Jumanne, 1 Novemba 2011

ACHINJWA HADHARANI IKIWA NI ADHABU KWA KUFANYA UCHAWI.



NewsImages/6032714.jpg
Raia wa Sudan akichinjwa kwa kujishughulisha na uchawi
Tuesday, November 01, 2011 1:09 AMRaia wa Sudan aliyehukumiwa kuchinjwa nchini Saudi Arabia baada ya kupatikana na hatia ya kuwaroga watu amechinjwa hadharani kwenye maegesho ya magari.
Abdul Hamid bin Hussain bin Moustafa al-Fakki, raia wa Sudan mwenye umri wa miaka 36 aliyekuwa akiishi nchini Saudi Arabia amechinjwa kwa jambia baada ya kupatikana na hatia ya kujishughulisha na ushirikina.

Abdul alitiwa mbaroni tarehe 8 mwezi disemba mwaka 2005 baada ya kunaswa katika mtego wa polisi wa masuala ya dini kuhusiana na ushiriki wake katika masuala ya kishirikina.

Katika mtego huo, polisi mmoja wa kiume alimfuata Abdul na kumtaka amroge baba yake ili baba yake amuache mke wake wa pili.

Abdul alisema kuwa anaweza akafanya uchawi huo na alitaka alipwe Riyali za Saudi Arabia 6,000 ambazo ni sawa na dola 1600 za Marekani.

Abdul alitiwa mbaroni na kufikishwa mahakamani akituhumiwa kujishughulisha na ushirikina.

Alipatikana na hatia na alihukumiwa adhabu ya kifo na mahakama ya mji wa Madina mnamo machi 27 mwaka 2007.

Abdul alichinjwa tarehe 19 mwezi septemba mwaka huu na ni wiki hii video za kunyongwa kwake zimeanza kuonekana kwenye mitandao.

Abdul alifungwa kitamba cheusi usoni na alipelekwa kwenye maegesho ya magari mbele ya umati wa watu. Pigo moja tu la jambia lilitosha kukitenganisha kichwa chake na kiwiliwili chake.

Abdul amekuwa mtu wa 44 kuchinjwa nchini Saudi Arabia mwaka huu na amekuwa raia wa kigeni wa 11 kuchinjwa mwaka huu.

Mtangazaji wa televisheni ya Lebanon, Ali Hussain Sibat, ambaye naye alitiwa mbaroni kwa kujishughulisha na utabiri wa mambo yajayo, amehukumiwa adhabu ya kifo na siku yeyote ile anaweza kuchinjwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni