Hadi habari hii inarushwa matokeo hayo bado hayajatangazwa huku ikileta shauku kwa wapenda siasa nchini kutokana na jimbo hilo kujaa mbwembwe na vituko vya kila aina wakati wa kampeni zilizohitimishwa juzi na kura kupigwa jana.
Katika matokeo hayo taarifa za awali zinaonyesha mchuano mkali kati ya CCM na CHADEMA ambapo vyama hivyo vinaonyesha kuwa kidedea katika baadhi ya matokeo ya kata wilayani humo.
Matokeo hayo ya awali, yalikuwa yamebandikwa kwenye vituo vya kupigia kura muda mfupi baada ya zoezi la kuhesabu kura kukamilika.
Jimbo la Igunga lina kata 26 na lina jumla ya wakazi 325,000 na wapiga kura 171,265 walijiandikisha kupiga kura
Uchaguzi huo, unafanyika kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Rostam Aziz, aliyejiuzulu Julai 13 mwaka huu.
Rostam alikuwa mbunge wa jimbo hilo kwa miaka 15 mfululizo kuanzia mwaka 1994 na alijiuzulu kwa kile alichodai anaachana na siasa uchwara ndani ya chama hicho.
Vyama nane vimeshiriki kwenye uchaguzi huo na kusimamisha wagombea wao ambapo [CCM] ilimsimamisha Dk.Peter Kafumu , [CHADEMA] ilimsimamisha Mwalimu Kashindye, [CUF] ilimsimamisha Leonard Mahona
Said Cheni (DP), Hemed Dedu (UPDP), Hassan Rutegama (Chausta), John Maguma (Sau) na Steven Making.
Muda wowote kuanzia sasa matokeo hayo yanaweza yakatangazwa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni