'Daktari Asiyeweza Kazi Aachie Ngazi ' - JK | ||
Rais Jakaya Kikwete | RAIS Kikwete amesema serikali haina uwezo wa kulipa kiwango cha mshahara cha Sh.Mi.3.5 wanachokitaka kulipwa madaktari | |
Na kuwataka madaktari ambao hawataridhika na kiwango kilichowekwa waachie ngazi na wakatafute mwajiri atakayekuwa na uwezo wa kuwalipa kiasi hicho Rais Kikwete aliyasema hayo pia katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi kupitia vyombo vya habari Rais Kikwete amesema, Serikali kwa sasa haiwezi kuwaahidi madaktari kima hicho kwani ikifanya hivyo malipo ya daktari anayeanza kazi yatakuwa ShMil. 7.7 kwa mwezi kitu ambacho hakiwezekani. Mwisho alimalizia kwa kusema “nawasihi madaktari kuacha mgomo warejea kazini, kwani Watanzania wanateseka na kupoteza maisha kwa kukosa maatibabu”. Wakati huohuo,Uongozi wa Taasisi ya Mifupa (MOI) umebandika tangazo linalosema na kuwataka madaktari wanaotaka kuendelea na kazi wakajisajili kwa Mkurugenzi wa Tiba Tangazo hilo lilifanua kuwa madaktari watakaotaka kuendelea na kazi kujisajili ni mwisho leo |
KARIBU KATIKA BLOGU HII YA KUELIMISHA, KUBURUDISHA NA KUONYA KUPITIA MADA MBALIMBALI NA HATA PICHA. ONGEZA MAHUSIANO KWA KUJUMUIKA NA WENZIO HAPA.UNAWEZA TUMA PICHA NA MAELEZO KWA ANUANI HII;mkuu74@gmail.com
Jumatatu, 2 Julai 2012
RAIS KIKWETE ATOA MSIMAMO KUHUSU MADAKTARI.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni