Jumamosi, 17 Agosti 2013

PICHA YA LEO; WATAALAMU WANASEMA CHEKA UONGEZE SIKU ZA KUISHI, HEBU TUANGALIE PICHA YA HARUSI NA USAFIRI WA PIKIPIKI.

 Hivi ni namna ambavyo usafiri wa pikipiki unavyoweza kubeba watu wengi kushinda salon car mfano Mark II ambayo hubeba watu watano tu. Hii ni habari ya huko India jamaa hawataki mchezo wanaendelea na safari yao, Punda afe mzigo ufike.
Harusi inaendelea, Bw. Harusi mwenye suti nyeusi hana wasiwasi kapata mke na anamsafirisha katika toroli yeye mwenyewe ili kuonesha upendo wa dhati huku nyuma wakisindikizwa na wapambe wao ambao ni Mchungaji na mkewe kwenye baiskeli yao, haya ni mambo ya vichekesho toka Afrika ya Magharibi, Tchao.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni