingine. Ilibidi wasamaria wema wavunje mlango huo baada ya kusikia harufu ya vitu vinavyoungua na mwanga wa moto kuonekana kwa ndani, mwenye mali alijulishwa baadae na alikuta vitu vyake salama.

Jumamosi, 21 Januari 2012

MAKAMU WA RAIS AMALIZA ZIARA YA SIKU MBILI WILAYANI NACHINGWEA, AWEKA JIWE LA MSINGI SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA.

Makamu wa Rais Dk. Mohamed Bilal akifunua kitambaa kuashiriwa kuzinduliwa kwa Shule mpya ya Sekondari ya Wasichana ya Nachingwea hapo jana, alikuwa katika ziara ya siku mbili wilayani Nachingwea kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo mradi wa maji safi ujulikanao kama Mbwinji iinaotarajia kukamilika hivi karibuni unaojengwa na Wachina.
Kikundi cha ngoma kikifanya mazoezi ya kujiandaa kabla ya mgeni rasmi Makamu wa Rais hajawasili katika viwanja hivyo vya shule mpya ya Wasichana Nachingwea.
Wananchi wakisubiri kumsikiliza mgeni rasmi katika maeneo ya shule hiyo jana, leo amemaliza ziara yake hapa na ameelekea wilaya ya Lindi kwa ziara kama hiyo.

Jumanne, 17 Januari 2012

WANAKIJIJI WA IKUNGU WILAYANI NACHINGWEA WALALAMIKIA MWEKEZAJI ANACHAFUA MAZINGIRA KWA MADAWA YA SUMU KALI.

Kampuni inayojishughulisha na uchakachuaji wa mchanga uliobakizwa baada ya kuondoa dhahabu ijulikanayo kwa jina moja tu la MANJANJO iliyopo maeneo ya mlima Ikungu wilayani Nachingwea mkoani Lindi inalalamikiwa na wanakijiji kuwa inachafua mazingira pale dawa aina ya CYNADE inayotumika kukamata dhahabu katika hali ya kimiminika inapoingia katika vyanzo vya maji hasa wakati huu wa mvua za masika. Hali hii imezua sintofahamu kwa uongozi wa kijiji na wanakijiji halikadhalika na kupelekea wananchi kutaka Kampuni hiyo ifukuzwe kabisa eneo hilo.
Mambobado ilipata nafasi ya kutembelea eneo la mgodi ikiambatana na uongozi wa serikali ya wilaya na wawakilishi wa uongozi wa kijiji cha Ikungu ili kujionea hali halisi baada ya madai kuwa baadhi ya mbuzi walikufa baada ya kunywa maji yaliyochanganyika na dawa yenye sumu mara baada ya mkutano na wanakijiji na serikali yao ambayo wajumbe asilimia 90 walitangaza kujiuzulu nyadhifa zao kwa vile serikali haisikilizi kilio chao wakati wanaathirika na sumu. Tukiongea na mkemia wa kampuni hiyo alisema kuwa madai kuwa mbuzi wamekufa na dawa kuingia kwenye mkondo wa maji si kweli ila ni chuki za kisiasa kati ya wanakijiji kwa kulishana maneno ya uwongo ili waichukie kampuni yao.
Aliendelea kusema kuwa wao huvundika udongo uliotumika na wachimbaji wengine kama picha ya juu inavyoonesha na baadae huchanganya na maji yenye dawa iitwayo CYNADE katika mashimo maalumu yaliyojengewa kwa simenti pembeni ambapo dhahabu isiyoonekana kwa macho hujichanganya na maji yenye dawa na kuingia eneo maalumu kama inavyoonekana picha hii ya juu ambapo baadae huchangayika na makaa ya mawe na kukusanywa katika viroba na kupelekwa Mwanza kwa ajili ya kuchomwa ili kupata dhahabu halisi.
Hapa ndipo dhahabu huchanganyika na makaa ya mawe na kuopolewa tayari kwenda kuchomwa Mwanza ili kutenganisha makaa na dhahabu, baadae maji yenye dawa iliyopoa hurudishwa tena kwenye mzunguko wa kwanza na kuongezwa dawa tena iwapo imepungua. Mtaalamu alisema maji haya yaliyotumika hawayaachii ila wanayatumia tena na hayana madhara isipokuwa katika hatua ya mwanzo kabla hayajatumika, aliyashika maji haya na kunawa ingawa alisema yana madhara iwapo yataingia machoni, mdomoni au kwenye vinyweleo ambapo huduma ya kwanza itatakiwa ili kuzuia madhara.
Hapa ni maji yaliyojichuja toka kwenye udongo uliotumika na kuchanganyika na maji ya mvua ambapo walionekana vyura ndani yake wakicheza kwa maana kuwa hayana sumu, pamoja na hayo hakuna maji yanayoachiwa kuingia kwenye mkondo wa maji. Watalamu wa mazingira wametaarifiwa  pamoja na wale wa madini ili waje kutatua mgogoro huu, Afisa Afya pia ametoa maelekezo ya nini kifanyike ili kuboresha miundombinu.





Jumatatu, 16 Januari 2012

REGIA MTEMA KUAGWA KESHO KARIMJEE

Mbunge huyo alifariki juzi saa 5:15 baada ya kupata ajali mbaya ya gari katika eneo la Ruvu JKT, mkoani Pwani baada ya gari alilokua akiendesha kupinduka zaidi ya mara mbili.
Gari lililopata ajali na kusababisha kifo cha Mh. Mtema
Taarifa zilizotolewa na jeshi la polisi mkoani humo zilisema , marehemu Mtema alikuwa akiendesha gari aina ya LandCruiser namba T 296 BSM alipokuwa akitokea Dar es Salaam kuelekea mkoani Pwani.
Taarifa hiyo ilisema akiwa akiendesha gari hilo alipofika eneo hilo alitaka kulipita gari lililokuwa mbele yake lakini alishindwa kufanya hivyo ndipo gari lake lilipopinduka na kusababisha kifo chake.




Mh, Regia Mtema enzi za uhai wake.
Alisema Mtema alikuwa akiendesha gari aina ya Landcruiser lenye namba T 296 BSM, akitokea Dar es Salaam kuelekea Chalinze.
Taarifa zaidi zilieleza kwamba Mtema alikuwa anakwenda kukagua kiwanja chake mkoani humo na umauti kumfika njiani, pia marehehmu ameacha pacha wake ambaye alinusuruka na kifo hicho muda mchache tu alipomshusha pacha wake.
Mwili huo unatarajiwa kuagwa kesho katika viwanja vya Karimjee na kuzikwa keshokutwa huko Ifakara nyumbani kwao

Jumatatu, 9 Januari 2012

PICHA YA LEO;WANAJUA MADHARA YAKE!!?

Picture
Wananchi wakiwania kuchota mafuta toka katika gari ya mafuta iliyoaguka huko Iringa maeneo ya Ihemi  barabara ya Mbeya -Dar es salaam.
Picture
Walinda usalama nao walikuwepo lakini hawakuchukua hatua yoyote, hatujifunzi kutokana na makosa kwa nini!!? Picha toka francis gordwin blog.

Jumamosi, 31 Desemba 2011

HERI YA MWAKA MPYA 2012.

IT IS HEREBY SUBMITTED THAT  2011 HAS BEEN OVERTAKEN BY EVENTS, THEREFORE IT IS WITHDRAWN AND 2012 IS FILED.WITHOUT PREJUDICE TO THE FOREGOING, I DISPUTE ALL CLAIMS THAT 2011 IS THE END OF EVERYTHING. JUST FORGET AND FORGIVE THE PAST, LIFE GOES ON. MAY 2012 COMES WITH REVOLUTION, BE BLESSED. I ALSO SUBMIT THAT THE READER OF THIS MESSAGE WHETHER IS A LEARNED FRIEND OR A LAYMAN, THE AFFIDAVIT OF OUR FRIENDSHIP, PRAYERS AND GOOD WISHES FOR THE NEW YEAR 2012 IS ATTACHED HEREWITH, I CRAVE LEAVE FOR IT TO BE CONSTRUED AS PART OF THESE GREETINGS.

Jumamosi, 12 Novemba 2011

SAFARI YA KUSINI, HALI MBAYA YA BARABARA MAENEO YA NANGURUKURU.

Basi likishindwa kuendelea na safari kutokana na utelezi maeneo ya Nangurukuru Kilwa sehemu ambayo kuna matengenezo ya barabara na magari kupita pembeni(dirvesion), kasoro za barabara hizo ni kuwa hazijaimarishwa hivyo ikinyesha mvua kidogo tu magari hayapandi milima sababu ya utelezi.
Hii ni barabara inayorekebishwa na wengine waliamua kupita huku baada ya njia nyingine kutokupitika kwa msongamano
Safari ni hatua, baadae gari yetu iliharibika, Msafiri kafiri.

Ijumaa, 14 Oktoba 2011

TAKUKURU YABAINISHA UPUNGUFU KATIKA UGAWAJI VOCHA ZA PEMBEJEO.


TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Mbeya imetaja upungufu ilioubaini baada ya kufuatilia shughuli nzima ya ugawaji wa pembejeo za ruzuku kwa msimu wa kilimo uliopita.

Mkuu wa Takukuru mkoani hapa, Daniel Mtuka alisema hayo katika kikao chake na waandishi wa habari na kutaja upungufu uliobainika kuwa ni pamoja na baadhi ya wataalamu wakiwemo maofisa kilimo wilaya kulipwa kupitia dhana ya kujitolea.

Mtuka alisema kutokana na hali hiyo, ilikuwa rahisi mno kwa wataalamu na wajumbe wa Kamati kurubuniwa kwa kuwa wakati wakifanya shughuli hiyo, wanakuwa wakikabiliwa na changamoto nyingine ikiwemo za kushughulikia mahitaji ya familia zao.

“Utakuta mtu anajitolea kufanya shughuli hiyo inayogharimu fedha nyingi lakini nyumbani kwake wakati huo huo ana matatizo na pengine ya magonjwa na inakuwa rahisi kurubuniwa,” alisema.
Credits; Mwananchi Gazeti 

LEO NI KUMBUKIZI YA MIAKA 12 TANGU BABA WA TAIFA HILI ALIPOTUTOKA OKTOBA 14 1999, TUMWOMBEE APUMZIKE KWA AMANI.

Mwl. Nyerere akiwa na mgeni wake IDD amin DADA kabla hawajafarakana.
Mwenge wa Uhuru.
Akicheza bao na wazee wenzie akiwamo rais Mwinyi na mkewe mama Maria.
Jeneza la mwalimu.





Alhamisi, 6 Oktoba 2011

KISA CHA KAMBARAGE NYERERE 1952


 
Mwalimu Nyerere akiwa na Bibi Titi
Wazungu na Waasia hawakutaka kutambua kuwa Tanganyika ni nchi ya Waafrika
Katika makala iliyopita, Mwandishi MOHAMED SAID alielezea jinsi harakati za Uhuru zilivyowashikisha akina Hamza Mwapachu, Kasella Bantu na wengineo na baadaye akaongezeka Mwalimu Julius Nyerere aliyezitia nguvu zaidi harakati hizo….

KUONGEZEKA kwa Mwalimu Julius Nyerere kulitia nguvu sana baraza hii. Mijadala ya siasa miongoni mwa vijana hawa sasa ilivuka kutoka manung’uniko ya ndani ya nchi kama migomo ya wafanyakazi na matatizo ya ardhi ya Wameru na kuingia kujadili masuala ya kimataifa ya mrengo wa kushoto na hasa kuhusu kuwa na utawala wa Waafrika Tanganyika.
Kwa ufupi mijadala sasa ililenga katika kuutokomeza utawala wa Waingereza katika Tanganyika.
Nyerere alimwona Abdulwahid kama mtu mwenye akili sana, kijana aliyejiweza kihali na mtu mwenye moyo mkubwa usiokuwa na hasad wala choyo.
Watu walioishi na marehemu Abdulwahid wanasema alikuwa mtu karimu sana hujapatapo kuona na mwenye haiba ya kupendeka.
Abdulwahid alimuona Nyerere, kama mtu aliyeelimika vizuri kati yao na mwenye ustadi katika mijadala. Nyerere alipata nafasi ya kuifahamu dunia vizuri lau kama alikulia kijijini. Zaidi Nyerere alikuwa amepata uerevu wa siasa kutokana na uhusiano wake na Fabian Society, wakati alipokuwa mwanafunzi Uingereza.
Mijadala mizito sana ilijitokeza katika vile vikao vya kila Jumapili wakati akili na ujuzi wa siasa wa Abdulwahid vilipopambana na uhodari wa majadiliano wa Nyerere.
Abdulwahid alipata uzoefu mkubwa wa uongozi katika siasa nyumbani kwao kwa baba yake aliyeasisi African Association kisha wakati wa vita Burma na baada ya vita serikali ya kikoloni ilipomteua kuwa katibu wa kwanza wa chama cha wafanyakazi Dockworkers Union akiwa kijana mdogo wa miaka 24.
Nyerere hakuwa na ujuzi wowote katika siasa ukimlinganisha na Abdulwahid. Wakati African Association Tabora kiliposhiriki katika mgomo wa mwaka 1947, ambao chanzo chake kilikuwa mgomo wa makuli Dar es Salaam, Nyerere hakujihusisha na harakati zile za wafanyakazi ingawa yeye ndiye alikuwa katibu wa African Association pale Tabora.
Jukumu kubwa la mgomo ule lilibebwa na Salum Abdallah na wanachama wa kawaida katika African Association.
Salum Abdallah baada ya kuundwa kwa TANU, mwaka 1955 alikuwa rais muasisi wa Tanganyika Railway African Union (TRAU), katibu akiwa Christopher Kassanga Tumbo. TRAU na TANU vilishirikiana vizuri sana katika kupambana na serikali ya kikoloni.      
Kutokana na Nyerere kuingia katika harakati zile pale New Street pakawa na kuheshimiana na mapenzi makubwa baina yake, Abdulwahid, Ally Sykes, Dossa Aziz na John Rupia.
Kila Jumapili Nyerere alikuwa akisafiri kutoka Pugu hadi Dar es Salaam kuhudhuria baraza lile lililokuwa likijadili siasa za Tanganyika.
Baada ya kikao, Dossa Aziz au Dunstan Omar alimrudisha Nyerere kwa gari hadi Pugu. Hivi ndivyo Nyerere alivyokuja kuingia ndani ya TAA Makao Makuu na hatimaye akaja kupendekezwa kugombea cheo cha juu kabisa cha uongozi wa chama mnamo Aprili, 1953.
Uongozi wa TAA ulimpendekeza Julius Nyerere ili kukiimarisha chama kwa kuwa na Waafrika wenye elimu ya juu ndani yake. Ilibakia kwa Nyerere kukubali au kukataa. Kujadili siasa haikuwa sawa na kuongoza chama kilichokusudia kunyakua madaraka kutoka kwa serikali ya kikoloni.
Hivi vilikuwa ni vita dhidi ya ukoloni na ilibidi mtu ajitayarishe kwa lolote ambalo lingetokea.
Nyerere alikuwa ndiyo kwanza amerudi kutoka masomoni Uingereza mwaka uliopita na alikuwa anataka kutulia aanze maisha. Vijana wenzake wa mjini aliowakuta katika siasa pale Dar es Salaam kama Abdulwahid na mdogo wake Ally, na Dossa Aziz walikuwa watu wenye uwezo wao na wakiishi ndani ya mji wao ukilinganisha na yeye mgeni, tena amekulia kijijini
Katika mazingira kama yale ya Dar es Salaam ya miaka ya mwanzoni 1950 Nyerere kamwe hangeweza kujijengea nguvu ya siasa bila ya kushikwa mkono na wenyeji.
Uongozi wa TAA ulitambua thamani ya elimu ya Nyerere na uwezo wake wa uongozi kwa chama na nchi yenyewe hapo baadaye.
Abdulwahid pamoja na viongozi wenzake wa TAA waliamini kwamba kuwa na Mwafrika aliye na elimu ya juu kama rais wa chama kungeimarisha uongozi wa TAA na kutoa sura nzuri machoni mwa serikali ya kikoloni na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukitembela Tanganyika.
Nyerere amenukuliwa kusema kuwa ilikuwa dhamira yake kufundisha kwa muda kisha aingie kwenye siasa. Hatimaye Nyerere alishawishiwa kukubali kuchukua jukumu la kuongoza TAA.
Uchaguzi baina ya aliyekuwa rais wa TAA, Abdulwahid na mwalimu wa shule asiyefahamika vyema pale mjini, Julius Nyerere, ulifanyika kwenye Ukumbi wa Arnatouglo tarehe 17 Aprili, 1953.
Nje ya uongozi wa TAA ambao ulimpendekeza kugombea nafasi hiyo, Nyerere alikuwa mgeni kabisa kwa wote aliokuwa akiwaomba kura zao. Maisha ya Nyerere katika siasa yalianza hapo. Nyerere alikuwa mgeni na alikuwa hana historia ya kuongoza mapambano ya umma dhidi ya serikali ya kikoloni.
Ukoo wa Sykes ulikuwa unatambulikana katika siasa za Dar es Salaam kwa takriban robo karne. Ukoo huu ndiyo ulioanzisha na kuongoza vyama vyote viwili, African Association na Al Jamiatul Islamiyya. Ukoo wa Sykes ulikuwa unafahamika kwa kuongoza mapambano dhidi ya serikali. Ushahidi wa haya unapatikana katika nyaraka kati ya ukoo huu na serikali ya kikoloni.
Katika kipindi cha miaka zaidi ya ishirini, serikali kwa nyakati tofauti, kati ya mwaka 1929 hadi 1953 ilikuwa na barua za Kleist Sykes na za mwanaye Abdulwahid wakiwa viongozi wa African Association kuhusu madhila tofauti yaliyokuwa yakiwakabili wananchi.

Uchaguzi ulikuwa kwa kunyoosha mikono. Denis Phombeah aliyekuwa akifanya kazi pale  Arnatouglo ndiye alikuwa msimamizi wa uchaguzi. Phombeah aliwaomba Abdulwahid na Nyerere kutoka nje ya ukumbi ili uchaguzi uanze. Wiki nzima kabla ya uchaguzi Phombeah alikuwa akizunguuka mji mzima na pikipiki yake akimfanyia kampeni Nyerere. Lakini kwa hakika hakukuwa na haja ya kufanya hivyo.
Uongozi wa ndani wa TAA wa Abdulwahid, Ally, Dossa Aziz na Rupia ulikuwa tayari umekwishaamua kumpa Nyerere urais wa chama. Inawezekana labda kwa kuwa Phombeah hakuwa katika wandani wa TAA yeye hakujua uamuzi uliokuwa umepitika. Kwa hakika uchaguzi huu ulikuwa kutimiza utaratibu tu, mambo yote yalikuwa yamepangwa na yakapangika