Jumamosi, 17 Agosti 2013

VODACOM WASEMA KATIZO LA MAWASILIANO JANA LILITOKANA NA KUUNGUA VIFAA KATIKA MTAMBO WAO MKUU.


TAARIFA KUTOKA VODACOM KUHUSU TATIZO LA MTANDAO

Moto uliozuka leo katika mitambo ya kuendesha mtandao (switch) wa Vodacom umezimzwa jioni hii.

Akizungumza jioni hii Afisa Mkuu wa Mawasiliano wa Vodacom, Georgia Mutagahywa alisema moto huo ulipelekea kusimama kwa huduma zote za kampuni hiyo.

"Tunawaomba radhi wateja wetu wote kutokana na usumbufu wa kukosa mawasiliano uliosababishwa na kuungua kwa vifaa muhimu vya kuendesha mitambo yetu. Ninapenda kuwahakikishia kwamba wataalam wetu wanafanya kila jitihada kurudisha mawasiliano ya mtandao wa Vodacom haraka iwezekanavyo,"

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni