Jumapili, 2 Oktoba 2011

MSEMAJI WA ILIYOKUWA SERIKARI YA LIBYA AKAMATWA.


NewsImages/5980658.jpg
Moussa Ibrahim
Msemaji maarufu wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi amekamatwa na waasi wakati akijaribu kuukimbia mji wa Sirte akiwa amevaa nguo za kike.
Msemaji wa Gaddafi, Moussa Ibrahim, ametiwa mikononi mwa wanajeshi wa serikali ya waasi baada ya kukamatwa akiwa amevaa nguo za kike ili asitambulike.

Imeripotiwa kuwa Ibrahim alikuwa akijaribu kutoroka mapambano makali yanayoendelea katika mji wa Sirte kati ya wanajeshi wa Gaddafi na wanajeshi walioipindua serikali yake.

Wanajeshi wengi wa Gaddafi wako kwenye mji wa Sirte ambao ndiko alikozaliwa Gaddafi. Mji huo umezungukwa pande zote na wanajeshi wanaipinga serikali ya Gaddafi.

Ibrahim alikamatwa ndani ya gari akiwa amevaa hijabu akijaribu kutoroka mji wa Sirte.

Ibrahim alijipatia umaarufu duniani kwa kuwa msemaji mkuu wa serikali ya Libya wakati waasi walipoanza kuandamana na kufanya mashambulizi ya kuipinga serikali ya kanali Gaddafi.

Alijulikana sana kwa mashirika ya habari ya kigeni ambapo alikuwa akivikusanya vyombo vya habari kwenye hoteli ya Rixos Hotel ya jijini Tripoli na kumwaga sera za kuiunga mkono serikali ya Gaddafi. Alikuwa akitoa taarifa za msimamo wa Gaddafi na kulaani mashambulizi ya NATO nchini Libya akisema kuwa NATO na nchi za magharibi haziitendei haki Libya.

Ilikuwa haijulikani Ibrahim amejificha wapi hadi jana alipokamatwa.

Hadi sasa mapambano yanaendelea kuiteka miji michache inayomuunga mkono Gaddafi.

Gaddafi mwenyewe hadi sasa hajulikani yuko wapi ingawa familia yake imekimbilia kwenye nchi za Algeria na Niger.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni