Jumanne, 1 Novemba 2011

KESI YA JERRY MURRO NA WENZIE KUHUKUMIWA MWISHONI MWA NOVEMBA HII.

HUKUMU ya kesi inayomkabili aliyekuwa mtangazaji wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC1), Jerry Muro na wenzake inatarajiwa kutolewa mwishoni mwa mwezi huu
.
Murro na wenzake ambao wanadaiwa kula njama na kuomba rushwa ya Sh milioni 10, watahukumiwa Novemba 30 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salam ambako kesi hiyo inaendeshwa.


Jerry Murro katikati akiwa na askari kanzu(picha na maktaba).


Jana kesi hiyo ilitajwa na kupangiwa tarehe ya hukumu mbele ya Hakimu Frank Mosha . Pande zote, mashitaka na utetezi zimekwisha wasilisha majumuisho yao.

Upande wa utetezi uliwasilisha majumuisho Oktoba 21 mwaka huu na upande wa Jamhuri uliwasilisha majumuisho Oktoba 28 mwaka huu ukiiomba mahakama iwaone washitakiwa kuwa wana hatia.

Hakimu Mosha alisema “Kwa kumbukumbu za mahakama pande zote mbili zimeshawasilisha majumuisho yao na hivyo tupange tarehe ya hukumu ambayo ni mwezi mmoja kuanzia sasa,”.


Februari 5 mwaka jana, Muro, Edmund Kapama na Deogratius Mugasa walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na makosa kula njama, kuomba rushwa na kujifanya wao ni watumishi wa serikali.


Muro peke yake anakabiliwa na makosa ya kula njama na kuomba rushwa, wakati Mugasa na Kapama wanakabiliwa na mashtaka yote matatu.


Wanadaiwa kutaka kupokea rushwa hiyo kutoka kwa aliyekuwa Mhasibu wa Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni