Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akitoka katika Mahakama ya Hakim Mkazi Kisutu Dar es Salaam, baada ya kutoa ushahidi wake katika kesi ya uhujumu uchumi wa zaidi ya euro milioni 2, sawa na sh bilioni 3 inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, na Grace Martin. Pia Mh. Kikwete anatakiwa nae awepo Mahakamani kutoa ushahidi, Katiba itamruhusu kuingia Mahakamani akiwa madarakani au watamsubiri amalize mda wake wa kuwa madarakani!!!?
KARIBU KATIKA BLOGU HII YA KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUONYA KUPITIA MADA MBALIMBALI NA HATA PICHA. ONGEZA MAHUSIANO KWA KUJUMUIKA NA WENZIO HAPA.UNAWEZA TUMA PICHA NA MAELEZO KWA ANUANI HII;mkuu74@gmail.com
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo SHERIA. Onyesha machapisho yote

Jumatatu, 7 Mei 2012
Alhamisi, 3 Mei 2012
HAKIMU AMTAKA WAKILI WA CHADEMA ALIPE GHARAMA ZA MASHAHIDI.
HAKIMU wa Makahama ya Hakimu Mkazi Arusha, Charles Magesa amemwamuru wakili wa utetezi katika kesi inayowakabili viongozi wa Chadema na wafuasi wao 19, kulipa gharama za usumbufu wa mashahidi wawili na mawakili wa serikali watatu ambao walifika kwa ajili ya kesi hiyo kuanza kusikilizwa.
Hakimu, Magesa alitoa amri hiyo baada ya Wakili Method Kimomogolo kutofika mahakamani hapo bila kutoa sababu za msingi na badala yake kumtuma Wakili Albart Msando kumwakilisha.
Msando alidai wakili huyo hakuweza kufika mahakamani hapo kwa sababu anakabiliwa na kesi mbili Mahakama ya Rufaa mkoani Arusha ambazo mojawapo ni kesi ya kuvuliwa Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema na ya wanakijiji wa Soitsambu na TBL siku ya Ijumaa.
Amri hiyo ilitolewa na Magesa kutokana na Wakili Msando kusimama na kudai kuwa mshtakiwa Dk. Willibrod Slaa pamoja na mchumba wake, Josephine Mshumbusi wamefiwa na mtu wao wa karibu.
Aliongeza kuwa wakili Kimomogolo hakufika mahakamani hapo kutokana na kuandaa rufaa mbili ambazo anatakiwa kuziwasilisha siku ya Ijumaa ya wiki hii .
Alisema kutokana na wakili kushindwa kufika mahakamani hapo pamoja na Slaa na Josephine aliomba Mahakama hiyo kuahirisha usikilizwaji wa kesi hiyo pia kwa sababu washtakiwa wote wana haki ya kuwakilishwa na mawakili wote wawili ambao ni Msando na Kimomogolo.
Alisema mawakili wa Serikali ambao ni Mwahija Ahmed, Awamu Mbwangwa na Edwin Kakolaki pamoja na mashahidi wao kama wanaona kuahirishwa kwa kesi hiyo kunahitaji gharama waseme ili warudishiwe.
Wakili wa Serikali aliiomba Mahakama itoe amri wakili Kimomogolo alipe gharama walizotumia kwa ajili ya kujiandaa na usikilizwaji wa kesi hiyo pamoja na mashahidi wao wawili.
Hakimu Magesa alikubaliana na hoja ya Wakili wa Serikali ya kuamuru gharama za mawakili wa Serikali pamoja na mashahidi kwa kesi hiyo ambao walikuja jana zilipwe. Kesi iliahirishwa hadi Juni 5 mwaka huu

Ijumaa, 2 Machi 2012
'ASKOFU' AKAMATWA KWA RUSHWA ARUSHA
Thomas Mollel almaarufu Askofu.
WAKATI mwanachama wa CCM, Siyoi Sumari, akitangazwa mshindi katika mzunguko wa pili wa kura ya maoni Arumeru Mashariki, mfanyabiashara maarufu mkoani hapa anayechimba, kuuza na kununua madini aina ya tanzanite, Thomas Mollel ‘Askofu’ amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwa tuhuma za kutoa rushwa kwa madiwani. Askofu huyo ambaye pia ni Diwani wa Mbuguni, Arumeru, alikamatwa usiku wa manane wa kuamkia jana kwa tuhuma hizo zinazohusiana na kura ya maoni ambayo ilipigwa jana na kumpa Siyoi ushindi wa kura 761 dhidi ya William Sarakikya ambaye alipata kura 361.
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, iliagiza kurudiwa kwa kura ya maoni ikihusisha wagombea hao baada yao na wengine waliojitokeza kutofikisha zaidi ya nusu ya kura za wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Katika kura hizo, Siyoi aliongoza kwa kupata kura 361 akifuatiwa na Sarakikya aliyepata kura 259. Kamati Kuu ilifanya uamuzi huo ili kupata mgombea ambaye atapata asilimia 50 au zaidi ya hapo.
Matokeo ya jana yalitangazwa na Msimamizi, Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa. Wajumbe waliopiga kura walikuwa 1,124 ambapo kura mbili ziliharibika.
Askofu akamatwa Kuhusu Askofu kukamatwa, ilidaiwa kwamba alikutwa kikaoni akishawishi madiwani kwa rushwa ili wampigie kura ya maoni Siyoi, ili apate ridhaa ya CCM kugombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki.
Kamanda wa Takukuru wa Mkoa wa Arusha, Mbengwa Kasomambuto, alidai kwamba hadi jana walishamkamata Askofu na watuhumiwa wengine wawili.
Kasomambuto alidai kuwapo mtandao wa kutoa rushwa na kwamba Askofu alikabidhiwa kazi ya kushawishi kundi la madiwani hao na juzi juzi kukutana na baadhi yao kwenye kikao ambacho hakikuwa rasmi wala halali.
Aliwataja wengine waliokamatwa, kuwa ni Elirehema Kaaya ambaye awali aligombea katika mzunguko wa kwanza wa kura hiyo lakini alishindwa kwa kupata kura 205.
Ilidaiwa kuwa naye alihusika kushawishi waliompigia kura awali, ili wampigie Siyoi katika uchaguzi wa marudio uliofanyika jana. Mwingine ni Ezekiel Mollel, ambaye ni Katibu wa Jumuiya ya Vijana ya CCM Wilaya ya Monduli.
“Wote watatu tunawashikilia na wako kwa uchunguzi zaidi na ukikamilika wote watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka ya rushwa,” alisema Kamanda huyo.
Aliongeza kuwa Elirehema ni Katibu Mwenezi wa CCM Nyamagana ambaye alishika nafasi ya tatu katika uchaguzi huo. Alidai kwamba mtuhumiwa huyo baada ya kuhojiwa, alikutwa na tuhuma za kupewa jukumu la kushawishi kwa rushwa wajumbe waliompigia kura katika uchaguzi wa awali wapatao 205 ili wahamishie kura zao kwa Siyoi.
Jumapili, 19 Februari 2012
JAJI MKUU AASA MAHAKIMU WAACHE TABIA YA KUHAIRISHA KESI
MAHAKIMU nchini wametakiwa kuacha utamaduni wa kuahirisha kesi bila sababu za msingi hali inayoleta manung'uniko kati ya mshitakiwa na mdai haki.
Aidha mawakili na wanasheria nao wameaswa kuacha tabia ya kujali maslahi kwa wateja wao
bali waangalie jinsi ya kuwasaidia kupata haki badala ya kuwatetea huku wakijua
wateja wao hawatafanikiwa.
Hayo yalisemwa jana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande wakati alipokuwa
akifungua mkutano wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unaofanyika mkoani
Arusha kwa siku mbili.
Alisema kwenye Mahakama kuna utamaduni kwa baadhi ya Mahakimu kuahirisha kesi bila
sababu za msingi na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo kunaleta malalamiko kati ya
mtuhumiwa na aliyefungua kesi hali inayopelekea wananchi kukosa imani na Mahakama.
Pia alisema si busara kwa mawakili ambao ni maofisa wa Mahakama kujali fedha kwa
wateja wao huku wakijua haki itatendeka na kuwaasa kuacha tamaa za fedha badala
yake watoe huduma kwa wananchi ambao wanahitaji msaada wa kisheria pasipo kuwa na
fedha.
"Acheni tabia ya kutaka fedha huku mkijua wateja wenu hawatafanikiwa katika kesi
inayowakabili pia na Mahakimu acheni tabia ya kuahirisha kesi bila ya kuwa na sababu
za msingi."
Aliongeza kuwa baadhi ya wananchi hawana uwezo wa kawaida kupata mawakili wa
kuwatetea kutokana na fedha lakini kisheria inatakiwa mawakili kujitolea kuwasaidia
washitakiwa kwenye kesi zao, hivyo wawe na moyo wa huruma na si kuangalia maslahi
yao binafsi.
Naye Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Francis Stola aliiomba Serikali
kutenga fedha kwa wakati za mashauri ya kesi za uchaguzi na yale ya dharura ili kesi
hizo ziweze kuamuliwa kwa wakati badala ya kupoteza muda.
Pia alisema wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa maktaba, vitabu vya sheria
pamoja na tatizo la rushwa kwa baadhi ya wanasheria ambao wanatia doa taaluma hiyo
na kusisitiza kuwa taaluma hiyo ni muhimu katika kusaidia jamii mbalimbali

Ijumaa, 3 Februari 2012
SIKU YA SHERIA TANZANIA YAADHIMISHWA MAHAKAMA YA WILAYA NACHINGWEA LEO KWA MAHAKAMA YA WAZI.
Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Nachingwea akimsomea mashtaka mtuhumiwa ajulikanae ka ma Tuju wa Matangini Nachingwea ya kosa la kupatikana napombe haramu ya Gongo nusu lita leo asubuhi katika siku ya kuadhimisha mwanzo wa kalenda ya Mahakama Tanzania.
Tuju akiwa kizimbani. Ujunbe a siku ya sheria leo ni 'adhabu mbadala'
Jumatano, 30 Novemba 2011
JERRY MURO NA WENZAKE HAWANA HATIA, WAACHWA HURU NA MAHAKAMA YA KISUTU LEO.
![]() |
Jerry Muro kushoto akiwa na watuhumiwa wenzie Mgasa katikati na Kapama kulia, leo wameachiwa huru na Mahakama baada ya takribani miaka miwili ya kesi yao. |
Jumatano, 9 Novemba 2011
DK SLAA ASHITAKIWA KWA KUTOA MANENO YA UCHOCHEZI KUWA WATAANDAMANA KUMTOA RAIS KIKWETE MADARAKANI.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa, akishuka kutoka kwenye Karandinga la Polisi, kusomewa mashitaka yanayomkabili na washitakiwa wengine 26 waliofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume na sheria. Picha na Filbert Rweyemamu.
Mahakamani
Dk Slaa, Lissu na wafuasi wengine 25 wa Chadema walifikishwa mahakamani jana kujibu mashtaka matatu tofauti likiwamo la uchochezi ambalo linamkabili Dk Slaa pekee.
Viongozi hao wa Chadema na wafuasi wao, walifikishwa mahakamani wakiwa chini ya ulinzi mkali wa maofisa wa polisi majira ya saa nane mchana na kesi hiyo ilianza kutajwa mahakamani saa 9:00 alasiri.
Wakili wa Serikali, Haruna Matagane alisema watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa makosa mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali usiku wa Novemba 7, mwaka huu na saa 12 asubuhi Novemba 8, mwaka huu licha ya kutakiwa kutawanyika na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Peter Mvulla.
Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Devota Kamuzora, mwendesha mashtaka huyo alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walikaidi amri halali ya SSP Mvulla kinyume cha sheria walipotakiwa kutawanyika.
Alisema Dk Slaa anashitakiwa kwa kosa moja pekee la kutoa maneno ya uchochezi kinyume na sheria mnamo Novemba 7, mwaka huu saa 11:30 jioni.
“Tunatoa muda ifikapo saa kumi na moja jioni wanataka kumpeleka kwa ndege Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Zuberi Mwombeji kwa IGP Said Mwema ili wampangie wilaya nyingine ya kuhamia,” Matagane alisema akinukuu kauli inayodaiwa kutolewa na Dk Slaa.
Wakili huyo wa Serikali alisema Dk Slaa pia anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kutaka Lema atolewe Kisongo ifikapo saa kumi jioni la sivyo kutakuwa na maandamano ya kumtoa Rais Jakaya Kikwete madarakani.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Mawakili wa utetezi, Method Kimomogoro na Arbert Msando waliomba watuhumiwa hao wapatiwe dhamana kwa kuwa yanaruhusu kufanya hivyo ombi ambalo lilikubaliwa na Hakimu Kamuzora akiwataka washtakiwa wote kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja kuweka ahadi ya kiasi cha Sh5 milioni.Watuhumiwa 20 wakiwamo viongozi walipata dhamana na kesi yao imeahirishwa hadi Novemba 22, mwaka huu.
Ijumaa, 7 Oktoba 2011
Alhamisi, 22 Septemba 2011
ANTI-CORRUPTION WEBSITE IS DUE ONLINE, HONGERA FREDRICK FUSSI NA WENZIO.
Kijana mwanzilishi wa mtandao huo, Fredrick Fussi.
Unaweza kuripoti vitendo vya rushwa kupitia / report corruption via: ripotirushwa.or.tz
----
Corruption in the health sector in Tanzania has been a stumbling block upon accessing services, something that has culminated loss of lives, especially people with meager income.
In a move towards finding the lasting solution on the vice which has been increasing at alarming rate, Tanzania Youth Vision Association (TYVA) launched anti-graft awareness community campaign in September10, this year in all secondary schools of Dar es Salaam region, aimed at creating awareness and sensitization.
The campaign, sponsored by the World Bank (WB) through the British Council, is part of Anti Corruption Journalism for Health (ACJH) project which kicked off in the mid of August this year, to fight and combat corruption in the health sector.
The campaign is colored by various testimonies from different students who adduced before the public the scenarios in which they were forced by officials from the health sector to give bribes in exchange of the service. It was held at Azania Secondary School in Dar es Salaam.
“I once bribed a doctor when I was undergoing medical examination to fill in the form for joining Azania Secondary school so that I could ease the exercise when I realized that it was very hard to be examined without bribing the doctor on duty’’, said Mbwana Msangula.
Msangula says that a doctor at Amana hospital in Ilala district solicited 3,000/- from him. He had no other alternative than to give him, simply because he was in a great need to proceed with his studies.
According to ACJH Project Manager Mr Fredrick Fussi this campaign dubbed ‘Ripoti Rushwa Community Campaign’’ started with secondary schools in Dar es Salaam and Cost regions, after which it would involve the community at large in both regions

source: http://www.wavuti.com/
WAKILI FELIX MKONGWA KIZIMBANI KWA KUGHUSHI
Wakili wa kujitegemea Felix Mkongwa amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashitaka ya kughushi na kujipatia kiwanja kwa njia za udanganyifu.
Wakili wa Serikali Leonard Shayo alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi Rita Tarimo kwamba Mkongwa alitenda makosa hayo Juni 3, 2005 jijini Dar es Salaam.
Katika shitaka la kwanza, anadaiwa kuwa alighushi mkataba wa kuuziana kiwanja namba 600 block G Tegeta jijini Dar es Salaam ikionesha kwamba imesainiwa na mmiliki halali George Kimwaga akijua sio kweli.
Mkongwa anadaiwa katika shitaka la pili kwamba alijipatia mali kwa njia za udanganyifu na kwamba tarehe hiyo alijipatia kiwanja hicho akionesha kwamba ameuziwa na Kimwaga.
Wakili Mkongwa amekana mashitaka hayo na yuko nje kwa dhamana baada ya kukamilisha masharti ya dhamana yaliyomtaka kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na kusaini hati ya dhamana ya Shilingi milioni 10. Kesi hiyo itatajwa Oktoba 24 mwaka huu.

Jumatano, 21 Septemba 2011
WANAZUONI WAKIISLAMU WALAANI KITENDO CHA DC IGUNGA KUVULIWA HIJAB
WANAZUONI wa Kiislamu nchini wameipa siku tatu Chadema Taifa kulaani kitendo cha wafuasi na viongozi wake kulidhalilisha vazi tukufu la hijab na kumwomba radhi Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Fatuma Kimario, kwa kumvua sitara yake.
Wamesema iwapo chama hicho kitapuuza kufanya hivyo na kupita muda huo wanazuoni hao na Waislamu wataiona Chadema kama chama chenye sera na madhumuni ya kuhujumu Uislamu na Waislamu wa Tanzania na kuhimiza Waislamu kukiepuka kama ukoma.
Kauli hiyo iko kwenye tamko la Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania (HAY-AT) lililosomwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Sekretarieti Kuu ya Umoja huo, Shehe Sherali Hussein Sherali na kusema siku tatu hizo zilianza jana.
Wanazuoni hao zaidi ya 10 wakiongozwa na Mwenyekiti wao, Shehe Suleimani Kilemile, walitoa tamko hilo mbele ya waandishi wa habari na kusema baada ya hapo umoja huo utakaa na kutafakari hatua stahiki za kukabiliana na dharau hizo na kuelekeza Waislamu cha kufanya.
Sherali alisema ifahamike, kwamba shambulio lolote dhidi ya hijab ni dhidi ya Uislamu na Waislamu wote, haliwezi kuvumilika na watakabiliana na yeyote anayetaka kuidhalilisha amri ya hijab iliyo katika Quran sura ya 33:59.
“Tunataka ifahamike, kwamba yeyote atakayelidharau vazi la hijab kwa kauli au vitendo, atakuwa amewachokoza Waislamu na sisi kamwe hatukubali hilo liendelee na kukaa kimya, tutachukua hatua stahiki na ikibidi tutalazimika kuondoa munkari kwa mikono yetu wenyewe, kama dini yetu inavyotuelekeza,” alisema.
Aliongeza kuwa wanalaani na kupinga kitendo kilichofanywa na wanaodaiwa kuwa wafuasi na viongozi wa Chadema kumvua nguo Mkuu huyo wa Wilaya na kumwacha bila sitara.
Alisema Kimario ni Mwislamu anayefuata mafundisho ya Uislamu yanayomtaka kila
mwanamke ajisitiri kwa vazi la hijab, hivyo kumvua ni kumdhalilisha kwa wanajamii kama mwanamke wa Kiislamu, mama mwenye watoto na kiongozi wa Serikali.
Tumetafakari tukio hili kwa undani na tunalichukulia kama shambulio la wazi na la makusudi dhidi ya mafundisho yetu na dini ya Kiislamu, yanayomtaka kila mwanamke aliyevunja ungo, kujisitiri kwa kuvaa vazi la hijab,” alisema Sherali.
Aliwaomba Watanzania wote, wanaharakati wa asasi za kijamii na wa haki za binadamu, viongozi wa vyama vya siasa na wa dini zote, kulaani na kupinga unyanyasaji huo wa kijinsia na kidini unaokwenda kinyume na Katiba ya nchi na utamaduni wa Watanzania wa kuheshimiana.
“Tumesikitishwa na ukimya wa asasi za kijamii zinazodai kutetea haki za binadamu na za wanawake, kutolaani kitendo hiki cha mwenzao kudhalilishwa kijinsia, kuendelea kukaa kimya kunatulazimisha kuwaona wanafiki na ndumilakuwili juu ya madai yao ya kutetea wanawake,” alisisitiza.
Alisema wanaitaka Serikali ilitafakari kwa kina tukio hili la kudhalilishwa mwanamke Mwislamu, akilitumikia Taifa kama mmoja wa viongozi wake, kukaa kimya kutatoa tafsiri hasi juu ya jinsi inavyolichukulia tukio hilo na kuitaka kuwachukulia hatua kali wahusika.
Wanawake Waislamu Katika hatua nyingine, kikao cha wanawake Waislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee Jumapili, wanawake walilaani tukio hilo.
Kikao hicho chini ya Mwenyekiti wake Fatma Juma, kiliwataka wanawake na wapenda amani wote kulaani kitendo hicho cha udhalilishaji wanawake.
Walisema kitendo hicho kimeonesha dharau, si tu kwa Uislamu, bali hata kwa madhehebu mengine na kinaweza kuvuruga amani na utulivu uliopo nchini hivi sasa.
Tamko la kikao hicho, lilisema litaanza kusambazwa katika misikiti yote Ijumaa, ili Waislamu waelewe namna walivyoguswa na kusononeshwa na tukio hilo.
Shura ya Maimamu
Habari zaidi zilizopatikana zilisema Shura ya Maimamu nayo itakutana hivi karibuni kujadili tukio hilo la mwanamke wa Kiislamu kuvuliwa hijab.
Mbali ya kukutana huko, Shura hiyo itaandaa maandamano ya kupinga kitendo hicho ambacho wamekitafsiri kuwa ni matusi dhidi ya Uislamu.
Katibu wa Shura ya Maimam, Shehe Ponda Issa Ponda, jana alithibitisha kuwapo kwa ajenda hiyo.
Akizungumza na gazeti hili jana alisema kitendo kilichofanywa na wafuasi wa Chadema kimekosa utu, ustaarabu, uungwana na maadili mema na kinapaswa kukemewa na wapenda amani wote nchini, bila kujali itikadi zao, kwani kikiachwa kitazidi kukomaa na kuonekana ni
jambo la kawaida katika jamii.
Akizungumzia kadhia hiyo, Katibu wa Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini (Baraza Kuu), Shehe Ramadhan Sanze, naye alisema taasisi yake inaungana na wanaolaani tukio hilo .
“Mtazame DC Fatuma namna alivyokuwa akivutwa, akivuliwa nguo na akitukanwa na vijana wale wa Chadema ambao baadhi yao ni sawa na watoto wake wa kuzaa, hakika inatia uchungu,” alisema Shehe Sanze kwa masikitiko na kuongeza kuwa wanawake kote nchini wamedhalilishwa kwa uhuni ule.
Nao baadhi ya Waislamu ndani ya Chadema wameeleza kukasirishwa na kitendo hicho cha wenzao kumvua kwa nguvu hijab Mkuu wa Wilaya.
Waislamu hao ambao hawakutaka kutajwa majina, walisema watakutana hivi karibuni kujadiliana juu ya hatua za kuchukua kutokana na tukio hilo la kudhalilisha dini yao.
Kwa karibu wiki nzima baada ya tukio hilo la Igunga watu mbalimbali wametuma salamu zao za kulaani tukio hilo kupitia Radio Imani ya Morogoro na Radio Kheri na Radio Quran.
Viongozi watatu wa Chadema wakiwamo wabunge wawili wamefikishwa mahakamani Tabora, wakikabiliwa na mashitaka manne ya wizi wa simu, shambulio, matusi ya nguoni na utekaji
nyara. Kesi yao iliahirishwa juzi hadi Oktoba 10.
Chadema wang’aka
Akizungumzia tuhuma hizo jana, Mwanasheria wa Chama cha Chadema Tundu Lissu alisema hawajapata taarifa ya suala hilo na kuwataka wanazuoni hao kufahamu kuwa Mkuu wa Wilaya hakuvuliwa hijab na wala hakudhalilishwa kama inavyodaiwa.
Alisema ushahidi wa suala hilo unaonekana katika kesi waliyofunguliwa wanachama hao na hakuna tuhuma za kumdhalilisha kijinsia wala shambulio la aibu.
“Hatuna chochote cha kuomba msamaha kutokana na hali halisi ilivyokuwa, labda kama ingekuwa kweli alivaa hijab,” alisema Lissu.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa picha, Mkuu huyo wa Wilaya alikuwa amevaa mtandio, gauni linaloishia magotini na lenye mikono mifupi wakati hijab anavyoelewa yeye ni nguo inayofunika mwili mzima isipokuwa uso

MAHITA AKUBALI AMRI YA MAHAKAMA
Bw. Omari Mahita.
Hatimaye, aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Omar Mahita amekubali kutekeleza hukumu ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam kuhusu mtoto aliyekuwa akimkataa kwamba si wake, ambaye alizaa na mtumishi wake wa ndani, Rehema Shabani.
Jana Mahita alilipa gharama za malimbikizo ya matunzo ya kumhudumia mtoto huyo kuanzia mwaka 2003 hadi siku ya hukumu ilipotolewa Septemba mwaka juzi, ambapo alilipa Shilingi milioni 9 kupitia kwa wakili wake, Charles Semgalawe kwa kampuni ya udalali ya Nasm Auction Mart ambayo ilipewa jukumu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kufuatilia fedha hizo, na kuahidi kulipa Shilingi milioni 3 zilizobaki baada ya siku 30 kuanzia jana.
Mahakama hiyo pia ilimtaka Mahita kulipa Sh 100,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto huyo baada ya kulipa Sh milioni 12 hizo.
Uamuzi wa Mahakama ulitokana na Mahita kugoma na hivyo mama wa mtoto kurudi mahakamani na kutoa taarifa. Mtoto wao, Juma Mahita kwa sasa anasoma kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari ya Hananasif Kinondoni.
Kampuni ya Nasm Auction Mart ilitoa notisi ya siku 14 kwa Mahita awe amelipa fedha hizo, vinginevyo hatua ya kutumia nguvu kukamata mali zake ingetumika. Notisi hiyo ilikuwa inamalizika jana na kwa kuwa sehemu ya fedha hizo ilitolewa na kuhidi kumaliza kiasi kilichobakia ndani ya siku 30, hatua ya kutumia nguvu iliondolewa.
Katika kesi hiyo, Mahakama ya Kinondoni ilijiridhisha kuwa mtoto huyo ni wa Mahita kutokana na ushahidi wa upande wa mlalamikaji uliowasilishwa mahakamani hapo, ukiwapo wa vipimo vya vinasaba (DNA).
Hata hivyo, Mahita alikata rufaa kupinga hukumu hiyo, rufaa ambayo nayo ilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu.
Katika uamuzi wa rufaa hiyo, Jaji Dk. Fauz Twaib wa Mahakama Kuu, aliunga mkono hoja za wakili wa mlalamikaji kuwa ingawa sheria inatamka fidia ya Shilingi 100/- lakini mahakama inaweza kuangalia hali ya maisha na uwezo wa mlalamikiwa na hivyo kuweza kuongeza kiwango hicho. Alisisitiza kuwa katika shauri husika, kiwango kilichoamuriwa na Mahakama ya chini kilizingatia hali ya kiuchumi hususan gharama za maisha na uwezo wa mrufani kuweza kulipa na kwa mujibu wa barua kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwenda kwa Mahakama, mrufani hakuweza kufika kwa ajili ya uchunguzi mara sita kwa nyakati tofauti.
Jaji Twaib akasema Mahakama ya Kinondoni ilikuwa sahihi na hivyo kumtaka Mahita kulipa pia gharama za kesi hiyo

Mtoto Juma na mama yake.

WAKOREA WAPATIKANA NA HATIA YA KUTOA RUSHWA.
Boss wa Takukuru, Bw. Edward Hosea.
Raia wawili wa Korea waliokuwa wakikabiliwa na makosa ya kutoa rushwa, wamehukumiwa kwenda jela miaka mitano kila mmoja baada ya kukiri kosa mahakamani.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Dodoma iliwafikisha mahakamani raia wawili wa Korea kwa kosa la kutoa hongo ya Shilingi 100,000 kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Waliofikishwa mahakani ni Yun Yong Sim na Kim Song Hul ambao wanakabiliwa na kosa la kutoa rushwa kwa ajili ya kumshawishi Mganga Mkuu, Godfrey Mtey ili aweze kuwapa kibali cha Zahanati yao ambayo ilifungiwa kutokana na kutokukidhi vigezo.
Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma, Hassan Momba, aliwahukumu washtakiwa kwa kosa la kutoa rushwa ya Shilingi 100,000 kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Kaimu Kamanda wa TAKUKURU mkoani Dodoma, Sostenes Kibwengu alisema kuwa raia hao waliwekewa mtego baada ya kupokea taarifa za jambo hilo ambapo walifanikiwa kuwatia mbaroni na kuwafungulia mashtaka ya kutoa rushwa mahakamani.
Kibwengu alisema kikosi chake chini ya Kamanda wa Mkoa, Eunice Mmari kilianza kutilia shaka nyendo za raia hao baada ya kupewa taarifa za siri na raia wema na viongozi wenyewe waliotaka kuhongwa.
Walifungiwa kutoa huduma katika Zahanati yao ambayo ipo eneo la Area C’ Manispaa ya Dodoma baada ya Wizara ya Afyana Ustawi wa Jamii kubaini ilikuwa imejengwa na kutoa huduma chini ya kiwango, “Walifungiwa ili warekebishe baadhi ya mambo yakiwamo mazingira pamoja na kuzuiwa kuuza dawa za asili ambazo hazikuwa na vibali ndipo walipoanza kuhaha kwa ajili ya kuweka mambo sawa kwa wakubwa,’’alisema mmoja wa watu wanaoishi karibu na eneo hilo.
Taarifa zinaonyesha kuwa mbali na kufungiwa kituo hicho, lakini raia hao walikamatwa na kuwekwa korokoroni ingawa siku mbili baadaye walionekana mitaani wakitafuta namna ya kunusuru biashara yao.
Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Uhamiaji Mkoa wa Dodoma, raia hao hata vibali vyao si halali na kwamba wanaishi kwa kutumia ujanja ujanja kutoka kwa baadhi ya watu, “Ni kweli ningekuambia kikamilifu lakini msemaji hayupo hapa isipokuwa hata mimi naweza kusema uhalali wa wao kuishi hapa nchini ni wa mashaka mashaka lakini usinitaje,’’alisema mmoja wa wafanyakazi wa Uhamiaji.
Momba alisema ametoa hukumu hiyo mapema, kutokana na washtakiwa hao kutosumbua mahakama, baada ya kukiri kutenda kosa hilo, “Mahakama imeridhika pasipo na shaka yoyote, baada ya watuhumiwa wenyewe kukiri kosa lao, kuwa walikuwa wametenda kosa hilo, hivyo watatumikia kifungo cha miaka mitano kila mmoja gerezani au watatakiwa kulipa faini ya Shilingi 500,000 kwa kila mmoja, kwa maana hiyo wote wawili watatakiwa kulipa ni Shilingi 1 milioni,’’ alisema Momba.
Hata hivyo, watuhumiwa hao kwa pamoja walilipa faini na kukwepa kwenda gerezani.
Hukumu ya watumiwa hao imekuja ikiwa ni siku moja tangu TAKUKURU waliposhinda kesi dhidi ya Ofisi Utamaduni wa zamani Manispaa ya Dodoma, Stansalaus Kobelo, baada ya kutiwa hatiani kwa kosa kama hilo. Kobelo alihukumiwa juzi na mahakama hiyo kwa kosa la kutaka rushwa kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wa Sekondari ya Jamhuri, ili kumsaidia mambo yake. Alilipa faini ya Shilingi 500,000/=
Jumatano, 14 Septemba 2011
MWENYEKITI SERIKALI YA MTAA KORTINI KWA RUSHWA YA LAKI MOJA.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Iringa, imemfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Ilula-Mtua, William Ngandago (75), kwa tuhuma za kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 100,000.
Ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Restituta Kessy, aliyekuwa akisaidiana na Philemon Msegu kuwa William alikamatwa Julai 27, mwaka huu katika Kijiji cha Ilula-Mtua, baada ya kudaiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 100,000.
Mwenyekiti huyo anadaiwa kuomba na kupokea rushwa hiyo kutoka kwa Patrick Mtanga kama kishawishi ili aweze kumsaidia kumwekea dhamana ndugu yake, James Ndala, ambaye alikamatwa na Mwenyekiti huyo na kuwekwa katika mahabusu ya Polisi kituo cha Ilula.
Kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo jana kwa mara ya kwanza mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Iringa, Dainess Lyimo.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Bi. Restituta Kessy.
Ilidaiwa na Mwendesha Mashitaka wa Takukuru Mkoa wa Iringa, Restituta Kessy, aliyekuwa akisaidiana na Philemon Msegu kuwa William alikamatwa Julai 27, mwaka huu katika Kijiji cha Ilula-Mtua, baada ya kudaiwa kuomba na kupokea rushwa ya Sh. 100,000.
Baada ya upande wa mashitaka kutoa maelezo hayo, Hakimu Lyimo aliahirisha kesi hiyo na kuamuru mtuhumiwa kurejeshwa mahabusu hadi hapo kesi hiyo itakapotajwa tena Septemba 27, mwaka huu.
CHANZO: NIPASHE
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)