Jumamosi, 25 Februari 2012

ETI TV ZA VICHOGO MWISHO KUTUMIKA 2013!!!?




NewsImages/6277570.jpg
Luninga lenye tumbo au wengine wanaita chogo
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa ametangaza kuwa Luninga - televisheni za teknolojia ya analojia zenye `michogo au matumbo’ hazitafanya kazi kuanzia Januari Mosi, 2013 au ziunganishwe na ving’amuzi vitakavyonunuliw
Hatua hiyo imekuja baada ya Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa kutangaza kusitishwa kwa matangazo ya Televisheni kwa kutumia analojia kwenda digitali kuanzia Januari Mosi 2013. Bei ya ving’amuzi katika kampuni mbalimbali zinaanzia Sh70,000.


Wakati huo huo, kuna baadhi ya luninga za digitali ambazo ving’amuzi vimejengewa ndani hizo zitatumika kama kawaida. Wananchi wanapaswa kujiandaa mapema hasa kununua ving’amuzi kwa luninga ambazo zinatumia teknolojia ya analojia.


Wataalam wanasema faida ya digitali ni kuongezeka kwa ubora wa picha, matangazo na ongezeko la vituo vya televisheni. Pia kuingia kwa teknolojia ya digitali katika matangazo ya televishenikunapelekea kupatikana kwa wingi zaidi katika vyombo vya mawasiliano kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa intaneti

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni