Ijumaa, 2 Agosti 2013

MJUE MNYAMA KIBOKO; ANA UWEZO WA KULALA USINGIZI AKIWA MAJINI.

    
Kiboko ni mwanyama ambae ana uwezo wa kuuchapa usingizi huku mwili wake wote ukiwa umeza kabisa ndani ya maji. Sehemu kubwa ya maisha ya kiboko huwa ni ndani ya maji. Kiboko huwa anakuja nchi kavu usiku baada ya jua kuzama. Hufanya hivi kwa sababu nyingi. Mwili wa kiboko ni mkubwa na uzito wake pia ni mkubwa ukilinganisha na ukubwa wa mwili wake. Kwa kuwa kwenye maji muda mwingi, kunaipunguzia miguu ya kiboko kazi ya kuubeba uzito wa mwili wake.

Kuhusu muda wa kutoka ni kwamba Ngozi ya kiboko huwa inaitaji kuwa na unyevu unyevu muda wote. Endapo ataenda mbali na maji, uwezekano wa ngozi yake kunyauka na kumletea madhara ni mkubwa. Ndio maana hutoka nje ya maji baada ya jua kuzama. hapo huweza kwenda mbali hata kilomita nane mbali na bwawa kutafuta chakula. Kiboko hula Majani. Licha ya kwamba Kiboko ndio mnyama wa porini anaeongoza kwa kuuwa watu wengi barani afrika, mashambulizi mengi ya mnyama huyu huchukua sura ya kujihami zaidi na sio jaribio la kupata chakula. Kiboko sio mla nyama.

jambo moja la kustaajabisha kuhusu kiboko ni kwamba hajui kuogelea. Licha ya kwamba sehemu kubwa ya maisha yake huishi majini, kiboko hajui kuogelea na tena kiboko mkubwa hana uwezo wa kuelea. Kiboko hukaa ktk sehemu ze mto zenye maji ya kina kifupi ambako anakuwa 'anasimama' kwa miguu yake. Au zile sehemu ambazo kuna 'kisiwa' kilichotengenezwa kwa mchanga uliomwaga na maji katikati ya mto.
Kinachomsaidia kiboko ni uwezo wake mkubwa wa kubana pumzi, hali inayompa uwezo wa 'kukimbia' akiwa majini - chini kwa chini - na kwenda mbali. na anapohitaji kupumua, hujirusha (propel) kuelekea juu ambako ataibukua na kuvuta pumzi na kisha kurudi chini mara moja. Viboko watoto ndio wanauwezo wa kuelea na kuogelea. uzito wa mwili unavyoongezeka, ndivyo uwezo wa kuoelea unavyopotea.
Picha zote ni viboko wa Selous wakiwa ndani ya Mto Rufiji
Credits tembeatz blog

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni