Friday, October 14, 2011 2:18 AMMwanamke mwenye umri wa miaka 54 wa nchini Marekani aliwahishwa hospitali baada ya kupoteza kumbukumbu ya muda mfupi wa maisha yake baada ya kumaliza tendo la ndoa na mumewe. | ||
Mwanamke huyo ambaye jina lake halikutajwa aliwasili kwenye hospitali ya jijini Washington nchini Marekani akiwa amekumbwa na mshtuko mkubwa kwa kupoteza kumbukumbu ya mambo yote yaliyotokea katika maisha yake kwa masaa 24 yaliyopita. Hali hiyo ilimtokea mwanamke huyo baada ya kupewa malavi davi ya nguvu na mumewe kiasi cha kupelekea apoteze kumbukumbu. Madaktari waliohojiwa kutokana na hali ya mwanamke huyo walisema kuwa mwanamke huyo alisumbuliwa na ugonjwa unaojulikana kitaalamu kama "transient global amnesia" ambayo huufanya ubongo upoteze kumbukumbu kwa muda mfupi. Ugonjwa huo hausababishi madhara kwa ubongo lakini huweza kumsababishia mtu kuwa mwenye stress sana. Hali iliyomtokea mwanamke huyo iliripotiwa kwenye jarida la Journal of Emergency Medicine, ambapo ilielezwa kuwa hali kama hiyo humtokea mtu mmoja katika kila watu 100,000 kila mwaka. Hali hii imeelezwa kuwa mara nyingi hutokea pale mtu anapoufanyisha mwili wake mazoezi mengi kuliko kawaida au kufanya kitu kinachouchosha sana mwili |
KARIBU KATIKA BLOGU HII YA KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUONYA KUPITIA MADA MBALIMBALI NA HATA PICHA. ONGEZA MAHUSIANO KWA KUJUMUIKA NA WENZIO HAPA.UNAWEZA TUMA PICHA NA MAELEZO KWA ANUANI HII;mkuu74@gmail.com
Ijumaa, 14 Oktoba 2011
APOTEZA KUMBUKUMBU BAADA YA KUFANYA MALAVIDAVI YA NGUVU.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni