Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NIFAHAMISHE. Onyesha machapisho yote
Inaonyesha machapisho yaliyo na lebo NIFAHAMISHE. Onyesha machapisho yote

Jumatano, 1 Agosti 2012

TUNDU LISSU AMEWATAJA WABUNGE WALA RUSHWA HADHARANI, NI WA CHAMA TAWALA CCM.


Lissu awataja wabunge wala rushwa hadharani


NewsImages/6551346.jpg
MBUNGE WA SINGIDA Mashariki [Chadema], Tundu Lissu, jana alitaja majina ya wabunge saba wanaohusika na kashfa ya rushwa zinazohusisha Shirika la Umeme Tanzania [TANESCO].
Lissu alitaja majina hayo mbele ya vyombo vya habari katika mkutano wake aliouitisha na wanahabari mjini Dodoma

Katika kikao hicho mbunge huyo alithubutu kwa kujiamini kutaja majina hayo bila hata chembe ya uoga wabunge wote wanaohusika na rushwa kupitia shirika hilo

Aliwataja wabunge hao wa CCM ambao wengi ni wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini bungeni ambayo kamati hiyo tayari imeshavunjwa na Spika. Anne Makinda.

Alianza kwa kutaja Sara Msafiri [VitiMalum], Mariam Kisangi [Viti Maalum], Christopher Ole Sendeka [Simanjiro], Vicky Kamata [Viti Maalum] Bw. Yusuph Nassir [Korogwe Mjini], Bw. Charles Mwijage [Muleba Kaskazini] na Munde Tambwe [Viti Maalum] hao ni ambao kutoka Chama cha Mapinduzi [CCM].

Katika orodha yake hiyo Lissu aliwatetea wabunge wengine kutoka CHADEMA ambao wako katika kamati hiyo kutoka CHADEMA, ambao ni John Mnyika [Ubungo], David Silinde [Mbozi Magharibi] na Mwanamrisho Taratibu Abama [Viti Maalum] kuwa hawahusiki kabisa katika kashfa hiyo.

Katika taarifa yake hiyo alisema wabunge hao ndio chachu ya kuporomoka kwa Tanesco ambapo aliwataja mbunge Sara Msafiri na Munde Tambwe, wamekuwa wakipewa tenda ya kuiuzia matairi TANESCO

Alifafanua mbunge Yusuph Nassir na Mariam Kisangi kuwa wanamiliki vituo vya mafuta hivyo na ndio mana wamekuwa wakipokea rushwa kwa mgongano wa kimasilahi kutoka Wizara ya Nishati.

Alimuelezea Ole Sendeka kuwa, mbunge huyo amekuwa mtetezi namba moja kutetea Kampuni ya Orxy na Camel kwa kukosa tenda ya kuizuia mafuta IPTL kwa kudai ni vituo ambavyo vinafaa

Amesema wabunge hao wote kwa pamoja wamekuwa wakipata manufaa kutoka shirika hilo

Hivyo kupitia taarifa yake hiyo amemuomba Spika wa Bunge avunje kamati zote zinazotiliwa mashaka na utoaji wa rushwa

Leo asubuhi mbunge Ole Sendeka amemuomba Spika ampe muongozo kuhusiana na tuhuma alizopewa na Lissu kuwa athibitishe kauli zake alizozitoa kupitia vyombo vya habari kumchafua kw watanzania

Jumatatu, 2 Julai 2012

RAIS KIKWETE ATOA MSIMAMO KUHUSU MADAKTARI.


'Daktari Asiyeweza Kazi Aachie Ngazi ' - JK


NewsImages/6503146.jpg
Rais Jakaya Kikwete
RAIS Kikwete amesema serikali haina uwezo wa kulipa kiwango cha mshahara cha Sh.Mi.3.5 wanachokitaka kulipwa madaktari
Na kuwataka madaktari ambao hawataridhika na kiwango kilichowekwa waachie ngazi na wakatafute mwajiri atakayekuwa na uwezo wa kuwalipa kiasi hicho

Rais Kikwete aliyasema hayo pia katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kupitia vyombo vya habari

Rais Kikwete amesema, Serikali kwa sasa haiwezi kuwaahidi madaktari kima hicho kwani ikifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa ShMil. 7.7 kwa mwezi kitu ambacho hakiwezekani.

Mwisho alimalizia kwa kusema “nawasihi madaktari kuacha mgomo warejea kazini, kwani Watanzania wanateseka na kupoteza maisha kwa kukosa maatibabu”.

Wakati huohuo,Uongozi wa Taasisi ya Mifupa (MOI) umebandika tangazo linalosema na kuwataka madaktari wanaotaka kuendelea na kazi wakajisajili kwa Mkurugenzi wa Tiba

Tangazo hilo lilifanua kuwa madaktari watakaotaka kuendelea na kazi kujisajili ni mwisho leo

Jumapili, 17 Juni 2012

MWANAFUNZI MWENYE VIPAJI LUKUKI AGONGWA NA TRENI NA KUFARIKI HAPO HAPO JUMA LILOPITA.


Agongwa na Treni Akichati na Simu Kwenye Reli Dar


NewsImages/6470370.jpg
Jackson Thobias enzi ya uhai wake
Kijana Jackson Thobias mwenye umri wa miaka 17 amefariki dunia baada ya kugongwa na treni kwenye maeneo ya kipawa jijini Dar es Salaam. Aligongwa na treni baada ya kutembea juu ya reli huku akichati kwa simu yake na akisiliza muziki kwa kutumia headphone.
Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias, aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na Treni maeneo ya kwao kipawa.

Aligongwa na treni akiwa anatembea juu ya reli huku akiwa anasikiliza muziki kwa headphones huku pia akichati katika simu yake wakati akitembea kwenye reli.

Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.

Marehemu Jackson ndiye aliyeshinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School concert iliyoandaliwa na group ya Friends 4 Friends mei 12 mwaka huu.

Pia alishinda dougie competition wakati 5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.

Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17. Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani, Amen

Jumatano, 2 Mei 2012

JK AWAACHA WAFANYA KAZI NJIA PANDA MEI MOSI



Kikwete aacha njia panda wafanyakazi ongezeko la mishahara


NewsImages/6390358.jpg
Rais Jakaya Kikwete akishiriki kuimba wimbo wa wafanyakazi akiwa kashikana mikono na Rais wa Jumuiya ya Vyama vya wafanyakazi (TUCTA), Omary Ayub Juma[kusho, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa kw
Wednesday, May 02, 2012 11:42 AMRAIS Jakaya Kikwete amewaacha njia panda wafanyakazi nchini kuhusiana na suala zima la nyongeza ya mishahara ambapo katika hotuba yake ya Sikukuu ya Wafanyakazi hakubainisha wazi suala hilo
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), awali na kilo chao kikuu kwa serikali walitoa mapendekezo kima cha chini cha mishahara kifikie sh 315,000/=.

Madhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi [MEIMOSI] kitaifa yamefanyika katika Viwanja vya Mkwakwani, mkoani Tanga

Rais Jakaya Kikwete hakuweza wazi suala la ongezeko la mshahara “serikali inatambua mazingira magumu ya kazi waliyonayo wafanyakazi, hivyo serikali iko tayari kuyaboresha”.

Kikwete alisema serikali haitasubiri mpaka iwe na uwezo mkubwa kifedha, bali itaendelea kukigawa kile kilichopo ili kupunguza madhara kama ilivyofanya kwa madaktari.

“Serikali imesikia kilo chenu, tunaendelea kuyafanyia kazi, iko siku yote yatatimia, tunaongeza mishahara kidogokidogo ”.

Katika hotuba yake alifafanua kuwa, uwezo mdogo wa kiuchumi wa nchi ndio kikwazo kikuu cha kurudisha nyuma maslahi ya wafanyakazi nchini hali inayosababisha kiwango cha mishahara kutopanda ipasavyo.

Alisema mapato ya ndani ni sawa na trilioni 3.2 huku mishahara ya watumishi inachukua trilioni 6.7 hivyo kuwa na tofauti kubwa

Aliednela kufafanua kuwa mishahara pekee ya wafanyakazi nchini huchukuwa karibu asilimia 48 ya matumizi pekee
Wafanyakazi nchini wamekuwa wakiomba kupunguziwa kodi ya mapato kwani mishahara waipatayo na kiwango cha kodi ni vitu viwili tofauti

Huku wafanyakazi wakiendelea kulalama ugumu wa maisha kila kukicha huku ongezeko la bei kwa bidhaa ukipanda hali inayofanya maisha kuwa magumu mno kwa mshahara wa kima cha chini

Jumanne, 24 Aprili 2012

MWANAMKE AUNGUZWA MOTO WA PASI HUKO NIGERIA.


Wivu wa Mapenzi Amuunguza Kwa Pasi ya Moto Mkewe


NewsImages/6373006.jpg
Mke wa Henry baada ya kuunguzwa vibaya na moto wa pasi
Mwanaume mmoja wa nchini Nigeria anashikiliwa na polisi kwa kumuunguza na pasi ya moto mkewe sehemu mbali mbali za mwili wake zikiwemo sehemu zake za siri kwa kile kilichodaiwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na baba yake mzazi.
Mwanaume aliyejulikana kwa jina la Henry Nnamdi mkazi wa jiji la Lagos nchini Nigeria, alimuua mtoto wake mchanga kwa kukibamiza kichwa chake kwenye sakafu mpaka alipofariki.

Henry hakuishia hapo alimchukua mke wake wa ndoa yao ya miaka miwili na kumfunga na kamba kwenye kiti kabla ya kutumia pasi ya moto kumuunguza mkewe sehemu mbali mbali za mwili wake.

Henry alimuunguza vibaya mkewe kwenye matiti yake na sehemu zake za siri na sehemu mbali mbali za mwili wake kiasi cha kumfanya mkewe apoteze fahamu na hajazinduka hadi sasa.

Chanzo cha yote ni wivu wa Henry kuwa mkewe ana uhusiano wa kimapenzi na baba yake Henry na kwamba huyo mtoto wake mchanga si mtoto wa damu yake kibailojia.
Henry anamtuhumu baba yake mzazi kutembea na mkewe.

Tukio hilo lililoutikisa mji wa Lagos, lilitokea wakati wa sherehe za pasaka mwezi huu ambapo majirani wa kitongoji cha Okota walishtushwa usiku usingizini na kelele za kuomba msaaada za mke wa Henry aliyejulikana kwa jina moja la Nnamdi.

Mke wa Henry huku akilia kwa uchungu wa maumivu ya kuunguzwa na moto wa pasi, aliwaita majirani waje kumuokoa.

Baada ya majirani kusita sita kuingia ndani ya nyumba ya Henry, walilazimika kuvunja mlango na kuingia ndani baada ya kelele za maumivu za mke wa Henry kuzidi.

Waliyoyashuhudia ndani baadhi walishindwa kuyangaalia kwa mara ya pili waligeuza njia na kurudi walikotoka na kwenda kuwaita polisi.

Polisi waliwahi kufika na kumkuta mke wa Henry akiwa amezimia hajitambui na maiti ya mtoto wake mchanga ikiwa kwenye sakafu.

Henry alikamatwa na kutiwa mbaroni huku mkewe akiwahishwa hospitali ambako madaktari hadi sasa wanapigania maisha yake ingawa bado fahamu zake hazijamrudia.

Baba yake Henry amekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wa mwanae akisisitiza kuwa mwanae atakuwa amehisi hivyo kwakuwa siku zote alikuwa akimpinga tabia yake ya kumnyanyasa na kumpiga mkewe. Majirani wengi wanamuunga mkono baba yake Henry kuwa ni mtu mzuri na hawezi kumsaliti mwanae na kulala na mkewe.

Henry anaendelea kushikiliwa na polisi

Jumanne, 20 Machi 2012

MAMA NA WANAE WASAULA NGUO MBELE YA SHULE, WAKAMATWA NA POLISI.



NewsImages/6316130.jpg
Mama na wanae walipoamua kumwaga radhi shuleni
Tuesday, March 20, 2012 1:33 AMMama mmoja na wanae wa kike na wa kiume wanashikiliwa na polisi nchini Marekani baada ya kusaula nguo zao zote na kuanza kusali mbele ya shule wakiwa uchi wa mnyama.
Polisi wa kitongoji cha Upper Darby kwenye jimbo la Philadelphia nchini Marekani wanamshikilia mama mmoja na wanae kwa kusali uchi wa mnyama mbele ya shule.

Taarifa ya polisi wa Upper Darby ilisema kuwa mama huyo mwenye umri wa miaka 43 aliyejulikana kwa jina la Sara Butler akiwa na wanae wa kike Joanne mwenye umri wa miaka 23 na Bessie mwenye umri wa miaka 22 pamoja na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 14 walisaula nguo zao zote na kuanza kusali kwenye maegesho ya magari mbele ya shule.

Taarifa zaidi zilisema kuwa awali siku ya tukio, mama huyo na wanae walifika kwenye shule ya sekondari ya Upper Darby High School wakitaka kumuona mmoja wa wanafunzi wa kiume. Walikataliwa kukutana naye kwasababu mama huyo si mzazi wake.

Mama huyo na wanae waliondoka na kurudi baada ya lisaa limoja na kuanza kusaula nguo zao mbele ya maegesho ya magari wakisali kwa kusauti wakimtaja Yesu Kristo.

Ili waonekane vizuri mama huyo na wanae walijaribu kupanda juu ya gari walilokuja nalo lakini polisi walioitwa eneo la tukio waliwahi kuwatia nguvuni mama na wanae.

Mama huyo na wanae wanaozidi umri wa miaka 18 walifunguliwa mashtaka ya kuvunja maadili ya jamii na kujianika uchi hadharani

Ijumaa, 2 Machi 2012

MWANAJESHI WA MAREKANI ANYONYWA ULIMI HADHARANI,AIBU YA DUNIA.

Aibu ya Mwanajeshi wa Marekani Apakatwa, Anyonywa Ndimi na Mwanaume Mwenzake
  

  
Mwanajeshi huyo mwenye cheo cha Sajenti aliyejulikana kwa jina la Brandon Morgan aliruka na kutua kwenye kifua cha mpenzi wake mwanaume mwenzake na kumkumbatia na kuanza kunyonyana ndimi live live bila chenga.

Tukio hilo lilitokea nchini Marekani wakati wa sherehe za kuwakaribisha nyumbani wanajeshi wa Marekani waliokuwa wakipagana vita dhidi ya Taliban nchini Afghanistan.

Picha ya sajenti Morgan akiwa amemdandia mpenzi wake wa kiume akinyonyana naye ndimi imekuwa gumzo kubwa sana duniani.

Sajenti Morgan ambaye ni mkazi wa California hajakasirishwa na kusambaa kwa picha hiyo na badala yake amewashukuru baadhi ya watu waliompongeza na kuwatakia maisha mema yeye na mpenzi wake wa kiume.

Sheria ya Marekani ya kupiga vita ushoga na usagaji ilifutwa miezi mitano iliyopita hivyo kuwapa nafasi mashoga na wasagaji kujitangaza wazi bila woga.

Angalia picha ya sajenti Morgan akinyonyana ndimi na mpenzi wake ambaye ni mwanaume mwenzake

Jumanne, 3 Januari 2012

WAATHIRIKA WA MAFURIKO KUONDOLEWA KWENYE KAMBI ZA MASHULENI.

Mbunge wa Mafia Mh. Shaha akisaidia kuokoa waathirika wa mafuriko kwa Boti ya kukodi.


Hayo yamekuja ili kutakiwa kuwapisha wanafunzi wanaotarajiwa kufungua shule wiki ijayo nchini kote

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki, alimesema Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Mgulani na Mbweni, limetoa nafasi za kuhifadhi waathirika hao baada ya kuondolewa katika kambi za shuleni
Amesema Shirika la Msalaba Mwekundu limeahidi kutoa mahema ya kutosha kwa ajili ya kuhifadhi waathirika hao Mabwe Pande na wanatarajia kuyafunga katika eneo hilo ndani ya wiki hii.

Amesema mahema hayo yatawahusu wenye nyumba waliopoteza nyumba zao na zoezi hilo halitawahusu wapangaji na hao kutakiwa kutafuta maeneo na kuondoka katika kambi hizo

Shule zinatarajiwa kufunguliwa Januari 9 mwaka huu, ambapo zilifungwa katika likizo ndefu iliyoanza mwanzoni mwa mwezi Desemba

NIFAHAMISHE ilitembelea kambi hizo na kupata maoni ya waathirika hao ambao walikuwa wamepanga na kutakiwa kuondoka katika kambi hizo na kusema kuwa, serikali haiwatendei haki kwani wao pia ni waathirika na kuiomba serikali iwafikirie japo wka nkwuapa msaada kidogo

Wamesema kuondoka katika kambi hizo kwa sasa itakuwa ngumu kwani hawana pa kuanzia na kuiomba serikali iwasaidie japo msaaada wa kuwapa kodi za pango japo ya mwaka mmoja ilki waweze kupanga.

Jumapili, 18 Desemba 2011

AVUNJA REKODI YA MSICHANA MFUPI KULIKO WOTE DUNIANI.

Msichana mfupi kuliko wote duniani


NewsImages/6129114.jpg
Bibie Jyoti Amge akichukuliwa vipimo vya urefu wake.
Mwanafunzi wa Kihindi, Jyoti Amge, ni msichana aliyevunja rekodi ya dunia ya msichana mfupi kuliko wote duniani, kwa mujibu wa rekodi inayosajiliwa na kitabu cha rekodi cha Guinness.
Runinga ya NBC ya Marekani, siku ya Ijumaa 17/12/2011, imeripoti kuwa Jyoti Amge mwenye umri wa miaka kumi na minane 18, ana urefu wa sentimeta 62.8. sawa na inchi 24.7. Kwa hiyo msichana huyo ndio msichana mfupi kuliko wote duniani akiwa amempita msichana wa Kimarekani Bridgette Jordan mwenye umri wa miaka ishirini na miwili 22, ambaye ana urefu unaovuka ule wa Jyoti Amge kwa sentimeta saba 7. Kwa mujibu wa habari hiyo, Bridgette Jordan, alikuwa anashikilia rekodi hiyo tangu Septemba 2011.

Siku ya Ijumaa, Bibi Jyoti Amge, alikuwa anasherehekea siku yake ya kuzaliwa katika jiji la Nagpur. Wakati huo huo amenukuliwa akisema “Furaha ilioje kwa kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa kwa kutimiza miaka kumi na minane 18 nikishika rekodi mpya. Kwa kweli tukio hili ni zawadi ya nyongeza kwa sherehe ya kuzaliwa kwangu.”

Alhamisi, 3 Novemba 2011

DAKTARI TEMEKE AUAWA




DAKTARI MKUU MSAIDIZI wa Hospitali ya Temeke ya jijini Dar es Salaam, Kassim Kateta [43] ameuawa na watu wanadaiwa kuwa ni majambazi usiku wa jana
Kateta alifariki jana usiku majira ya saa 3 akiwa katika duka lake la kuza madawa linalotambulika kwa jina la Kotindi Pharmas lililopo jirani na hospitali hiyo

Kamanda wa Polisi Mkoa waTemeke, David Missime amesema kuwa, watu wawili ambao hadi sasa hawajafahamika ni akina nani walimvamia daktari huyo dukani kwake na kumuamuru atoe fedha na vitu vingine vya thamani

Kamanda huyo amesema kuwa ,kabla daktari huyo hajafanya chochote mmoja wao kati ya watu hao alimfyatulia risasi ya kifua daktari huyo na kutokea mgongoni kisha wao kutoweka na gari la daktari huyo

Kamanda huyo amesema jeshi hilo linafanya juhudi za kuwasaka watu hao pamoja na kuchunguza chanzo cha mauaji hayo ambacho hadi sasa haijafahamika

Jumanne, 1 Novemba 2011

ACHINJWA HADHARANI IKIWA NI ADHABU KWA KUFANYA UCHAWI.



NewsImages/6032714.jpg
Raia wa Sudan akichinjwa kwa kujishughulisha na uchawi
Tuesday, November 01, 2011 1:09 AMRaia wa Sudan aliyehukumiwa kuchinjwa nchini Saudi Arabia baada ya kupatikana na hatia ya kuwaroga watu amechinjwa hadharani kwenye maegesho ya magari.
Abdul Hamid bin Hussain bin Moustafa al-Fakki, raia wa Sudan mwenye umri wa miaka 36 aliyekuwa akiishi nchini Saudi Arabia amechinjwa kwa jambia baada ya kupatikana na hatia ya kujishughulisha na ushirikina.

Abdul alitiwa mbaroni tarehe 8 mwezi disemba mwaka 2005 baada ya kunaswa katika mtego wa polisi wa masuala ya dini kuhusiana na ushiriki wake katika masuala ya kishirikina.

Katika mtego huo, polisi mmoja wa kiume alimfuata Abdul na kumtaka amroge baba yake ili baba yake amuache mke wake wa pili.

Abdul alisema kuwa anaweza akafanya uchawi huo na alitaka alipwe Riyali za Saudi Arabia 6,000 ambazo ni sawa na dola 1600 za Marekani.

Abdul alitiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani akituhumiwa kujishughulisha na ushirikina.

Alipatikana na hatia na alihukumiwa adhabu ya kifo na mahakama ya mji wa Madina mnamo machi 27 mwaka 2007.

Abdul alichinjwa tarehe 19 mwezi septemba mwaka huu na ni wiki hii video za kunyongwa kwake zimeanza kuonekana kwenye mitandao.

Abdul alifungwa kitamba cheusi usoni na alipelekwa kwenye maegesho ya magari mbele ya umati wa watu. Pigo moja tu la jambia lilitosha kukitenganisha kichwa chake na kiwiliwili chake.

Abdul amekuwa mtu wa 44 kuchinjwa nchini Saudi Arabia mwaka huu na amekuwa raia wa kigeni wa 11 kuchinjwa mwaka huu.

Mtangazaji wa televisheni ya Lebanon, Ali Hussain Sibat, ambaye naye alitiwa mbaroni kwa kujishughulisha na utabiri wa mambo yajayo, amehukumiwa adhabu ya kifo na siku yeyote ile anaweza kuchinjwa.

Jumamosi, 15 Oktoba 2011

WANAWAKE WAWABAKA WANAUME HUKO ZIMBABWE, WAHITAJI MBEGU ZAO KWA USHIRIKINA.



NewsImages/6004758.jpg
Sophie Nhokwara mmoja wa wanawake watatu waliokamatwa kwa kuwabaka wanaume
Uchawi wa mpya umeibuka nchini Zimbabwe ambapo mbegu za uzazi za wanaume zimekuwa dili kiasi cha kundi la wanawake kuwabaka wanaume na kisha kuiba mbegu zao za kiume.
Wanaume kaeni chonjo sasa maana wanawake siku hizi nao wanabaka wanaume kama inavyotokea nchini Zimbwabwe ambapo wanaume wengi wamekuwa wakibakwa au kulazimishwa kufanya mapenzi na wanawake kinguvu ilimradi tu wanawake waweze kupata mbegu zao za kiume.

Kesi za wanaume kubakwa zimeripotiwa kwenye miji ya Gweru, Harare na Mashonaland.

Wanawake watatu wametiwa mbaroni kwenye mji wa Gweru kutokana na matukio ya kuwabaka wanaume waliyoyafanya hivi karibuni.

Wanawake hao watatu walikamatwa kwenye gari lao ambalo walikuwa wakilitumia kama chambo cha kuwavuta wanaume wakijifanya wanawapa lifti.

Ndani ya gari hilo kulikutwa jumla ya kondomu 33 ambazo zilikuwa na mbegu za kiume za wanaume mbalimbali ambao hadi sasa hawajajulikana.

Wanaume wanapokubali kupewa lifti, hutekwa kwa bunduki na kupelekwa sehemu za mbali ambako hulazimishwa kufanya mapenzi na wanawake hao kwa kutumia kondomu au wakati mwingi bila hata kinga huku wakiwa wameelekezewa bunduki. Baada ya hapo wanawake hukusanya mbegu za kiume na kisha huwatupa wanaume waliowateka pembeni ya barabara.

Wanawake waliotiwa mbaroni wametajwa kuwa ni Rosemary Chakwizira mwenye umri wa miaka 24, Sophie Nhokwara mwenye umri wa miaka 26, na Netsai Nhokwara ambaye naye pia ana umri wa 24, wote ni wakazi wa Gweru. Pia dereva wao mwanaume naye ametiwa mbaroni kwa makosa ya kufanya shambulizi nje ya maadili. Dereva huyo pia anatuhumiwa kesi ya mauaji baada ya kumuua kwa kumgonga kwa gari mtoto na kisha kukimbia.

Inasemekana kuwa wanawake hao wamekuwa wakizikusanya mbegu za kiume za wanaume wanaowateka na wamekuwa wakizitumia mbegu hizo za kiume kwenye mambo ya kishirikina.

Wakazi wa Gweru hawakuamini masikio yao pale majina ya wanake hao yalipotajwa kuwa wanabaka wanaume.

"Wanawake hawa wanajulikana sana hapa kwakuwa wamekuwa wakionekana kwenye kumbi za starehe mara kwa mara", alisema mmoja wa wakazi wa Gweru.

Mkazi mwingine wa Gweru aliyejitambulisha kwa jina la Harry Mohammed Misi aliiambia redio moja nchini Zimbabwe "Tumeshtushwa sana na haya yanayotokea kwenye jamii yetu, wanaume sasa nao wanabakwa na wanawake, inaonekana sasa mambo yamebadilika".

Polisi wa Zimbabwe wamesema kuwa watatumia DNA ili kugundua mbegu kiume za wanaume waliobakwa na wanawake hao

Alhamisi, 13 Oktoba 2011

NYUMBA YA JAMBAZI SUGU YACHOMWA MOTO.

NewsImages/6001866.jpg
Nyumba ikitekea kwa moto.

Ile nyumba ya jambazi maarufu katika mkoa wa Iringa yateketezwa kwa moto na wanachi wa eneo hilo la kigamboni. Jambazi hilo kwa jina Msafiri Ilomo alikuwa akitumia nyumba hiyo kama ghala la kuhifadhia vitu vya wizi.
Ile nyumba ya jambazi maarufu katika mkoa wa Iringa yateketezwa kwa moto na wanachi wa eneo hilo la kigamboni.

Jambazi hilo kwa jina Msafiri Ilomo alikuwa akitumia nyumba hiyo kama ghala la kuhifadhia vitu aina mbalimbali ambavyo alikuwa akivinyang'anya kwa njia nguvu na vitisho ukiwa mbishi hutumia nondo kwa kumchapa binadamu mwenzie mbavuni au kichwani.

Baada ya nyumba hiyo kuteketezwa na moto jopo la wananchi walionekana wakibeba vitu vya aina malimbali kwa njia isiyo halali katika eneo hilo na kutokomea kusikojulikana.

Mheshimiwa Amani Mwamwindi ambaye ndiye meya wa Manispaa ya Iringa alifika katika eneo hilo na kushuhudia vitu vya aina mbalimbali vlivyoporwa kutoka kwa wananchi.

Mstahiki meya alisema kabla ya kukubaliana na wananchi juu ya uvunjaji wa chumba hiyo alilitaka jeshi la Polisi kuchukua mali zote kutoka kwenye nyumba hiyo,ambapo polisi wa usalama walikuwepo hapo kwa muda huo.

Tayari watu zaidi ya wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa na jambazi hilo kwa kutumia nondo, katika hali ya kusikitisha zaidi jambazi hilo lilikuwa likiwabaka Wanawake mbalimbali.

Mheshimiwa Mwamwindi alisema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa juu ya tukio hilo la ujambazi katika kata hiyo ya Mwangata ambao wananchi wengi walikuwa wakiishi kwa hofu kubwa kwa kipindi kirefu zaidi.

Meya aliendelea kusema kijana Damas Kisinga amepoteza maisha kwa kupingwa na Nondo na kundi hilo la kijambazi ,kijana huyo Damas alizikwa juzi katika eneo la Makanyagio.

Majambazi hayo yalishindwa kabisa mbinu zao baada ya kuzungukwa na wananchi wakati walipovamia nyumba ya diwani wa Kata ya Mkwawa Thobias Kikula.

Mpaka sasa majeruhi waliopigwa na nondo na kukatwa na mapanga ni Michael Chengula 37 aliyevujwa mkono kabla ya kuchukuliwa simu na fedha taslimu laki moja na Mpiga picha Adilian Lusasi 45 aliyeporwa kamera yake pamoja na picha za wateja wake.

Diwani Lugenge alisema jambazi huyo alikuwa amefunga dishi la DSTV kitu ambacho wananchi wameona si cha kawaida katika nyumba hiyo ya udongo na kuitilia mashaka na kuivamia.

Bwana Lugenge aliendelea kusema takribani mwezi mmoja sasa tangu jambazi hilo lifiwe na mtoto wake ambaye aliweza kumzika kwa siri na msiba aliupeleka wa wazazi wake kwa kuhofia wananchi kujua siri kubwa ndani ya nyumba yake.

Mpaka sasa vitu vilivyokwisha kamatwa ni Nguo,Visu,DVD,TV,Sofa,Magodoro,Baiskeli,Mabati na simu aina mbalimbali, Vitanda, Vyombo vya makanisani na misikitini na mali nyingine nyingi ambazo zilijaa ndani ya chumba hiyo.

Kwa sasa vitu hivyo vipo mikononi mwa jeshi la polisi Iringa.

Jumatatu, 3 Oktoba 2011

MATOKEO UCHAGUZI IGUNGA KUTANGAZWA MUDA WOWOTE KUANZIA SASA, VINARA NI CHADEMA NA CCM.

Hadi habari hii inarushwa matokeo hayo bado hayajatangazwa huku ikileta shauku kwa wapenda siasa nchini kutokana na jimbo hilo kujaa mbwembwe na vituko vya kila aina wakati wa kampeni zilizohitimishwa juzi na kura kupigwa jana.

Katika matokeo hayo taarifa za awali zinaonyesha mchuano mkali kati ya CCM na CHADEMA ambapo vyama hivyo vinaonyesha kuwa kidedea katika baadhi ya matokeo ya kata wilayani humo.

Matokeo hayo ya awali, yalikuwa yamebandikwa kwenye vituo vya kupigia kura muda mfupi baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika.

Jimbo la Igunga lina kata 26 na lina jumla ya wakazi 325,000 na wapiga kura 171,265 walijiandikisha kupiga kura

Uchaguzi huo, unafanyika kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz, aliyejiuzulu Julai 13 mwaka huu.

Rostam alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 15 mfululizo kuanzia mwaka 1994 na alijiuzulu kwa kile alichodai anaachana na siasa uchwara ndani ya chama hicho.

Vyama nane vimeshiriki kwenye uchaguzi huo na kusimamisha wagombea wao ambapo [CCM] ilimsimamisha Dk.Peter Kafumu , [CHADEMA] ilimsimamisha Mwalimu Kashindye, [CUF] ilimsimamisha Leonard Mahona

Said Cheni (DP), Hemed Dedu (UPDP), Hassan Rutegama (Chausta), John Maguma (Sau) na Steven Making.

Muda wowote kuanzia sasa matokeo hayo yanaweza yakatangazwa

Jumapili, 2 Oktoba 2011

MSEMAJI WA ILIYOKUWA SERIKARI YA LIBYA AKAMATWA.


NewsImages/5980658.jpg
Moussa Ibrahim
Msemaji maarufu wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi amekamatwa na waasi wakati akijaribu kuukimbia mji wa Sirte akiwa amevaa nguo za kike.
Msemaji wa Gaddafi, Moussa Ibrahim, ametiwa mikononi mwa wanajeshi wa serikali ya waasi baada ya kukamatwa akiwa amevaa nguo za kike ili asitambulike.

Imeripotiwa kuwa Ibrahim alikuwa akijaribu kutoroka mapambano makali yanayoendelea katika mji wa Sirte kati ya wanajeshi wa Gaddafi na wanajeshi walioipindua serikali yake.

Wanajeshi wengi wa Gaddafi wako kwenye mji wa Sirte ambao ndiko alikozaliwa Gaddafi. Mji huo umezungukwa pande zote na wanajeshi wanaipinga serikali ya Gaddafi.

Ibrahim alikamatwa ndani ya gari akiwa amevaa hijabu akijaribu kutoroka mji wa Sirte.

Ibrahim alijipatia umaarufu duniani kwa kuwa msemaji mkuu wa serikali ya Libya wakati waasi walipoanza kuandamana na kufanya mashambulizi ya kuipinga serikali ya kanali Gaddafi.

Alijulikana sana kwa mashirika ya habari ya kigeni ambapo alikuwa akivikusanya vyombo vya habari kwenye hoteli ya Rixos Hotel ya jijini Tripoli na kumwaga sera za kuiunga mkono serikali ya Gaddafi. Alikuwa akitoa taarifa za msimamo wa Gaddafi na kulaani mashambulizi ya NATO nchini Libya akisema kuwa NATO na nchi za magharibi haziitendei haki Libya.

Ilikuwa haijulikani Ibrahim amejificha wapi hadi jana alipokamatwa.

Hadi sasa mapambano yanaendelea kuiteka miji michache inayomuunga mkono Gaddafi.

Gaddafi mwenyewe hadi sasa hajulikani yuko wapi ingawa familia yake imekimbilia kwenye nchi za Algeria na Niger.

Jumanne, 27 Septemba 2011

MTOTO MWENYE SURA MBLI AZALIWA PAKISTAN, MUNGU MKUBWA.


NewsImages/5968126.jpg
Mtoto mwenye sura mbili aliyezaliwa nchini Pakistan
Mamia ya watu wamekuwa wakimiminika kwenye wadi ya wazazi ya hospitali moja nchini Pakistan ili kumshuhudia mtoto mwenye kichwa chenye sura mbili aliyezaliwa juzi nchini humo.
Mtoto huyo alizaliwa usiku wa kuamkia ijumaa akiwa na kichwa kimoja chenye sura mbili tofauti.

Mtoto huyo aliyezaliwa kwa njia ya kawaida bila ya operesheni alikuwa na uzito wa kilo 3.2. Alizaliwa kwenye mji wa Palandri uliopo Azad Kashmir nchini Pakistan.

Hali aliyo nayo mtoto huyo inajulikana kitaalamu kama "Craniofacial duplication" ambapo kichwa chake kilikuwa na sura mbili ambapo alikuwa na midomo miwili, macho manne, pua mbili isipokuwa tu alikuwa na masikio mawili tu.

Ana ubongo mmoja na kwajinsi maumbile yake yalivyoungana madaktari wanasema kuwa ni vigumu sana kumfanyia operesheni ya kurekebisha sura yake ili awe sawa na watoto wengine.

Daktari wa hospitali ya HFH aliyozaliwa mtoto huyo aliyejitambulisha kama daktari Nasira, alisema kuwa wana matumaini madogo sana mtoto huyo ataishi muda mrefu kwani hadi sasa anashindwa kupumua vizuri na analishwa kwa kutumia mrija.

"Tuna matumaini madogo ya kunusuru maisha ya mtoto huyu", alisema daktari Nasira.

Mtoto huyo alizaliwa katika familia ya bwana Khalil Ahmed na mkewe Shahida Perveen ambao wana watoto watatu waliozaliwa bila ya kuwa na dosari yoyote kwenye maumbile yao.

Mama wa mtoto huyo bado amelazwa hospitali pamoja na mtoto wake ambaye amelazwa kwenye kitengo maalumu akipatiwa matibabu maalumu ya kunusuru maisha yake

Jumatano, 14 Septemba 2011

JAMAA AKOJOA MAHAKAMANI, HAKIMU ASHANGAA.


NewsImages/5949810.jpg
Wednesday, September 14, 2011 2:07 AMDalili za kesi kwenda vibaya zilianza kuonekana pale mshtakiwa mmoja wa nchini Marekani alipoamua kukojoa mahakamani na kumfanya hakimu amuambie 'Sijui ulivyolelewa, unaonyesha tabia mbaya mahakamani'.
Kijana mweusi mwenye umri wa miaka 17 wa nchini Marekani alimuudhi hakimu pale alipoamua kusaula nguo zake na kukojoa mahakamani mbele ya umati wa watu waliokuwepo mahakamani kusikiliza kesi hiyo.

Kijana huyo aliyetajwa kwa jina la Corey Webb alifikishwa mahakamani kwa kumpiga risasi afisa wa polisi wakati alipokuwa akiwazuia kutoroka toka kwenye jela ya watoto.

Webb kabla ya kuamua kukojoa mahakamani alikuwa akifanya vituko mbali mbali kama vile kupiga kelele wakati akisomewa mashtaka yake. Aliwashangaza watu alipomtaka hakimu amfukuze wakili aliyekuwa akimtetea.

"Sijui umelelewaje lakini kukojoa kwenye pipa la taka ndani ya mahakama ni tabia mbaya", alisema jaji huyo baada ya Webb kuteremsha nguo zake na kukojoa ndani ya mahakama.

Kesi iliahirishwa hadi siku nyingine

Jumatatu, 15 Agosti 2011

EWURA YASALIMU AMRI KWA WAFANYABIASHARA.


EWURA Yasalimu Amri, Yapandisha Bei ya Mafuta

NewsImages/5881366.jpg
Godwin Samwel, Meneja Biashara Ewura alipokuwa akitoa taarifa mbele ya vyombo vya habari jana
Monday, August 15, 2011 3:52 PMBAADA ya kumalizika kwa mgomo ambao umetingisha jiji na mikoa tofauti hapa nchini kwa ajili ya kupunguzwa kwa bei,jana Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeongeza tena bei ya mafuta inayoanzwa kutumika leo
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Meneja Biashara Ewura,Bw. Godwin Samwel alisema wamepandisha bei ya mafuta kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania katika soko la dunia

Bei hizo zimebainishwa kuwa petroli imepanda na kufikia Sh. 100.34 , dizeli Sh. 120.47 na mafuta ya taa kwa Sh 100.87 hizo ni bei kwa lita moja

Amesema kuwa bei hizo mpya zinaonyesha bei ya nishati hiyo katika soko la dunia kupanda kwa wastani wa asilimia 5.42, huku thamani ya shilingi ya Tanzania ikiwa imeshuka kwa Sh 47.12 sawa na asilimia 2.96 kwa dola moja ya Marekani.

Mbali na kutoa bei hiyo mpya pia aliwaagiza wauzaji wa mafuta nchini kuuza bei elekezi na isizidi bei hiyo kwani wanaweza kuuza bidhaa za mafuta kwa bei ya ushindani alimradi bei hizo zisivuke kikomo.

Wakati huohuo mkoani Dodoma Wilayani Mpwapwa imeripotiwa kuwa siku ya tatu leo hakuna mafuta katika vituo vitoavyo huduma hiyo kwa madai ya kutokuwepo kwa mafuta hayo.

Chanzo: www.nifahamishe.com

Jumanne, 2 Agosti 2011

MWANAUME AKUTWA NA VIA VYA UZAZI VYA KIKE.



Mkulima mmoja wa nchini India ambaye pia ni baba wa watoto wawili amewashangaza madakatri baada ya kugundulika mbali ya kuwa ni mwanaume rijali tumboni mwake ana viungo vyote vya kike vya kumuwezesha mwanamke kupata ujauzito.
Mkulima huyo aliyetambulika kwa jina la Ryalu aliwahishwa hospitali baada ya kusumbuliwa na maumivu ya tumbo.

Wakati madaktari wakimfanyia upasuaji wakidhani anasumbuliwa na ugonjwa wa kidole cha tumbo, walipigwa na butwaa walipogunudua mwanaume huyo ana mfumo kamili wa uzazi wa kike.

Tumboni mwake mbali ya kwamba kulikuwa na mfumo kamili wa uzazi wa kiume pia kuligundulika kuna mfumo kamili wa uzazi wa kike kukiwa na mji wa mimba, mayai ya uzazi ya kike, nyonga, mirija ya fallopian na tishu za sehemu ya siri ya kike.

Madaktari wa hospitali katika mji wa Bhopal, Madhya Pradesh, walishangazwa kugundua viungo hivyo vya uzazi vya kike vikiwa kwenye sehemu ya chini ya tumbo la Ryalu.

Daktari Pramod Kumar Shrivastava, wa hospitali hiyo alisema kwamba Ryalu kwa nje hana tofauti na wanaume wengine, alikuwa na viungo vyote vya uzazi vya kiume na alikuwa akiishi maisha ya kawaida kama mkulima.

"Tumeviondoa viungo vyote vya uzazi vya kike na hivi sasa anaendelea vizuri", alisema daktari Shrivastava.

Taarifa zaidi ziliongeza kwamba Ryalu hakuwahi kusumbuliwa na matatizo yoyote ya tumbo hadi hivi karibuni alipokumbwa na maumivu makali tumboni na kuwahishwa hospitali.

"Hana matatizo yoyote ya kijinsia, homoni zake zote ni za kiume na hana matiti kwenye kifua chake", aliongeza dakati mwingine wa hospitali hiyo

Jumatano, 13 Julai 2011

MWANAUME AKATWA UUME HUKO MAREKANI.



Kieu Becker
Wednesday, July 13, 2011 10:52 PMStaili ya wanawake kuwaadhibu wapenzi wao kwa kuzikata sehemu zao za siri imeendelea nchini Marekani ambapo mwanamke mmoja nchini humo amejikuta akitupwa rumande kwa kuukata kwa kisu uume wa mume wake na kisha kuusagasaga kwa mashine.
Mwanamke mmoja wa California nchini Marekani amejikuta akitupwa rumande baada ya kumlisha madawa ya kulevya mumewe, kumfunga kwa kamba na kisha kuukata uume wake kwa kisu na ili kuhakikisha kipande hicho cha uume hakitaungwa tena na madaktari alikidumbukiza kipande hicho cha uume kwenye mashine ya kusaga uchafu.

Taarifa ya polisi ilisema kwamba siku ya jumatatu usiku, mwanamke huyo aliyetajwa kwa jina la Kieu Becker mwenye umri wa miaka 48, alimuandalia mumewe chakula ambacho alikiwekea madawa ya kulevya.

Mumewe mwenye umri wa miaka 51 ambaye jina lake halikutajwa, alijihisi vibaya baada ya kula chakula hicho na haukupita muda mrefu alipoteza fahamu.

Kieu alimburuza mumewe na kumlaza kitandani ambapo alimvua nguo zake zote na kisha kuifunga mikono na miguu yake kwenye kitanda.

Kieu alisubiri mumewe apate fahamu kabla ya kuanza kumshambulia kwa kisu chenye urefu wa sentimita 25.4.

"Alikuwa ameishazinduka wakati uume wake ulipokatwa", alisema msemaji wa polisi.

Taarifa ya polisi ilisema kwamba Kieu alikichukua kipande cha uume wa mumewe na kukiweka kwenye mashine ya umeme ya kusaga taka ambayo huwekwa chini ya sinki la maji kwenye majumba mengi ya Marekani.

Baada ya kuhakikisha kipande hicho cha uume kimesagwasagwa sana kiasi cha kuwa vipande vidogo vidogo, Kieu alipiga simu polisi na kuwajulisha kilichojiri. Polisi walipofika walimkuta mumewe akiwa bado kitandani mikono na miguu yake ikiwa imefungwa kwa kamba, alikuwa akivuja damu sana.

Kieu alitupwa rumande akifunguliwa mashtaka ya kufanya ukatili, kuteka mtu na kumlewesha mtu kwa madawa ya kulevya ili kufanya kosa la jinai. Ili aachiwe huru kwa dhamana, Kieu alitakiwa kutoa dola milioni moja.

Mume wa Kieu aliwahishwa hospitali ambapo alifanyiwa operesheni ili kuokoa maisha yake. Ingawa hali yake bado ni mbaya sana, madaktari wanaamini mwanaume huyo atapona.

Kieu hakuleta upinzani wowote wakati alipokuwa akitiwa mbaroni na atapandishwa kizimbani siku ya jumatano.

Taarifa zaidi zilisema kwamba Kieu na mumewe walifunga ndoa mwezi disemba mwaka jana na walikuwa kwenye harakati za kuivunja ndoa yao ingawa sababu ya mgogoro kwenye ndoa yao haikujulikana.